Huijui Mali. Sijawahi kufika ukanda wa kaskazini lakini nimeishi Bamako na kusini mwa Mali mpakani na Ivory Coast.
Kwa huduma za jamii, na uhuru wa watu, kwa hali ya sasa, Mali ni bora kuliko Tanzania. Watu wapo free sana, siyo kama hapa kwetu. Flyovers pale Bamako wakati nikiwa kule zilikuwa 4. Sikuwahi kuona umeme ukikatika hata siku moja. Wala sikuwahi kuona maji yakiwa yamekatika licha ya kwamba maji na umeme hutegemea mabwawa tu ambayo hujazwa kwa mpango maalum kutoka mto Niger.
Uwanja wao wa ndege ulikuwa modern zaidi ya mara 5 ya wetu wa Dar wa zamani. Barabara za lami zinatembea sambamba na line ya umeme, kila kijiji inapopita kunakuwa na taa za barabarani toka mwanzo mpaka mwisho wa kijiji. Mitaa yao pale Bamako ni salama sana. Watu wakiwa wamekaa sehemu labda ya chakula, unapoondoka unaacha simu yako mezani kuishiria kuwa kiti hiki kina mtu tayari. Watu magari yao wakati wote hawafungi milango, na muda mwingine mtu unakuta ameacha mpaka ufunguo ndani ya gari, ofisi zinalala milango ikiwa imerudishiwa tu bila ya kufungwa, na laptop zikiwa ndani - husikii habari ya kuibiwa.
Siku moja niliingia Bamako saa 5 usiku nikitokea Uholanzi, sikuwa na local money. Wenyeji waliniambia niende sokoni kubadilisha kwa sababu muda ule maduka yote ya kubadilisha fedha yamefungwa, nikaenda sokoni, nilishangaa kuona mtu ana dola kwenye bag kama la kilo 10 hivi na bag jingine kama la kilo 20 la CFA. Ni usiku wa manane, yupo sokoni kama Kariaokoo, anawabadilishia watu pesa, hana mlinzi yeyote LAKINI yupo salama.
Bamako viwanja vyote vinepimwa, na miundombinu hutangulia kabla ya watu kugawiwa viwanja. Barabara ni pana hasa, na pembeni ya barabara kuna viwanja vya mpira vya ukubwa tofauti tofauti kwaajili ya burudani. Jioni ndiyo burudani karibia ya kila mtu.
Hiyo ndiyo Mali ninayoifahamu. Ujasiri huu wa sasa, sijui umetoka wapi. Ama kweli binadamu usimkadirie.
Sent using
Jamii Forums mobile app