Furaha Dominic: Rais Samia awe mwangalifu na hao waliomzunguka, wengi wao ni Wafitinishi (KUPE) walimdanganya Magufuli!

Furaha Dominic: Rais Samia awe mwangalifu na hao waliomzunguka, wengi wao ni Wafitinishi (KUPE) walimdanganya Magufuli!

Siku ile ya kuomba kura jinsi alivoikamata mic na kuongea sentensi moja tu niliuona ni mtoto wa mjini lakini leo nimemsikia anaongea ndio kani prove wrong.

Having said that, kwa ushawishi alionao huyu jamaa katika jimbo basi he deserves attention ya mama hasa kwa vilemjomba wake hakumuona kuwa ni favourite nephe!
 
Furaha Dominic ambaye ni mpwa wa hayati Magufuli aliyegombea ubunge jimbo la Kawe na kushika nafasi ya kwanza huku Pascal Mayalla akiwa wa 162 amesema siku atakayokutana na Rais Samia atampa orodha ya Wafitini wote waliomzunguka.

Furaha anadai CCM kumejaa siasa chafu za kupakana matope, kufitinishana, kuchongeana na kusingiziana huku KUPE wa chama wakimnyonya damu Rais.

Furaha amesema ameshuhudia mengi sana katika utawala wa mjomba wake ( Magufuli) ikiwemo yeye mwenyewe kudhibitiwa na kikundi cha Wasiojulikana ili asigombee ubunge

Furaha alikuwa akihojiwa na Aloyce Nyanda katika kipindi cha The Big Agenda, Star tv.

Mjadala ulikuwa mkali na Furaha alionekana akifuta machozi mara kwa mara huku mtangazaji Mtozi akimfariji.
Mahijiano yataendelea tena Ijumaa kwani jana hayakukamilika.

Mungu wa mbinguni awabariki sana!

Kama Furaha analizwa na CCM wewe ni nani hadi Uchekelee?
Kulikuwa na sababu ya kutaja nafasi aliyoambulia Paschal Mayalla, huo utukutu tu.
 
Nimemsikiliza huyu kijana. inakuwaje anajua mambo mengi ya karibu as if alikuwa ni msaidizi wa Rais .... Ina maana Rais JPM alikuwa anaendesha mambo ya nchi kama familia.
 
Hahahaaaa........ Chadema kuna makarai by Katambi!
Tumbo lenye njaa huponza ubongo, huyu dogo katambi ndiye alikoswakoswa mabomu ya machozi kipindi anaandaa maombi kwa ajili ya Tundu Lisu. Pia Chadema ndiyo imemtengeneza hadi ccm wakamtamani wakamnunua kupitia kwa dalali kiroboto. Leo hii kuitusi Chadema naamini hata kwa Mungu ana makosa.
 
RAIS SAMIA ATUMIE MANENO YA FURAHA KUJENGA UPYA TAIFA.

Na Elius Ndabila
0768239284

Mjadala mkubwa leo kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vingi vya habari ni juu ya uteuzi wa Mhe Dkt Tulia kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la JMT kupitia Chama Cha Mapinduzi. Niwatoe kwenye mjadala huu na kuwapeleka kwa FURAHA MTOTO WA DADA YAKE NA HAYATI JPM.

Kati ya tarehe 10 au 11 Ndg Furaha aliyejitambulisha kama Mjomba wa hayati Dkt Magufuli alikuwa akifanyiwa mahojiano na kituo cha Star Tv. Leo nimefanikiwa kuingia youtube na kuitazama video hiyo yenye urefu wa zaidi ya dakika 55.

Baada ya kuitazama na kuisikiliza video hii nimepigwa na butwaa. Kama Mhe Samia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia vyanzo vyake ameiona basi Mungu amuongoze sana ktk kurejesha upendo, Kwani kuna watu waliumizwa kwa kuonewa. Sidhani kama Furaha anaweza kulidanganya Taifa.

