boniuso
JF-Expert Member
- Mar 13, 2013
- 786
- 1,043
MAKOSA 3 AMBAYO WATU WENGI HUFANYA WANAPOWEKA MALENGO
Kila mtu hujiwekea malengo yake kwa kukusudia kubadilisha maisha yake lakini malengo mengi huwa hayatimii
Watu wengi huwa hawajifunzi ila huiga na kufanya vitu kwa sababu wameona kuna watu wanafanya
Kama utakuwa miongoni wa watu wengi duniani ambao hufanya makosa hayo ndio sababu unapoteza hamasa ya kutimiza malengo yako
Makosa hayo ni
1. KUFANYA VITU KWA KUIGA
Watu wengi hawana uwezo mkubwa wa kufikiri hivyo hufanya lolote ambao huona watu wengi wanafanya
Ukiona fursa ambayo kila mtu anaikimbilia ujue hiyo sio fursa
Siku zote fursa haiwezi kuonekana kwa watu wengi
Ingekuwa fursa zipo kwa ajili ya watu wengi kila mtu angekuwa amefanikiwa sana
Kwa sababu fursa zipo sehemu ambazo watu wengi hawazijui ndio sababu watu wengi huiga tu akiona mtu anaandika kitabu na yeye anaandika,akiona mtu anauza nguo na yeye anauza, akisikia mtu amekuwa na pesa kwa kuimba nyimbo na yeye anaimba, akisikia biashara ya mahindi inalipa anaingia kichwa kichwa.
Wengi huanza kwa kubwa saa ndani ya muda mfupi hukata tamaa kwa sababu uwezo wao kufikiri ni mdogo sana huangalia matokeo tu kama sababu ya wao kufanya kazi badala ya kuangalia mchakato.
Watu hutamani sana mafanikio lakini hawapo tayari kulipa gharama za mafanikio hayo.
Wapo huteseka sana na huishia kusema nataman niwe na furaha kama wengine lakini hana juhudi zozote kuondokana na huzuni hiyo
Hurejea maisha yaleyale kila siku huku akitarajia matokeo mazuri
Kutarajia maisha kubadilika wakati upo vilevile ni kuchanganyikiwa
Usiwe sehemu ya watu wengi 85% ya watu duniani hawana furaha katika kazi zao kwa maana wanafanya kazi ili kuishi tu kwa sababu wanapata pesa kwenye kazi hizo.
Ukiwa na tamaa ya vitu kutoka nje yako kama pesa, pongezi, kusifiwa, watu kukushangilia hizo ni motishq na hamasa za muda tu endapo vikiondolewa utapoteza hamasa ya kazi na utakata tamaa.
Watu wengi huanzisha vitu na kuishia njiani kwa sababu hawajui siri ya kuendelea na mapambano ipo kwenye hamasa ya kwako wewe sio hamasa kutoka kwa motivational speaker au watu waliokuzunguka.
Watu waliokuzunguka hawawezi kukupa furaha ya kazi kama wewe huipendi kazi yako.
Ukifanya vitu kwa sababu unapata pesa siku pesa ukikosekana huwezi kuifanya kazi hiyo.
Watu zaidi ya 99% duniani hufanya kazi za ndoto zao kwa sababu wameona wengine wamefanikiwa na wengi huingia kichwani kichwa kwa sababu wanataka mafanikio makubwa sana kama ya wengine hivyo huruka step wanataka kukimbia kabla ya kutembea.
Ukianzisha pharmacy kwa lengo uuze dawa utalazimisha hata ambao sio wagonjwa wanunue dawa.
Ukiandika kitabu kwa lengo uuze tu utawalaumu watu kama hawanunui
Ukianza kucheza mpira kwa sababu umeona waliofanikiwa endapo hautapata mafanikio haraka utakata tamaa
Hakuna mtu ambaye amefanikiwa bila kupitia maumivu hivyo ondoa tamaa ya mafanikio badala yake furahia mchakato wa mafanikio
Kwako mafanikio iwe zawadi sio lengo
Kumbuka malengo 9 kati ya 10 huuwa hayatimii
2. KUWEKA TAMAA YA PESA
Watu wengi huwa na tamaa kubwa sana ya mafanikio ya kiuchumi kuliko uhalisia wenyewe
Akiona kuna mtu amependeza hutaka kuiga kile anafanya mwenzio akifikiria kuwa atakuwa kama yeye kwa kulala na kuamka
Kitu pekee unaweza kuanzia juu ni kuchimba shimo
Ila kitu chochote chenye thamani huwezi kukipata kwa kutamani kukipata
Huwezi kuwa mrefu au mfupi kwa kutamani kuwa hivyo
Ukianzisha biashara kwa lengo upate pesa hiyo biashara imekushinda
Ukiandika kitabu kwa lengo upate pesa hivyo kitabu huwezi kukiuza
Ukitafuta kazi kwa lengo upate pesa kazi imeshakushinda
Watu wengi ambao hukata tamaa na maisha ni kwa sababu ya tamaa ya pesa kwa haraka ndani ya muda mfupi
Ukweli ni kuwa hakuna binadamu ambaye ni mwenye furaha saa 24 hayupo na hawawezi kutokea
