ikipendaroho
JF-Expert Member
- Jul 26, 2015
- 3,903
- 3,856
Kulikuwa na sababu ya kutaja nafasi aliyoambulia Paschal Mayalla, huo utukutu tu.Furaha Dominic ambaye ni mpwa wa hayati Magufuli aliyegombea ubunge jimbo la Kawe na kushika nafasi ya kwanza huku Pascal Mayalla akiwa wa 162 amesema siku atakayokutana na Rais Samia atampa orodha ya Wafitini wote waliomzunguka.
Furaha anadai CCM kumejaa siasa chafu za kupakana matope, kufitinishana, kuchongeana na kusingiziana huku KUPE wa chama wakimnyonya damu Rais.
Furaha amesema ameshuhudia mengi sana katika utawala wa mjomba wake ( Magufuli) ikiwemo yeye mwenyewe kudhibitiwa na kikundi cha Wasiojulikana ili asigombee ubunge
Furaha alikuwa akihojiwa na Aloyce Nyanda katika kipindi cha The Big Agenda, Star tv.
Mjadala ulikuwa mkali na Furaha alionekana akifuta machozi mara kwa mara huku mtangazaji Mtozi akimfariji.
Mahijiano yataendelea tena Ijumaa kwani jana hayakukamilika.
Mungu wa mbinguni awabariki sana!
Kama Furaha analizwa na CCM wewe ni nani hadi Uchekelee?
Bwashee katika uchaguzi wa Kawe watu maarufu walikuwa Wawili tu Pascal Mayalla na Askofu Gwajima!Kulikuwa na sababu ya kutaja nafasi aliyoambulia Paschal Mayalla, huo utukutu tu.
Nimekusoma Bwashee ila wajumbe hawakumtendea haki Kaka yetu 162, mbali mno mkuu.Bwashee katika uchaguzi wa Kawe watu maarufu walikuwa Wawili tu Pascal Mayalla na Askofu Gwajima!
Wote hao wako CCM?.
Kupe, Chawa, Ndorobo, Papasi, Sisimizi, Kiroboto, Mchwa
Hahahaaaa........ Chadema kuna makarai by Katambi!Wote hao wako CCM?.
Ndiyo Sehemu Yao Ya Kujidai Ndani Ya CcmWote hao wako CCM?.
Tumbo lenye njaa huponza ubongo, huyu dogo katambi ndiye alikoswakoswa mabomu ya machozi kipindi anaandaa maombi kwa ajili ya Tundu Lisu. Pia Chadema ndiyo imemtengeneza hadi ccm wakamtamani wakamnunua kupitia kwa dalali kiroboto. Leo hii kuitusi Chadema naamini hata kwa Mungu ana makosa.Hahahaaaa........ Chadema kuna makarai by Katambi!
Kama ni hivyo ccm inatakiwa ifanyiwe fumigation halafu tuwafagie hawa wadudu waharibifu wote. Au uozo ndio mtaji wao?!!Ndiyo Sehemu Yao Ya Kujidai Ndani Ya Ccm
Ndiyo Ukweli WenyeweKama ni hivyo ccm inatakiwa ifanyiwe fumigation halafu tuwafagie hawa wadudu waharibifu wote. Au uozo ndio mtaji wao?!!
Hiyo siyo shida! Ila kwa nini johnthebaptist anaendelea kusema? Hiyo tu ndiyo imeniuma rohokwaiyo Paschal mayala alikua wa 162?
Kikulacho ki nguoni mwako!Huyu mjomba alikuwa personal secretary wa JPM