Funzo la mapinduzi toka nchini Mali: Maafisa waaandamizi wa Serikali ya Tanzania tendeni haki na kwa usawa kwani hamuijui kesho yenu

Funzo la mapinduzi toka nchini Mali: Maafisa waaandamizi wa Serikali ya Tanzania tendeni haki na kwa usawa kwani hamuijui kesho yenu

Ni kwa sababu wamekariri pia ni wanufaika,ongea na wa chini yao usikie mawazo yao wanawalaumu wananchi ndo wajinga wanawachelewa pa kuanzia.
Huwa wananchi ndo uanza wao uja kumaliza mchezo
ofcourse wananchi ndio wakulianzisha ila kabla hawajalianzisha kina Sirro wanaleta Vijana wake na Mabomu kitaani kuwapiga raia na raia wakishaona mabomu wanasanda hivyo maandamano yanazimwa fasta.
 
Hivi kwa utawala huu wa awamu ya 5 kama utaendelea hivi unafikiri hatutaingia road?
Yaani kuna wajinga wanaamini hizi Sheria kandamizi zinazotungwa kumsifia Rais tutazivumilia tu? Haiwezekani nchi yote itungiwe Sheria za kumuona binadamu mmoja ni bora sana kuliko wengine mtarajie muwe salama milele, kwa taarifa yenu hata huko mnokoona yanatokea kuna watu hawakuwahi kuota hiyo ndoto mpaka waliposhuhudia kwenye runinga malaika wao kala pingu ndio wakaamini.

Kinachotokea Mali ni raisi kushindwa kukabiliana na Ugaidi ambao unasaidiwa na ISIS na Al-Qaida.

Na jambo la pili ni kushindwa kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19.

Hayo yote hayafanani kabisa na Tanzania yetu ambayo ni kisiwa cha Amani na Utulivu.
 
Huijui Mali. Hayo unayoongea yapo kule Kaskazini kabisa ambako sehemu kubwa ni jangwa.

Kati na Kusini wapo vizuri. Na maeneo mengine wapo vizuri kuliko sisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe unatwambia Mali ya kihistoria as if aliyepinduliwa ni kiongozi wa kihistoria.
Uongozi ulioondolewa ni mbovu na ulikuwa incompetent. Hiyo historia ya wana maendeleo mazuri kwa hiyo ndio wabweteke wakose usalama, washindwe kiuchumi, rushwa na ufisadi vitamalaki.

Uingereza mara baada tu ya WW 2, Winston Churchill alishindwa uchaguzi. Wangekuwa wanatumia historia na experience iliyopita kuamua yajayo unadhani angeshindwa.

Na hilo la kusema Kaskazini ndo kuna shida tu, ndio maana waasi wa Tuareg wanasumbua. Simply utaambiwa kama mnaona hili eneo halifai kuendelezwa tuache tujitenge, hapo ndipo nchi za Afrika hukosea. Najua wajua kwa nini Biafra ilitokea, kwanini Somaliland imejitenga, kwanini South Sudan imejitenga, hapa Msumbiji kuna ugaidi, Mashariki ya DRC, etc.
 
Kinachotokea Mali ni raisi kushindwa kukabiliana na Ugaidi ambao unasaidiwa na ISIS na Al-Qaida.

Na jambo la pili ni kushindwa kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19.

Hayo yote hayafanani kabisa na Tanzania yetu ambayo ni kisiwa cha Amani na Utulivu.
Kwani kuna sehemu nimesema matatizo ya Mali yanafanana na yetu? Hoja yangu ni wananchi kuchoshwa na baadhi ya mambo halafu Serikali ipo tu inaangalia na kulazimisha mambo hayo yaonekane ya kawaida.
Sisi Tanzania tuna yetu mabaya sio lazima yawe ugaidi, na kuhusu uchumi kila nchi ina kipimo chake, sasa wengine mkisema tuko vizuri sisi wengine tunasema hatuko vizuri na tuna hoja zetu.
Mkisema nyinyi mna amani sisi wengine tunasema hatuna amani na ushahidi na mifano halisi tunayo, Sasa twendeni hivyohivyo.
 
