Funzo la mapinduzi toka nchini Mali: Maafisa waaandamizi wa Serikali ya Tanzania tendeni haki na kwa usawa kwani hamuijui kesho yenu

Ndo maana nakwambia huijui Dunia na hata hiyo Mali huijui. Eti risasi 38! Ndo nini sasa? HIzo risasi zilipigwa tanzania yote au kuna nini? Yaani unatagemea maanadamano ya Lissu ndo yaondoe serikali! Shiiit!

Kama unaweza kujadili JF kwa nini huwezi hata google ujue Mali ikoje na ilikuwaje? Elimu gani hiyo kichwani, mwanachama?
 
Mali ni Mali na Tanzania ni Tanzania, hatuko hivyo!. Sisi ni watu piece sana!.
P
Nimeishi Mali. Wamali ni watulivu, wapole, waaminifu, mbali kuwazidi Watanzania.

Nikifikiria yaliyotokea inakuwa vigumu kuamini kuwa ni wale ambao tulikuwa tukishinda na kwa namna fulani tukihisi, wamezubaa kuliko watu wa huko kwetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani mtu uko serious unalinganisha hali ya Mali na ya Tanzania. Watanzania tuko dhaifu sana, tunaamini tunaishi kwenye tabu kumbe kuna nchi zikipata maisha kama yetu zinagoma kabisa kubadili chochote zinakuwa zimefika.

Mali kwa mwaka huu tu wanajeshi zaidi ya 40 wamekufa kwa mashambulizi ya kigaidi, hawajalipwa stahiki zao, uchumi umefeli kabisa, tangu 2012 kuna waasi wa Tuager wanapambana na serikali, jeshi la UN likiongozwa na Ufaransa lipo linalinda usalama, makabila ya kule yanapinzana, baadhi ya watu wa dini fulani wanaojitoa mhanga, kuna ufisadi na rushwa ya kupindukia (sio hivi virushwa vyetu vya kuhonga wajumbe na kuwanunua Lijualikali)

Kati ya haya yote machache kipi kinatokea Tanzania?
 
Huijui Mali. Sijawahi kufika ukanda wa kaskazini lakini nimeishi Bamako na kusini mwa Mali mpakani na Ivory Coast.

Kwa huduma za jamii, na uhuru wa watu, kwa hali ya sasa, Mali ni bora kuliko Tanzania. Watu wapo free sana, siyo kama hapa kwetu. Flyovers pale Bamako wakati nikiwa kule zilikuwa 4. Sikuwahi kuona umeme ukikatika hata siku moja. Wala sikuwahi kuona maji yakiwa yamekatika licha ya kwamba maji na umeme hutegemea mabwawa tu ambayo hujazwa kwa mpango maalum kutoka mto Niger.

Uwanja wao wa ndege ulikuwa modern zaidi ya mara 5 ya wetu wa Dar wa zamani. Barabara za lami zinatembea sambamba na line ya umeme, kila kijiji inapopita kunakuwa na taa za barabarani toka mwanzo mpaka mwisho wa kijiji. Mitaa yao pale Bamako ni salama sana. Watu wakiwa wamekaa sehemu labda ya chakula, unapoondoka unaacha simu yako mezani kuishiria kuwa kiti hiki kina mtu tayari. Watu magari yao wakati wote hawafungi milango, na muda mwingine mtu unakuta ameacha mpaka ufunguo ndani ya gari, ofisi zinalala milango ikiwa imerudishiwa tu bila ya kufungwa, na laptop zikiwa ndani - husikii habari ya kuibiwa.

Siku moja niliingia Bamako saa 5 usiku nikitokea Uholanzi, sikuwa na local money. Wenyeji waliniambia niende sokoni kubadilisha kwa sababu muda ule maduka yote ya kubadilisha fedha yamefungwa, nikaenda sokoni, nilishangaa kuona mtu ana dola kwenye bag kama la kilo 10 hivi na bag jingine kama la kilo 20 la CFA. Ni usiku wa manane, yupo sokoni kama Kariaokoo, anawabadilishia watu pesa, hana mlinzi yeyote LAKINI yupo salama.

Bamako viwanja vyote vinepimwa, na miundombinu hutangulia kabla ya watu kugawiwa viwanja. Barabara ni pana hasa, na pembeni ya barabara kuna viwanja vya mpira vya ukubwa tofauti tofauti kwaajili ya burudani. Jioni ndiyo burudani karibia ya kila mtu.

