Funzo kwa Tanzania: Shirika la ndege la South Africa limefilisika

Funzo kwa Tanzania: Shirika la ndege la South Africa limefilisika

Beberu wee !
Sasa mimi nina kosa gani? Pesa za kwetu na hatupangiwi matumizi na mtu yeyote. Unanitaje beberu? Kama hii miradi ingekuwa inapita bunge tumepata mawazo mbadala. Basi ndio hivyo tena.
 
Nawaza kwa sauti. Najaribu kudesa kwenye fikra za Mwalimu Nyerere. Wakati wa utawala wake serikali ilimiliki viwanda na mashirika mengi likiwemo ATC. Sio mashirika yote yalikua yanaleta faida lakini hakuyaacha yafe. Alikua ana akili nyingine kabisa. Alikua anayapa ruzuku ya kuyaendesha mwaka hadi mwaka. Hakuangalia mashirika haya kwa jicho la kuleta faida in terms of monetary directly kwa shirika mojamoja.

Sekta zilizokua zinaingiza faida ziliinua sekta/ mashirika yaliyokua yanapata hasara kama ATC kwasababu hayo mashirika yaliyokua yanapata faida yalikua yanabebwa indirectly na haya yanayopata hasara

Aliwahi kusema unapotaka kugawa keki ya taifa huwaiti watu ukawagaia pesa. Unawapa huduma bora kama afya, maji, elimu na kadhalika, tena bure na pia kutengeneza ajira ambazo watu watapata mshahara hata kutoka kwa mashirika yanayosuasua ambapo kimsingi yanapata ruzuku kutoka serikali kuu. Ndio maana enzi hizo ajira zilikua kedekede kuanzia serikalini hadi sekta binafsi

Walipokuja mabeberu na masharti yao ya ajabu wakatutaka tuuze au tubinafsishe mashirika yetu na viwanda vyetu. Kila kitu sasa kikawa kinatizamwa kwa jicho la faida na hasara ya kifedha tu! Mimi sio mchumi lakini naamini kuna sekta na mashirika mengine inabidi yawe retained na umma(serikali) hata kama ni kwa kupewa ruzuku. Leo tukisema Air Tanzania ife sio kwamba utapata ugali zaidi kwenye meza yako bali kuna watu walioajiriwa hapo ambao serikali ilikua inawalipa kutoka kwenye keki ambayo nao ni yao watakosa ajira na athari zake zinajulikana

Kwa maoni yangu, hata mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu hasa vyuo vya umma haikupasa kuwepo. Pesa hizo wangepewa au wasomeshwe bure ikiwa ni matumizi ya kawaida ya serikali kwa kutimiza wajibu wake kwa wananchi wake, nadhani ilikua ni mtazamo wa Marehemu Mwalimu Nyerere. I stand to be corrected
 
Tusitishane biashara huzaliwa na kufa. Kama wao wamekufa basi Airtz ndio imezaliwa sasa . Ukifuata maisha ya watu wengine utapata tabu saaaaaaana. Ishi maisha yako usiige. Airtz ikifa itafufuka Kq maisha yanasonga.
Nipo kwenye mall moja kwenye nchi fulani, kila siku wanakuja watu wapya kuchukua frem na kuanza biashara lakini wanafunga biashara zao baada ya miezi 3-6 baada ya kupata hasara. Laiti mtu angewaambia ukweli wasingeanzisha hizo biashara kichaa.
 
Hivi kuna shirika lolote la ndege Africa linalojiendesha kwa faida?
Ethiopia Airways mkuu lakini watu wana mashaka maana nchi haina uhuru kama sehemu nyinginezo. Serikali ina full control ya flow of information so hata kama kuna hasara, watu hawawezi kujua
 
Shirika kongwe la ndege la Afrika Kusini, limetangaza kufuta safari zake za nje ya nchi na baadhi ya safari za ndani, kutokana na kuishiwa fedha za uendesheji shirika linalozalisha hasara kwa miaka 9 mfululizo hadi sasa.

Shrika hili liliopata tuzo mbalimbali kwa ubora na huduma nzuri afrika na dunia kwa ujumla limeingia na kuwekwa katika uangalizi kwa mfilisi kutokana na kiasi kikubwa cha madni wanayodaiwa ambayo ni zaidi ya $3.9 billion toka 1994.

Habari hii ni mbaya na ishara mbaya kwa mashirika mengine ya ndege kutokana na gharama kubwa za uendeshaji na hasara ya mara kwa mara. Mashirika mengine yaliyo katika hali mbaya ya kiuchumi ni shirika la ndege la Kenya linaloendesha pia kwa hasara kwa zaidi ya miaka 5.

Hii inaleta tahadhari kubwa kwa mashirika ya ndege na biashara hii kwa ujumla.

Mashirika mengine ni Premera Air (Brazil), Saratov Air (Russia), Germania (German), Carfonia Parcific (USA), Jet Airways (India) na mengine mengi.

My take:
Serikali inayoendesha biashara ya usafirishaji wa anga (airlines) ni jasiri sana.
Kwa mawazo yako kila kitokeacho SA lazima kitokee na TZ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haija tokea au kuzugumzwa Kuna shirika la ndege hapa duniani limeingiza faida kiasi Fulani, Ila mashirika ya ndege yanayo pata tija(faida) yanabaki kimya tu au kinacho sifiwa NI huduma nzuri tu sio faida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja nipekuepekue taarifa za shirika kongwe kabisa la Ndege duniani KLM.
 
Yaani sisi tuanze kuifundisha serikali hii "sikivu" nini cha kufanya?? Serikali ina vyombo kibao na watu makini wa kupata taarifa isubiri thread za jf? Sisi kazi yetu ni kukosoa na kushauri kwa nia njema kabisa jukumu la kusikia na kufanyia kazi ushauri si letu tena!
Sijawahi kuona mnaongelea Ethiopia airway ....kila kukicha ni Kenya na South Africa.... Kama mna nia nzur kwa nini msilete nyuzi kuelezea na Ethiopia walivyofanikiwa ili serikali ijifunze pia hapo?....Inaonekana siku ukisikia Ndege ya ATCL imeanguka utachekelea sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani sisi tuanze kuifundisha serikali hii "sikivu" nini cha kufanya?? Serikali ina vyombo kibao na watu makini wa kupata taarifa isubiri thread za jf? Sisi kazi yetu ni kukosoa na kushauri kwa nia njema kabisa jukumu la kusikia na kufanyia kazi ushauri si letu tena!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mshauri sasa sio kukosoa tu.... Hamuwezi Kufundisha sababu ninyi sio professional kwenye biashara ya ndege na mambo ya avionics kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom