Furaha Dominic: Rais Samia awe mwangalifu na hao waliomzunguka, wengi wao ni Wafitinishi (KUPE) walimdanganya Magufuli!

Sikiliza nikwambie ndugu yangu soma alama za nyakati…hizi sinema zimeshapitwa na wakati..achaneni na hizo vitu ni waste of time…
Nilikua na mtazamo kama wako; kwamba huyu dogo eti alizuiliwa asiweze kumuona mjomba wake? Huyu angeweza kushinda KURA za maoni za ubunge pale KAWE bila ya nguvu ya mjomba?

Hakuna na umaarufu wowote wa yeye kupata walau kura 20, kama anabisha ajaribu mwaka 2025 kugombea tena baada ya mjomba wake kuitwa mbele za HAKI
 
Hizo ni harakati zake za kujipendekeza, na uchungu wa kushindwa ubunge 2020. Alidhani JPM kwa kuwa na unasaba naye, basi angempitisha kirahisirahisi tu awe mbunge. JPM wa too smart. Huyo aache ukupe!
 
Ingawa ni kwa shingo upande nayakubali haya mawazo ya huyo mpwa wa marehemu.

Viongozi wakuu wa nchi hii wamezungukwa na makupe na watu wenye roho mbaya.
 
Mkuu Mazindu Msambule, ni kweli alizuiliwa kumuona uncle wake, kwanza alifutwa ofisini kwa tanganyika jeki!, akahifadhiwa sehemu salama, alipoachiwa akataka kuripoti kwa uncle akanyimwa security clearance. Unapotaka kumuona rais, wewe kama ni ndugu, jamaa na marafiki ni rais mwenyewe ndio ana give ile first access, baada ya hapo unaingia na kutoka anytime as a family member, ukizuiliwa maana yake ni rais ndie amezuia ile access yako.

Kwenye kugombea Kawe ni kweli uncle wake alimgomea, hivyo kukotokea wafadhili usually wahindi na Waarabu waka msponsor dogo, hivyo ndio mgombea aliyeongoza kwa kuwa na mkono mrefu ulioshika kisu kikali, hivyo alikuwa anakata balaa!. Mtu wa pili mwenye kisu kikali ni Angela Kizigha!.

Baada ya CCM kumchinja na kumteua Gwajiboy, wana Kawe waliamua kuiadhibu CCM kwa kumtosa mtu wao hivyo wakafanya kumpiga chini Gwajiboy hivyo ni huyu dogo aliwazungukia tena na kuwaangukia wamchague Gwaji vinginevyo CCM ingekula mweleka. Hivyo umaarufu wake Kawe sio kwa sababu ya influence ya Mjomba bali amejua kuutumia vizuri nyota ya nasaba na sasa anafungua bonge la TV, FTV.
P
 
kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…