Fursa gani zinadharauliwa lakini zinaweza kukutoa kimaisha?

Hii nimeifanyia kazi mkuu, sijachimba kisima ile nimenunua lile simtank napakiza
kwenye Pickup.
Sawa mkuu hongera kwa kujiongeza, ila kama kijiji chenye shida ya maji kiko mbali sidhani kama utaweza kufikisha huduma.
 
mtaji wake unaendaje..
 
Yaani mkuu kila ninapofikiria kuhusu hiyo Project naiona kama ngumu sana
nimewahi kuwaza kujaribu lakini naiona kama inahitaji utaalamu mkubwa
lakini nitaifuatilia.
mkuu unaweza nipa ajira ya kukufanyia utafiti then nikaja na mpango wa biashara ulokamilika
 
biashara ya kutengeneza bio gesi na kuwasambazia wanakijiji wa karibu ka vile unasambaza maji, kikubwa ni kuwa na kisomea gesi kujua wametumia kiasi gani then unachukua chako, ni nzuri zaidi kwa wale wanye mifugo mingi hasa ng'ombe au wenye vyoo vya biashara
 
Hivi ni kweli kuku wakifikisha wiki ya nne na tano wanakula kama mchwa,je ukiwa na Kuku 1000 wanakula mifuko mingapi ya kg 50 kwa siku.Je masoko ya kuku wa nyama na mayai ya kuku wa kisasa yakoje.
 
 
Nimefuga kuku aina ya kroiler aisee wale ndege wanakula sijapata kuona nashukuru nimeweza kuwatoa wote na sasa nataka nihamie kwenye kuku wa nyama(broiler).
Wapo Sasso unaweza ukalia
 
Mkuu hii project vipi unauzoefu au utaalamu nayo?

Maana zamani sana marehemu Mzee alikuwa anajiandaa kufanya!
 
mkuu hii biashara ya chips naifanya dah naona 2 watu wanadharau ila mapato yake ni sawa na mfanyakaz anaelipwa 1.5 net income , ila nawaonaga wakitoka ofisin wanadharau hawajui kitu gani napata
Mkuu tupe details zaidi, huwa naitamani hii biashara
 
Kila sIku nafikiria kuanzisha biashara ya kukaanga mihogo maeneo ya Posta. Mihogo yenyewe inaweza kuwa sio fursa sana ila fursa itakuwa kwenye matangazo ya hiyo muhogo.Nitatangaza kuwa mihogo hii inaongeza nguvu za kiume. Hapo ndipo fursa ilipo..


Ha ha ha, hapo lazima utoboe. Lakini ukweli ni marketing, ubunifu ni muhimu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…