Mkuu, huyu ameshindwa kuandika ukweli, kilichomfurumusha huyo Raisi wa Mali ni kushindwa kudhibiti ufisadi ndani ya nchi yake, Jeshi likaona haina Maana kuwa wajeda waendelee kuona wizi ukitamalaki Wakati raia wengi wa nchi hiyo wanaishi maisha ya mateso na dhiki Ili Hali Utajiri wa nchi Yao ukigawanwa na wachache

Sasa anapokuja kulinganisha na hapa, Kwa kigezo kipi mpaka aseme Eti ni Bora hata hapa kufanyike kama Mali,

Nchi inavyojengwa kiasi hicho, kila mtu anaishi Kwa nguvu zake yeye mwenyewe, na Pesa inayopatikana inaonekana inafanya vitu, mafisadi wamebanwa mbavu hawapumui, Raisi aliyepo Sio pandikizi ni Mtanzania aliyewekwa na Watanzania,

Kwanza hao mapandikizi ndio inabidi wakataliwe kote Africa Ili Africa isonge mbele
wewe unajua Afrika tu ndio upeo wako hiyo Belarus hawaandamani? fuatilia mada Wananchi ndio wenye kila kitu hata huo ufisadi
 
Kwani kuna sehemu nimesema matatizo ya Mali yanafanana na yetu? Hoja yangu ni wananchi kuchoshwa na baadhi ya mambo halafu Serikali ipo tu inaangalia na kulazimisha mambo hayo yaonekane ya kawaida.
Sisi Tanzania tuna yetu mabaya sio lazima yawe ugaidi, na kuhusu uchumi kila nchi ina kipimo chake, sasa wengine mkisema tuko vizuri sisi wengine tunasema hatuko vizuri na tuna hoja zetu.
Mkisema nyinyi mna amani sisi wengine tunasema hatuna amani na ushahidi na mifano halisi tunayo, Sasa twendeni hivyohivyo.

Mali ni "special case" na tusingetumia nchi iliyo katika hali ya vurugu na ghasia kulinganisha na Tanzania.
 
wewe unajua Afrika tu ndio upeo wako hiyo Belarus hawaandamani? fuatilia mada Wananchi ndio wenye kila kitu hata hip ufisadi
Mkuu, ulichoandika kinaendana na hoja iliyopo?

Jikite kwenye hoja, na ukumbuke pia huko tuendako Dunia itakuwa ni tabu Sana kujitawala, sababu za Kwa nini huwenda Dunia istawalike Kwa miaka michache ijayo, huko tuendako zipo tu
 
Kenge huwa hasikii mpaka damu imtoke sikioni, ccm jiandaeni, kuishi kwa mazoea kutawagharimu very soon.
Kilichotokea nchini Mali na nchi mbalimbali duniani kuhusu viongozi madikteta kuondolewa madarakani kinatoa somo kwa maafisa waandamizi wa serikali ya Tanzania kwamba kwa kuwa hawaijui kesho yao basi ni vema kutenda haki na usawa kwa watu wote bila kujali vyama vyao vya siasa kwa kufuata katiba na sheria za nchi.

Ni bora kujiuzulu ikiwa agizo la Rais linapingana na katiba na sheria za nchi kuliko kushiriki katika uovu ambao utakuja kuwagharimu siku za usoni siku ambapo mnayemtetea mbele za watu hatokuwa na nguvu ya kuendelea kuwalinda.

Heshimuni vyama vyote vya siasa kwa mujibu wa katiba na sheria kwani leo ni CCM kesho ni CHADEMA. Dunia inakwenda kwa kasi sana na mabadiliko ya upepo wa kisiasa ni suala la siku moja tu.

KWA LEO NI HAYO TU, NAWATAKIA SIKU NJEMA
 
ofcourse wananchi ndio wakulianzisha ila kabla hawajalianzisha kina Sirro wanaleta Vijana wake na Mabomu kitaani kuwapiga raia na raia wakishaona mabomu wanasanda hivyo maandamano yanazimwa fasta.
HAO VIJANA CHOKA MBAYA NA WALA SI WANUFAIKA KAMA MABOSI ZAO HIO NGUVU YA KUTUPA HAYO MABOMU KWA UZALENDO NA KUNUFAIKA KUPI HUKO.
 
Maandamano ya kutengenezwa ni kiinimacho tu kuonyesha wananchi wanataka masuala fulani lakini kuna hila nyuma yake.

Kwamza uchaguzi wa 2013 alishinda kwa 77% hiyo ni ushahidi tosha kwamba wanachi wa Mali wana imani nae.

Ni maandamano ambayo yanaratibiwa na wanaojiita wapinzani ambao wanataka kuendelea kunufaika na "Chaos" iliyopo ya ugonjwa wa COVID-19, na Ugaidi unaoendelea( kumbuka magadi walivamia hoteli ya kitalii majuzi).

