realMamy
JF-Expert Member
- Apr 28, 2024
- 3,925
- 8,853
MY STORY: Nilisema nitamchukua Bada ya miaka 7 nimeenda nimekutana na Makaburi mawili!
Nakumbuka meseji yangu ya mwisho niliyomtumia ilikuwa ni kumwambia, "Wewe lea mtoto, akiwa mkubwa atakuja kunitafuta," na kwa taarifa yako, akifikisha miaka 7 nitakuja kumchukua. Hakunijibu hiyo meseji na mimi sikuwahi kumtafuta tena, nilikaa kimya kwa miaka 8 na katika maisha yangu yote kila nikiingia kwenye mahusiano nilikuwa nikimwambia mwanamke kuwa kuna mwanamke nilimezaa naye anang'ang'ania mtoto ila mtoto akikua nitakuja kumchukua.
Mwaka jana niliingia kwenye ndoa na nilijua mtoto wangu sasa atakuwa amefikisha miaka 9 naweza kwenda kumchukua na kuishi naye kama familia. Niliazimia kumtafuta X wangu. Nilihangaika kumtafuta mitandaoni lakini picha yake ya mwisho niliyoiona ilikuwa imepostiwa miaka 6 iliyopita, na ilikuwa ni picha akiwa na mtoto wangu mdogo. Nilimtumia meseji Facebook nikiamini kuwa, labda bado anatumia hiyo akaunti, lakini kwa miezi 3 haikujibiwa. Sikuweza kuwatafuta ndugu zake kwa jinsi nilivyokuwa nawafahamu nilijua isingekuwa rahisi.
Niliamua kwenda sehemu alipopokuwa anafanya kazi, hakuwa na kazi ya maana kihivyo, kuna duka alikuwa anauza lakini nilipofika huko hata mwenye duka alikuwa ameondoka. Katika kufikiria, ndipo nikakumbuka aliniambia kuwa kijijini kwao ni Rombo huko, nikakumbuka kile kijiji na kuamua kwenda huko nikiamini kwa kuwa najua jina la baba yake kijijini itakuwa rahisi kumpata.
Kweli nilijipanga nikaweka na pesa kidogo ya kutoa faini na nilipoenda huko haikuchukua muda nilipomuulizia yule mzee nilielezwa kuwa alifariki, lakini nikaonyeshwa nyumbani kwake. Nilifika nikakutana na mama yake, mtu mzima kidogo, ingawa hakuwa amewahi kuniona lakini ile tu kuniona siku ile alitambua kuwa mimi ni nani.
Baba Hanna (sio jina halisi) aliniita tu baada ya kuniona. Nilipata mshtuko wa ajabu, alijuaje ila ukweli mtoto wangu ingawa alikuwa ni wa kike lakini tulifanana sana, alichukua karibu kila kitu changu. Alinikaribisha vizuri, nikasalimia, na baada ya muda nikaanza kuomba msamaha kwa kuchelewa kurudi na kuniulizia mama wa mtoto wangu.
Alinijibu kwa kifupi tena bila kupaniki, akaniambia yuko hapo nje, moyo ulinipiga paaap! Kumbe yupo! Nikamuulizia na mtoto wangu akaniambia wote wako hapo nje, unataka kuwaona? Nilishtuka kidogo lakini nikamjibu ndiyo, akanyanyuka kwa taabu kwani alikuwa mtu mzima sana na miguu ilionysha kumuuma na kunambia, "Twende uwaone," tukatoka nje kidogo akaonesha sehemu ya hatua 20 hivi kisha akaniambia, "Hapo hapo, mtoto wangu huyo hapo kalala tangu mwaka juzi na binti yako huyo hapo kalala ni wiki ya pili sasa. Ndiyo maana unaona kaburi lake bado jipya jipya."
Nguvu ziliniishia nikajikuta nakaa chini, nilishindwa cha kuongea. Mama hakujali, alinyanyuka na kurudi ndani. Nilikaa pale kaburini kwa takribani masaa mawili, nipo tu, mama yake hakutoka wala hakuongea chochote. Kisha nikaamka na kurudi ndani, nikamuuliza mama, naomba uniambie nini kimetokea.
Sijui nini kilitokea huko mjini, lakini binti yangu alikuja na mtoto mdogo, akaja kuishi hapa kijijini. Pamoja na maisha magumu, alihangaika sana kulea mtoto wake huku akimsomesha shule nzuri kwa kufanya vibarua na kuuza vitu sokoni. Mume wangu ndiyo alitangulia na binti yangu yeye alifuata.
Ilikuwa ni ajali ya bodaboda, Mungu akamchukua. Nikabaki mimi na mjukuu wangu, maisha kama unavyojua nina watoto 5 lakini huyu aliyetangulia ndiye alikuwa kila kitu. Basi baada ya kufariki kila kitu kilikuwa shida, mjukuu wangu licha ya kusoma, nikamrudisha shule za kawaida, chakula kilikuwa cha shida kwani wajomba zake ni watu wa pombe tu, hata ukikaa hapa nusu saa utawaona wameharibikiwa.
Baada ya mama yake kufariki mambo yalikuwa magumu sana, mimi unaona hali yangu siwezi hata kutoka nje kuzunguka kufanya kibarua, hivyo nilikuwa napika maandazi humu ndani, mjukuu wangu ndiye anayesambaza. Alikuwa ananisaidia sana lakini siku moja alikwenda kuzungusha mandazi jioni na kupeleka madukani kama kawaida lakini hakurudi tena. Usiku tulimsubiri hakurudi, tulihangaika ili arudi lakini hakurudi, alikuja kuokotwa kwenye mtaro asubuhi ya kesho yake akiwa tayari amefariki. Sijui nini kilichomu*ua mjukuu wangu lakini ndiyo hivyo, mtoto wako hayupo tena.
Nilikuwa na maswali mengi lakini sikuweza kuuliza, nilitaka kujua alikutwa katika hali gani, nini kimetokea, kwanini mtoto wa miaka 9 kuzungusha mandazi usiku peke yake? Ila nikimwangalia yule bibi, machoni mwake ni shida tu, niliamua kuwa kimya. Mwisho akanambia, "Mama yake alisema ulisema akifikisha miaka 7 utakuja kumchukua. Ana miaka 9 sasa, kalala pale, unaweza kumchukua mtoto wako naona umetimiza ahadi yako!"
Bibi alionekana alishakata tamaa, sikuweza kumjibu, lakini baada ya hapo hakusema kitu kingine chochote na mimi. Nilikaa pale watoto walikuja lakini kama alivyosema walikuwa wameharibikiwa na pombe, hata hawakujali nilipojitambulisha, walianza kuniomba pesa. Niliondoka na kurudi kwenye kaburi la mwanangu, nikiwa sina la maana nimerudi mjini kuendelea na maisha, lakini mpaka leo maisha yamesimama!
Sijui kwanini nilitelekeza mwanangu wakati nilikuwa na uwezo, ila sasa naona najuta, sina maana hata tena kuwa na mtoto, sijui hata kama nitakuja kuwa baba bora tena! Ndugu zangu ambao kila siku walikuwa wananambia mwanamke asikubabaishe mtoto akifikisha miaka 7 unamchukua, wanaishia kunisema na kuniona kama shetani, sijui nafanya nini na haya maisha!
Kweli yamenikuta, pumzika kwa amani mtoto wangu, wewe na mama yako, sijui ni mateso gani ulipitia kabla ya kifo kawakuta, lakini mimi baba yako naomba unisamehe!
(Nimeikopi huko wanakojielezea yakiwakuta)