Adrian Stepp
JF-Expert Member
- Jul 1, 2011
- 2,764
- 2,591
Nilitazama yale mahojiano..alitisha sana kijana!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nilikua na mtazamo kama wako; kwamba huyu dogo eti alizuiliwa asiweze kumuona mjomba wake? Huyu angeweza kushinda KURA za maoni za ubunge pale KAWE bila ya nguvu ya mjomba?Sikiliza nikwambie ndugu yangu soma alama za nyakati…hizi sinema zimeshapitwa na wakati..achaneni na hizo vitu ni waste of time…
Kupe wa kwanza amejitokeza tayari.Sikiliza nikwambie ndugu yangu soma alama za nyakati…hizi sinema zimeshapitwa na wakati..achaneni na hizo vitu ni waste of time…
Hizo ni harakati zake za kujipendekeza, na uchungu wa kushindwa ubunge 2020. Alidhani JPM kwa kuwa na unasaba naye, basi angempitisha kirahisirahisi tu awe mbunge. JPM wa too smart. Huyo aache ukupe!Nilikua na mtazamo kama wako; kwamba huyu dogo eti alizuiliwa asiweze kumuona mjomba wake? Huyu angeweza kushinda KURA za maoni za ubunge pale KAWE bila ya nguvu ya mjomba???? Hakuna na umaarufu wowote wa yeye kupata walau kura 20, kama anabisha ajaribu mwaka 2025 kugombea tena baada ya mjomba wake kuitwa mbele za HAKI
Nasema, huyu ni KUPE MHUNI. Anaonekana kuwa na ^v-na-7^ vyote!Huyu anaugomvi na hao kupe!!huyu naye ni team wahuni
Pasco Mayala a.k.a njaa aachane na jina hilo,atafute ubini mwingine vinginevyo ni kama linamletea mikosi 😂Kwa hiyo Paskali alishika nafasi ya 162 kati ya wagombea 162. .!?
Ingawa ni kwa shingo upande nayakubali haya mawazo ya huyo mpwa wa marehemu.Furaha Dominic ambaye ni mpwa wa hayati Magufuli aliyegombea ubunge jimbo la Kawe na kushika nafasi ya kwanza huku Pascal Mayalla akiwa wa 162 amesema siku atakayokutana na Rais Samia atampa orodha ya Wafitini wote waliomzunguka.
Furaha anadai CCM kumejaa siasa chafu za kupakana matope, kufitinishana, kuchongeana na kusingiziana huku KUPE wa chama wakimnyonya damu Rais.
Furaha amesema ameshuhudia mengi sana katika utawala wa mjomba wake ( Magufuli) ikiwemo yeye mwenyewe kudhibitiwa na kikundi cha Wasiojulikana ili asigombee ubunge
Furaha alikuwa akihojiwa na Aloyce Nyanda katika kipindi cha The Big Agenda, Star tv.
Mjadala ulikuwa mkali na Furaha alionekana akifuta machozi mara kwa mara huku mtangazaji Mtozi akimfariji.
Mahijiano yataendelea tena Ijumaa kwani jana hayakukamilika.
Mungu wa mbinguni awabariki sana!
Kama Furaha analizwa na CCM wewe ni nani hadi Uchekelee?
Binadamu mwenye akili timamu unawezaje kuchoka kutafuta maisha?Ukichoka kutafuta maisha achana nayo kaa kwa kutulia subiri yakutafute yenyewe
Kwa hali hii tuliyo nayo sisi wakhojani hatumuangalii mtu usoni.Ndiyo ajitahidi kuongea asije kusahaulika milele
Kuwa na ajira siyo issue bali watu wanatafuta mpenyo wa kupiga mpunga mrefu kwa kipindi kifupiYeye ni Mkemia pale kwa Mkemia mkuu!
Mkuu Mazindu Msambule, ni kweli alizuiliwa kumuona uncle wake, kwanza alifutwa ofisini kwa tanganyika jeki!, akahifadhiwa sehemu salama, alipoachiwa akataka kuripoti kwa uncle akanyimwa security clearance. Unapotaka kumuona rais, wewe kama ni ndugu, jamaa na marafiki ni rais mwenyewe ndio ana give ile first access, baada ya hapo unaingia na kutoka anytime as a family member, ukizuiliwa maana yake ni rais ndie amezuia ile access yako.kwamba huyu dogo eti alizuiliwa asiweze kumuona mjomba wake? Huyu angeweza kushinda KURA za maoni za ubunge pale KAWE bila ya nguvu ya mjomba???? Hakuna na umaarufu wowote wa yeye kupata walau kura 20, kama anabisha ajaribu mwaka 2025 kugombea tena baada ya mjomba wake kuitwa mbele za HAKI
Kiukweli kuna watu humu wananionea sana!.Hehehe mkuu kulikuwa na ulazima gani wa kusema Pascal Mayalla alikuwa wa 162...
kweliRAIS SAMIA ATUMIE MANENO YA FURAHA KUJENGA UPYA TAIFA.
