Furahia upishi wako na gesi janja (M-GAS) yenye mita janja wala huhitaji kununua mtungi wa gesi tena

Furahia upishi wako na gesi janja (M-GAS) yenye mita janja wala huhitaji kununua mtungi wa gesi tena

M-Gas ni kampuni inayoungwa mkono kimataifa. Tuna bohari zetu, mitungi ya gesi na magari ili kukuhakikishia kuwa unapata gesi (LPG)bora ya kupikia na huduma bora zaidi.

M-Gas inatumia teknolojia janja kubadilisha maisha kwa kukuuzia gesi safi ya kupikia kwa Mtanzania saa 24, siku 7 kwa wiki.

M-Gas hukupa mtungi uliyojaa gesi, mita janja, jiko la gesi na kadi maalumu ili usilazimike kulipa bei ya juu ya kununua mtungi na jiko la gesi.

Hivyo unaweza kulipia gesi unapohitaji kwa kutumia M-PESA. Unaweza kulipa kwa kiasi kidogo wakati huna pesa.
View attachment 2372479

(i) Lipia Kwa Simu View attachment 2372471
Mita janja ya M-Gas imeunganishwa na M-Pesa. Mara tu unapoweka akaunti yako ya M-Gas kwa kutumia M-Pesa, kiasi hicho husoma kwenye mita.

(ii) Teknolojia Ya Mita Janja View attachment 2372473
Huna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu kukosa gesi au pesa. Mita janja hukuonyesha kiasi cha gesi kilichobaki kwenye mtungi wako na ni kiasi gani cha pesa ambacho umebakisha kwenye akaunti yako.

(iii) Ada Ya Mwanzo ni Bure View attachment 2372475
Unajua jinsi ilivyo ghali kununua mtungi wa gesi na jiko kwa pamoja. M-Gas hukupa jiko na mtungi kwa pamoja bure.

(iv) Lipia Gesi Kadiri Unavyotumia (Pay-As-You go)
Mita janja hukuruhusu kununua gesi kuanzia kiasi kidogo cha Shillingi Elfu Moja (TSh 1000) kwa kutumia M-Pesa. Unaweza kulipa tu kwa gesi unayohitaji leo.

(v) Furahia Upishi Safi na M-Gas View attachment 2372477
M-Gas ni safi kuliko mafuta ya taa au mkaa au kuni; Ni nzuri kwa afya yako na wale uwapendao. Sasa unaweza kufurahia upishi rahisi na safi ukitumia M-Gas.

(vi) Huduma Ya M-Gas Inavyofanya kazi

(a) Unawekewa mtungi mpya wa gesi, mita janja na jiko nyumbani kwako.

(b) Tunahakikisha kuwa imewekwa vizuri na salama.

(c) Unalipia gesi unayohitaji kwa kutumia M-PESA. Mita janja inakusaidia kutoa gesi.

(d) Unaweza kufurahia kupika chakula chako bila harufu ya mafuta ya taa au mkaa au kuni.

(e) Gesi inapokaribia kwisha kwenye mtungi, mita janja itatuma taarifa kwenye kampuni. Tutapanga ratiba ya kuja kukubadirishia mtungi uliojaa gesi bure kabisa.
View attachment 2372474
Karibuni M-Gas ufurahie upishi wako kwa kiasi chochote cha pesa ulichonacho.

Kwasasa M-Gas tunatoa huduma mkoa wa Dar Es Salaam tu.

Kwa mawasiliano zaidi na ushauri jinsi ya kutumia M-Gas: 0747744895
Huduma ya kijinga sana hii. Kuna wenzenu wanajiita kopa gas ndio ovyo kabisa. Yaani gas ya 5k unaweza hata usimalize kuandaa chajio. Wife analalamika sana. Yaani unahesabu moja,mbili,tatu..... Ndio pesa inavyoenda hivyo. Gas ya buku, hesabu mpaka buku, gas imeisha. Mtakuja kunikumbuka. Nyie ingieni mkenge tu
 
Najuta kujiunga na nyinyi.Nilikuwa nikijaza jiko la gesi ndogo kwa sh 23000 natumia mwezi mzima lkn humu m-gas imekula 50000 kwa mwezi kwa matumizi yaleyale! Nimejirudia home!
Unatumia jiko lako mwenyewe au ni la M-Gas boss?
 
Huduma ya kijinga sana hii. Kuna wenzenu wanajiita kopa gas ndio ovyo kabisa. Yaani gas ya 5k unaweza hata usimalize kuandaa chajio. Wife analalamika sana. Yaani unahesabu moja,mbili,tatu..... Ndio pesa inavyoenda hivyo. Gas ya buku, hesabu mpaka buku, gas imeisha. Mtakuja kunikumbuka. Nyie ingieni mkenge tu
Boss, gharama ya jiko ulishamaliza au bado?
 
Nadhani hapo kuna gharama ya jiko ndio maana gesi inaisha haraka.
Samahani ila hutojali ungesema kama bado unadaiwa, gesi ya 1000 itaisha kwa sec kadhaa na kama hudaiwi gesi ya 1000 itaisha kwa sec ngapi. Tuzungumzie kwenye jiko lenu likiwa limefunguliwa ges hadi mwisho
 
Back
Top Bottom