Fursa gani zinadharauliwa lakini zinaweza kukutoa kimaisha?

Fursa gani zinadharauliwa lakini zinaweza kukutoa kimaisha?

Hii nimeifanyia kazi mkuu, sijachimba kisima ile nimenunua lile simtank napakiza
kwenye Pickup.
Sawa mkuu hongera kwa kujiongeza, ila kama kijiji chenye shida ya maji kiko mbali sidhani kama utaweza kufikisha huduma.
 
Industry yenye moto ss iv ni e-sports ( online video game competition) video games kwa ujumla, artificial intelligence na crypto currencies, kwa kifupi kutatua changamoto za watu kwa kutumia technolojia.Kati ya hizi nilizotaja mm nimewekeza kwenye video games, zina addiction viby kwaiyo pesa zinanifata tu zenyewe. Toka nimeanza hii wiki ya tatu nahisi, minimum kwa siku haishuki chini ya 40k.
mtaji wake unaendaje..
 
Yaani mkuu kila ninapofikiria kuhusu hiyo Project naiona kama ngumu sana
nimewahi kuwaza kujaribu lakini naiona kama inahitaji utaalamu mkubwa
lakini nitaifuatilia.
mkuu unaweza nipa ajira ya kukufanyia utafiti then nikaja na mpango wa biashara ulokamilika
 
biashara ya kutengeneza bio gesi na kuwasambazia wanakijiji wa karibu ka vile unasambaza maji, kikubwa ni kuwa na kisomea gesi kujua wametumia kiasi gani then unachukua chako, ni nzuri zaidi kwa wale wanye mifugo mingi hasa ng'ombe au wenye vyoo vya biashara
 
Haha ha ha ha ha Watu wanawachukulia kuku Rahisi sana!! Kuku wanalipa sana lakini
sio mtaji wa kitoto ule, Inatakiwa ukaze msuli kwelikweli uache mambo yako mengi na
uwe na 'usiriasi' hautaki masihara, nikianza kuelezea hapa ninavyowajua wanJF wataanza
kuniuliza kwanini umeacha kufuga.
Hivi ni kweli kuku wakifikisha wiki ya nne na tano wanakula kama mchwa,je ukiwa na Kuku 1000 wanakula mifuko mingapi ya kg 50 kwa siku.Je masoko ya kuku wa nyama na mayai ya kuku wa kisasa yakoje.
 
Nikumbushe kisa kimoja cha ukweli kabisa ingawa ni cha siku nyingi. Yupo mchaga mmoja
ambaye alikuwa amebahatika kupata ajira hapa Jijini, baada ya muda fulani akaamua
kutafuta sehemu ambayo alifungua banda la chipsi. Alimwita mdogo wake kutoka nyumbani
Moshi akamweka hapo. Baada ya Muda fulani yule bwana akapata Likizo, akaamua kumsaidia
mdogo wake shuguli za chips.

Kwa mapato aliyoyaona muda huo mfupi akashtuka sana, akaamua kuacha kazi ili afanye
biashara hiyo ya Chipsi jambo ambalo lilileta mzozo na baba yake mzazi ambaye hakukubaliana
kabisa na mpango huo huku akisisitiza kuwa yeye hakumsomesha aje kuuza chipsi.

Yule Mchaga hakukubali, akaacha kazi na akafungua 'senta' nyingine ya Chipsi.....

Tuachane na huyo mchaga hebu nirudi kwenu wadau naomba tupeane uzoefu hapa
ni fursa gani ambazo macho ya kawaida haizioni kuwa Fursa za maana lakini zinaweza
kukupaisha Kimaisha?
 
Nimefuga kuku aina ya kroiler aisee wale ndege wanakula sijapata kuona nashukuru nimeweza kuwatoa wote na sasa nataka nihamie kwenye kuku wa nyama(broiler).
Wapo Sasso unaweza ukalia
 
biashara ya kutengeneza bio gesi na kuwasambazia wanakijiji wa karibu ka vile unasambaza maji, kikubwa ni kuwa na kisomea gesi kujua wametumia kiasi gani then unachukua chako, ni nzuri zaidi kwa wale wanye mifugo mingi hasa ng'ombe au wenye vyoo vya biashara
Mkuu hii project vipi unauzoefu au utaalamu nayo?

Maana zamani sana marehemu Mzee alikuwa anajiandaa kufanya!
 
Kila sIku nafikiria kuanzisha biashara ya kukaanga mihogo maeneo ya Posta. Mihogo yenyewe inaweza kuwa sio fursa sana ila fursa itakuwa kwenye matangazo ya hiyo muhogo.Nitatangaza kuwa mihogo hii inaongeza nguvu za kiume. Hapo ndipo fursa ilipo..


Ha ha ha, hapo lazima utoboe. Lakini ukweli ni marketing, ubunifu ni muhimu sana.
 
Back
Top Bottom