Furaha yetu sisi wanaume ni nini haswa?

Furaha yetu sisi wanaume ni nini haswa?

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2017
Posts
392
Reaction score
949
Kwa upande wa wanawake furaha yao ni kuolewa na kuzaa basi. Na endapo mwanamke atakosa hivi wanawake hupata maumivu makali na hujisikia kasoro kwenye jamii.

Ni maumivu gani aliyonayo Wema Sepetu au Lady Jay Dee kwa umri huo kukosa mtoto au watoto?
Kutokana na maumivu haya hupelekea wanawake aina kwenda kwa waganga kupata nguvu na uwezo binafsi, kwa kushindwa kuolewa mwanamke hujiona na nuksi au mkosi au kasoro. Ndio kitakwimu wanawake huongoza kwenye utafutaji limbwata ili amtukize mwanaume wake.

Upande wa kiumeni Sasa. Sisi furaha yetu ni nini?
1: Ni mwanamke?
2: Ni mali na fedha?
3: Ni mwanamke au wanawake?
4: Ni watoto na mbona sisi ndio magwiji wa kutelekeza Watoto wetu ukifananisha na wanawake?

Kama ni mwanamke, mbona sisi hata tusipo-oa tunaona shega tu? Na ni tofauti na wanawake waliozidi miaka 30 wanaopata stress za kuolewa. Sisi hatunaga wasi izidi isizidi ndio kwanza hatujali wala kwenda kwa waganga kusafisha nyota ili tuoe.

Furaha yetu sisi ni nini haswa?

Kama ni wanawake mbona tunawakatili kwa kuwafanyia vitendo vya kinyama na kikatili Sana? Unaweza ifanyia unyama furaha yako? Unaweza ikatili furaha yako?

Labda huenda ni Mali na fedha ndio maana kila kukicha tunazidamkia. Na tukishindwa tunaweka watoto zetu kafara na kudiriki ku-ua kabisa ili tuzipate. Muda mwingine tunadiriki kulala na mama zetu tupate hizo Mali na fedha. Muda mwingine kuiba, kukaba na kufanya ujambazi. Muda mwingine tuna-ua ma-albino tuzipate mali hizo.
 
Kulingana na roho ya mtu.

Ila asilimia kubwa ya wanaume furaha yao ni kukejeli wanawake wanapopata matatizohasa wanapotokea kuuawa na wanaume (chanzo nyuzi za mauaji ya wanawake ndani ya ndoa au nje ya ndoa),mabinti wanaobakwa au wanaopotea katika mazingira ya kutatanisha.
 
Ni mademu na bia tu. Na kuvipata hivyo inahitaji pesa nyingi. Kwa hiyo mwanaume furaha yake ni pesa nyingi sana. Yaani ni pesa nyingi sana

Wanaume twaweza terekeza wazazi, watoto, familia, mke ila hatuwezi telekeza pesa. Ndo maana tunaweka rehani chochote kwa ajiri ya pesa. Kuanzia roho zetu, roho za tuwapendao ilimladi tu tupate pesa. Kwa mwanaume ni hivi? HAKUNA KITAKACHOLINGANISHWA NA PESA TUKIONDOA UHAI NA AFYA

Lakini hapo kwa akina jd na wema umetudanganya

Wao ni wanawake huweziya image maumivu yao ungali we ni mwanaume labda kama wangekuja wanawake wenzao. Mama yangu anawatoto 7. Mi na mama yangu tunamjua jd ila ye jd hamjui mama yangu! Nani anafuraha hapo
 
Furaha ya mwanamme ni kumnyanyasa mwanamke.
Kumkatili mwanamke kwa kashfa masimango na kila aina ya unyanyapaa.
Pale aonapo mwanamke analia yeye hufurahi sana.
Furaha ya mwanamme ni kuhakikisha mwanamke anakuwa chini yake daima, maskini, mgonjwa, dependant kwa mwanamme.....
Kwa kumvunja nguvu na kumkatisha tamaa, kumvunja moyo, kumfanya dhalili na kuutweza utu wa mwanamke, kumshusha mara kwa mara akiukuza udhaifu wake mdogo.
Kwa sababu bila mwanamke uanaume wake haujakamilika.

Unyonge wa mwanamke ni mtaji na faida kwa mwaname. Na mwanamke akijipambanua kuwa yuko strong enough automatically katangaza vita na mwanamme!
 
Furaha ya mwanamke ni ndoa na mtoto?

Pengine katika jamii zetu za dunia ya 3 ambazo zinaamini kuolewa ni big deal.

Binadamu anabadilika. Kuna uwezekano mdogo wa kinachokupa furaha leo kikakupa furaha mwaka mbele.

Kama scenario yako ya furaha ya wanawake ni ya ukweli, then slowly hili linabadilishwa na uwepo wa watu kama JD, Wema, Lulu, Condoleeza Rice, Ellen D'Generes, Oprah Winfrey n.k.
 
Furaha yetu wanaume
1.Afya njema
2.Pesa
3.Pesa
4.Pesa
5.Pesa
6.Pesa
7.Pesa

hii dunia ukiwa huna pesa hata ukiwa kwny foleni ya kupanda gar pale ktuo cha mwendokasi unaonekana kama kibaka yan. kudadeq jaman tutafute pesa
 
Furaha ya binadamu yeyote ni kuwa na FURAHA.

Mwisho.

Sasa kila mtu ana kitu chake kinachompa furaha.
 
Back
Top Bottom