Kitu chochote ambacho utafanya kwa lengo upate pesa tayari kimekushinda kwa sababu usipopata pesa kwa muda uliotarajia tayari nguvu ya kufanya kazi inaondoka
Watu wote ambao huishia njia kwenye malengo yao sababu kubwa ni kutaka pesa kwa haraka
Ukweli ni kuwa hata kama utakuwa bingwa kiasi gani kama huwezi kuvumilia maumivu wakati ambao watu wengi wamestarehe huwezi kufanya chochote chenye maana
Kama unaishi kwa kufuata utaratibu unaotumika kwa watu wengi sahau kuishi maisha yenye furaha
Huwezi kuwa na furaha wakati unatumia muda mrefu kukaa na watu wenye hasira na wenye kulalamika kila wakati
Huwezi kuwaa na furaha wakati unakaa unajisema kwa mabaya ambayo unapitia
Huwezi kuwa na furaha wakati unajilaum sana kwa makosa ya zamani
Watu wengi hawapo tayari kupokea ukweli hivyo hupata hasira wakiambiwa ukweli
Wengi hutafuta majibu ya kufurahisha ili tu wajisikie furaha
Wapo wengi wenye msongo wa mawazo lakini hawapo tayari kuweka muda kukabiliana na msongo wa mawazo hivyo hutafuta njia za mkato ili kuondoa matatizo yao
Ukiwa na tamaa ya mafanikio ya haraka utateseka sana
Maisha sio vile unapanga wewe ni vile yamepangwa
Ukipuuza hekima ni wewe unakwenda kuteseka
Hekima huweza kumfanya mtu kuona maisha katika uhalisia wake badala ya kufuata mkumbo
Hekima ndio msingi wa mafanikio popote
3. KUACHA KUJIFUNZA VITU VIPYA
Kama unajua kusoma lakini husomi huwezi kutofautiana mawazo na mtu ambaye hajui kusoma
Utagundua kuwa wengi waliosoma huwa wenye mawazo sawa na wale ambayo hawajasoma kwa sababu hawana muda wa kujifunza vitu vipya
Huona cha darasani kimetosha
Neno hekima lipo katika kuhakikisha unapata utulivu wa akili
Katika watu wa kale waliita hekima kama falsafa ambapo ni neno Philosophy yenye maana ya Philo= Love au kupenda
Sophia yenye maana ya Hekima
Kwenye imani ya uyahudi neno hekima huitwa Chokmâh. Kwenye imani ya kiislamu neno hekima huitwa Hikma kwenye imani ya kigiriki neno hekima huitwa Sophia ambalo limezua neno Philosophy kwa kilatino hekima huitwa sapientia (sapiens yenye kuleta neno homo sapiens)
Kwenye ukristo neno hilo hupatikana katika Proverb 4:7
Kwa imani ya Buddha neno hekima huitwa PRAJNA
Watu wa kale miaka zaidi ya 2000 walifahamu kuwa ukikosa utulivu wa akili kila kitu kinakwenda hovyo
Hakikisha unapata utulivu wa akili
Mafanikio yapo kwenye kutatua matatizo ya watu endapo huwezi kutatua matatizo ya watu lazima utakuwa na tamaa ya kupata mafanikio ya haraka
Huwezi kudumu kwenye mafanikio kama huna motisha ya kutoka ndani ya moyo wako
Hakuna motivational speaker anaeweza kukupa hamasa kisha ukafanikiwa kama huna hamasa ya ndani ya moyo wako
Kama hupendi kazi yako huwezi kuiboresha
Kama unaenda kazini kwa sababu unalipwa huwezi kuiboresha kazi yako kama pesa haitakuwepo
Kama ndoto yako ni kuwa na pesa hiyo itabaki kuwa ndoto kwa sababu vikwazo hufanya watu kukata tamaa haraka
Kitu pekee cha kukuwezesha kuendelea na ndoto yako pale huoni matokeo mazuri ni hamasa ya ndani ya moyo wako
Unafanya kazi kwa sababu unaipenda sio kwa sababu unalipiwa
Watu huiga kazi bila kujua sababu ya kuifanya kazi hiyo
Kama sababu ya wewe kuanzisha biashara ni kupata pesa basi huweza kufanikiwa eneo hilo kwa sababu ukikosa pesa tu kwenye majaribio ya mwanzo tayari utapoteza hamasa na utakata tamaa
Unakata tamaa kwa sababu unataka matokeo ya haraka sana
Tumia hekima sio hisia katika kuendeleza kazi zako
Kupata kitabu cha
1. FIKRA ZAKO FURAHA YAKO (softcopy)
2. TIBA YA MSONGO WA MAWAZO (hardcopy & softcopy)
3. BADILI FIKRA ZAKO BADILI MAISHA YAKO (hardcopy & Softcopy)
4. MALEZI YA UBONGO KISAYANSI (hardcopy & softcopy)
5.TABIA ZA WATU WALIOFANIKIWA (Hardcopy & softcopy)
6. MISINGI 10 YA FURAHA SIKU ZOTE (hardcopy &softcopy)
+255766862579
+255622414991
Imeandikwa na Psychologist
Said Kasege
Temeke, Dar es salaam