Hiyo ndiyo Mali ninayoifahamu. Ujasiri huu wa sasa, sijui umetoka wapi. Ama kweli binadamu usimkadirie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ujanja wanaotumia ni kuwapa vyeo na mishahara minono hao viongozi wa jeshi ,sasa nani ataorganize wakati wanamlinda boss wao ili wale vizuri
Jeshi huwa halina rafiki!

Wale wanaojifanya Jeshi wanalijua sana au wameliweka mfukoni wawe makini sana, maana wanaume wakiamua kuingia kitaa, ni hatari
 
Mkuu, ninakuelewaga Sana, Ila unachosahau ni kwamba, hayo mambo Mazuri yalifanywa na viongozi waliopita kipindi hicho, sasa aliyepo ndiye ameshindwa kuyaendeleza hayo zaidi ya kuachia ufisadi utamalaki katika kipindi chake na ndiyo hiyo sababu ya kufurushwa.
 
Huijui Mali. Hayo unayoongea yapo kule Kaskazini kabisa ambako sehemu kubwa ni jangwa.

Kati na Kusini wapo vizuri. Na maeneo mengine wapo vizuri kuliko sisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa unaona ubovu wa systems za nchi. Mtu mwenye umri wa 25 yrs anakuwa mkuu msaidizi wa kambi kubwa zaidi. Yani dogo wa 25 yrs awe mkuu msaidizi wa yoyote ile hapa nchini.

Unless kama huu umri umekosewa.
Unamaanisha miaka 25 ni mtoto au? acha kuzingua mkuu
 
Kwahiyo ulitaka risasi 100!
 
Hivi unajua kuwa ni rahisi sana mfanyakazi anayelipwa sh milioni 10 kugoma kuliko anayelipwa sh laki 3?

Wala tusijipaishe sana. Bado nchi yetu ina mapungufu mengi ya kiutawala, sawa na baadhi ya nchi nyingi za Kiafrika. Na baadhi ya nchi kama vile Ghana, Botswana, South Afrika, Mauritius, Namibia, zipo vizuri zaidi kiutawala kuliko Tanzania.

Na tunavyoenda Tanzania sasa hivi, haitachukua muda tutadidimia zaidi maana wakati wenzetu wanapanda, sisi tunashuka. Wenzetu wanabadilisha sheria zao nyingi ili kuwapa zaidi uhuru raia, sisi tumekazana kutunga sheria za kuwadhibiti watu.

Nchi yetu ni kama ina dhamira ya kwenda kwenye primitivity badala ya civilization.

Rais Magufuli atakapomaliza muda wake, kutakuwa na kazi kubwa ya kubadilisha sheria ili tuweze kuendana na ustaarabu wa Dunia. Maana awamu hii, watawala wana hamu ya kuwaona wananchi wanafugwa kama ng'ombe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CreativityCode,

Nyie kila siku mnaleta hadisi zenu hamchoki? Ilikuwa sudani mara kwa mugabe na sehemu zingine hamchoki?

Tanzania sio huko mnakotaka tuwe, sisi sio wao
 
bro unaniondoa ushamba, shukrani kwa hilo. hizo nchi baadhi ulizotaja za kusini mwa Afrika ni kweli zipo vzuri sana
 
Aliyeongoza mapinduzi ni Brigadier general akiwa na makanali, unasemaje cheo cha chini?
 
Niulize unachotaka kujua. Uchumi wa Zimbabwe? Nguvu ya Mugabe Jeshini (Comrades), afya yake? Uwe specific maana nionavyo wote tuko JF kama bahari. Kuna uduvi hadi nyangumi.
Sawa Jack of All Trade. Mbumbumnu nakuuliza Taifa gani la nje lilikuwa nyuma ya kuondolewa Mugabe
 
Ikitokea ndo utajua nan anakula keki ya nchi hii

Sent from my itel P32 using JamiiForums mobile app
 
CreativityCode,
Mbona wrong citation, yaani ulichokiandika na reference uliyoweka haina relevance. Tanzania ni moja ya nchi inayaheshimika sana duniani, succession ya maraisi iko clear kabisa. Ushawahi kuona raisi wa tz kang'ang'ania madaraka? Tatizo you talk too much, mpaka wengine tunajiuliza malengo na nia zenu ni zipi? Misinformation must prevented in this country at any cost.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…