Na Elius Ndabila
0768239284
Mjadala mkubwa leo kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vingi vya habari ni juu ya uteuzi wa Mhe Dkt Tulia kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la JMT kupitia Chama Cha Mapinduzi. Niwatoe kwenye mjadala huu na kuwapeleka kwa FURAHA MTOTO WA DADA YAKE NA HAYATI JPM.
Kati ya tarehe 10 au 11 Ndg Furaha aliyejitambulisha kama Mjomba wa hayati Dkt Magufuli alikuwa akifanyiwa mahojiano na kituo cha Star Tv. Leo nimefanikiwa kuingia youtube na kuitazama video hiyo yenye urefu wa zaidi ya dakika 55.
Baada ya kuitazama na kuisikiliza video hii nimepigwa na butwaa. Kama Mhe Samia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia vyanzo vyake ameiona basi Mungu amuongoze sana ktk kurejesha upendo, Kwani kuna watu waliumizwa kwa kuonewa. Sidhani kama Furaha anaweza kulidanganya Taifa.
Furaha amenipa msamiati mwingine mpya. Amesema katika awamu iliyopita kulikuwa na KUPE. Amesema wapo watu waliokuwa wanamjua vizuri Mhe Magufuli kuwa ni mtu ambaye ukimpa taarifa hata kama umemdanganya lakini kama hajui kuwa unadanganya basi yeye alikuwa anaamini sana taarifa za mwanzo. Amesema wapo wengi aliwaumiza Kwa sababu ya kupe waliokuwa wakindanganya na walikuwa wanazisuka kama ni kweli kwa vielelezo vya kupika.
Amesema yeye alikuwa anaskitika kuna watu wapo hadi leo serikalini ambao mwanzo ndio walikuwa wanampelekea faili mbaya JPM juu ya Mhe Samia. Amesema moja wapo ya kupe mkubwa Rais Samia alimuondoa mapema kabisa alipoanza awamu ya sita. Ameendelea kusistiza kuwa wengi wa wale wanaondolewa na Rais anawajua na Rais anapiga mle mle. Amesema wengine ambao ndo walikuwa wapika taarifa za uongo leo tena ndio wanaongoza kucriticize baadhi ya mambo, akatolea mfano wa Mhe....
Furaha anasema kuwa wengine walipoona kuwa yeye Furaha anaweza kumwambia JPM kuwa hawa wanakudanganya walikuja wakafanikiwa kumchongea kwa JPM na wakatengeneza protocol ambazo ilikuwa ngumu kupenya kuongea nao.
Furaha anaongeza kwa kusema siku akikutana na Rais atampa orodha ya kupe wote waliokuwa wakienda Ikulu kilindi hicho na kumpotosha hayati. Anasema kupe hao waliwaumiza wengi na wengine JPM alipogundua anedanganywa alianza kuwarudisha kazini.
Hizi ni nukuu chache kati ya nyingi. Tafsiri yake ni nini? Tafsiri yake ni kuwa Kupe walifanikiwa kuliumiza hili taifa na kutengeneza migogoro kati ya jamii na serikali au chama.
Je, ni watu wangapi wapo jera pengine Kwa sababu ya hawa kupe waliompotosha Rais? Ni watu wangapi wana kesi kila namna Kwa sababu ya hawa kupe? Ni watu wangapi wamekosa teuzi, Ubunge na kufukuzwa kazi kwa sababu ya hawa ambao Furaha anawaita kupe? Tufakari.
Je, kuna uhusiano wa KUPE VS VIROBOTO au Kupe vs Wahuni?
Ninamuomba Mhe Rais kupitia vyanzo vyake Makini kuanza kuangalia namna ya kurudisha upendo ambao kupe waliuharibu. Na ikiwezekana hata kesi ambazo zipo Mahakamani au tuhuma ambazo bado upelelezi haujakamilika na zile ambazo upelelezi umekamilika lakini ushahidi ni wa kubumba DPP anaweza kuzifuta. Inawezekana zilitengenezwa na hawa kupe ili kuwadhibiti.