chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
HANDSHAKE kati ya Raila Amolo Odinga na Uhuru Kenyata ililenga kufanya mabadiliko makubwa ya kikatiba ili kuweka vyeo, pamoja na mambo mengine mengi. William Rutto aliwaambia wakenya kwamba shida yao sio katiba nyingine, shida yake ni kukomboa mama mboga na mtu wa bodaboda, kwamba shida ya wakenya ni uchumi, pesa ikae mfukoni na kuondoa umasikini.
Kwa namna yoyote ile hii ndio ajenda kuu kwa sasa kwa bara la Afrika. Wananchi hawali hayo vifungu ya katiba, haviwaletei barabara, maji, vituo vya afya, mbolea, reli au umeme. Nadhani ni swala la CCM kukazia hapo na kufafanua kwa kina, watanzania ni waelewa sana.
Chadema wamesimama na ajenda ya kushindwa, ajenda kama ya Raila Amolo Odinga ya kugawana vyeo na kuongeza matumizi ya serikali. Lema anataka awe Gavana wa Arusha, alishwe na kuvishwa na serikali na kutembelea V8. Kimsingi ni kujiposition kwa ajili ya ulafi.
Watanzania tutulie katiba hii inatosha, kama ina shida mahali ni kufanya rekebisho dogo tu!