ECOWAS ina wanachama 15 ikiwemo Mali hivyo haiwezi kuvumilia kuona raisi aliechaguliwa kihalali kupitia sanduku la kura anapinduliwa na kikundi cha wanajeshi wachache wenye uchu wa madaraka.

Ndio maana ECOWAS imefunga mipaka na kuzuia mizunguko ya fedha inayoihusisha Mali.
kwann ecowas huwa kimya panapo udikteta panapo wanachama wake
 
Hivi kwa utawala huu wa awamu ya 5 kama utaendelea hivi unafikiri hatutaingia road?
Yaani kuna wajinga wanaamini hizi Sheria kandamizi zinazotungwa kumsifia Rais tutazivumilia tu? Haiwezekani nchi yote itungiwe Sheria za kumuona binadamu mmoja ni bora sana kuliko wengine mtarajie muwe salama milele, kwa taarifa yenu hata huko mnokoona yanatokea kuna watu hawakuwahi kuota hiyo ndoto mpaka waliposhuhudia kwenye runinga malaika wao kala pingu ndio wakaamini.
sheria sio kinga ni sawa na kondomu tu inatumika kulingana na mahaitaji ya wakati huo
 
kwann ecowas huwa kimya panapo udikteta panapo wanachama wake

Mali ni nchi ambayo sasa hivi iko kwenye vurugu.

Hivyo hatua zinazochukuliwa na jumuiya kama ya ECOWAS yenye wajumbe nchi 15 ikiwemo Mali yenyewe ni za kuziheshimu.

Eneo la Sahara Magharibi limevamiwa na magaidi na wameweka kambi zao kaskazini mwa Mali.

Ni tishio kwa usalama wa nchi zote zinazoizunguka na pia ni tishio kwa usalama, maisha ya wananchi wa eneo hilo ambao wengi ndo wakimbizi wa kupitia Libya kupitia bahar ya Mediterranean kwenda Ulaya.

Ndo maana Ufaransa, Uingereza, Ujerumani na vikosi 15,600 vya UN wapo nchini Mali.

Tuwe twaangalia haya mambo katika picha kubwa.
 
Naomba itokee na kwetu hapa ili wale wasiotaka kufuata sheria na katiba ,wanaokiuka haki za binadamu kwa kujiona wao ni wao yawakute tuwaone nyuso zao watazificha wapi.
 
Mali ni nchi ambayo sasa hivi iko kwenye vurugu.

Hivyo hatua zinazochukuliwa na jumuiya kama ya ECOWAS yenye wajumbe nchi 15 ikiwemo Mali yenyewe ni za kuziheshimu.

Eneo la Sahara Magharibi limevamiwa na magaidi na wameweka kambi zao kaskazini mwa Mali.

Ni tishio kwa usalama wa nchi zote zinazoizunguka na pia ni tishio kwa usalama, maisha ya wananchi wa eneo hilo ambao wengi ndo wakimbizi wa kupitia Libya kupitia bahar ya Mediterranean kwenda Ulaya.

Ndo maana Ufaransa, Uingereza, Ujerumani na vikosi 15,600 vya UN wapo nchini Mali.

Tuwe twaangalia haya mambo katika picha kubwa.
mfumo mbovu wa tawala za kiafrika kutoheshimu katiba zao ndi umepelekea uzalishaji wa magaidi na wakimbizi afrika
 
mfumo mbovu wa tawala za kiafrika kutoheshimu katiba zao ndi umepelekea uzalishaji wa magaidi na wakimbizi afrika

Vipi kuhusu mifumo na tawala za nchi za kibeberu.

Mbona wanao magaidi wao hitaita "home-grown terrorists"?
 
Mali ni Mali na Tanzania ni Tanzania, hatuko hivyo!. Sisi ni watu peace sana!.
P
Sema hujui historia ya Mali, kwani wao walianzaje huko nyuma. Rudi ukasome ndio urudi utoe maoni.

Kama hakuna haki hakuna nchi inayoweza kuwa salama siku zote. Hakuna.
 
Sema hujui historia ya Mali, kwani wao walianzaje huko nyuma. Rudi ukasome ndio urudi utoe maoni.

Kama hakuna haki hakuna nchi inayoweza kuwa salama siku zote. Hakuna.
Mkuu Nyanjomigire, kwa bahati nzuri sana, mimi ni mpenzi wa somo la Historia, hivyo Mali ninayoujua mimi sio tuu Mali hii, bali mali ya tangu enzi za Manka Musa.

Hivyo naendelea kusisitiza, Mali ni Mali na Tanzania ni Tanzania.
P
 
Back
Top Bottom