Furaha amenipa msamiati mwingine mpya. Amesema katika awamu iliyopita kulikuwa na KUPE. Amesema wapo watu waliokuwa wanamjua vizuri Mhe Magufuli kuwa ni mtu ambaye ukimpa taarifa hata kama umemdanganya lakini kama hajui kuwa unadanganya basi yeye alikuwa anaamini sana taarifa za mwanzo. Amesema wapo wengi aliwaumiza Kwa sababu ya kupe waliokuwa wakindanganya na walikuwa wanazisuka kama ni kweli kwa vielelezo vya kupika.

Amesema yeye alikuwa anaskitika kuna watu wapo hadi leo serikalini ambao mwanzo ndio walikuwa wanampelekea faili mbaya JPM juu ya Mhe Samia. Amesema moja wapo ya kupe mkubwa Rais Samia alimuondoa mapema kabisa alipoanza awamu ya sita. Ameendelea kusistiza kuwa wengi wa wale wanaondolewa na Rais anawajua na Rais anapiga mle mle. Amesema wengine ambao ndo walikuwa wapika taarifa za uongo leo tena ndio wanaongoza kucriticize baadhi ya mambo, akatolea mfano wa Mhe....

Furaha anasema kuwa wengine walipoona kuwa yeye Furaha anaweza kumwambia JPM kuwa hawa wanakudanganya walikuja wakafanikiwa kumchongea kwa JPM na wakatengeneza protocol ambazo ilikuwa ngumu kupenya kuongea nao.

Furaha anaongeza kwa kusema siku akikutana na Rais atampa orodha ya kupe wote waliokuwa wakienda Ikulu kilindi hicho na kumpotosha hayati. Anasema kupe hao waliwaumiza wengi na wengine JPM alipogundua anedanganywa alianza kuwarudisha kazini.

Hizi ni nukuu chache kati ya nyingi. Tafsiri yake ni nini? Tafsiri yake ni kuwa Kupe walifanikiwa kuliumiza hili taifa na kutengeneza migogoro kati ya jamii na serikali au chama.

Je, ni watu wangapi wapo jera pengine Kwa sababu ya hawa kupe waliompotosha Rais? Ni watu wangapi wana kesi kila namna Kwa sababu ya hawa kupe? Ni watu wangapi wamekosa teuzi, Ubunge na kufukuzwa kazi kwa sababu ya hawa ambao Furaha anawaita kupe? Tufakari.

Je, kuna uhusiano wa KUPE VS VIROBOTO au Kupe vs Wahuni?

Ninamuomba Mhe Rais kupitia vyanzo vyake Makini kuanza kuangalia namna ya kurudisha upendo ambao kupe waliuharibu. Na ikiwezekana hata kesi ambazo zipo Mahakamani au tuhuma ambazo bado upelelezi haujakamilika na zile ambazo upelelezi umekamilika lakini ushahidi ni wa kubumba DPP anaweza kuzifuta. Inawezekana zilitengenezwa na hawa kupe ili kuwadhibiti.
 
... huwa najiuliza Bashiru aliwezaje kupanda vyeo haraka haraka hadi kuwa mkuu wa utumishi wa umma? Well, ni msomi mzuri lakini wapo wasomi wazuri kuliko yeye na/au wenye experience na maadili mazuri zaidi! Bahati mbaya kwake ndiye Katibu Mkuu Kiongozi aliyehudumu kwa muda mfupi zaidi. Kipindi kile uchawa ulikuwa dili haswa!
 
Nini kinachoweza kutuaminisha kwamba huyu the so-called Furaha si muongo? Hivi si kwamba anajaribu tu kuleta uchonganishi na kujipendekeza?

Hao ^wengine^ anaodai JPM aliwarudisha baada ya kugundua alidanganywa, ni wapi?

Why hakusema wakati JPM akiwa hai, ilhali akijua, according to him, kwamba watu wanaumizwa bila kosa? JPM angekuwa hai hadi leo angeendelea kuwa kimya (hadi lini)?

MY TAKE: HUYU FURAHA NDIYE KUPE MKUBWA, MTU MCHONGANISHI, MWONGO & MJIPENDKEZAJI!
 
Back
Top Bottom