Mada kama hizi ndizo zinazotakiwa kujadiliwa maana zinakomboa watu. Kwa upande wangu, acha ni-share na wana, kwanza biashara ni kujitoa na kujiwekea malengo yanayofuatwa na NIDHAMU.
Nilipokuwa chuo nilianzisha biashara baada ya kuona nina uhitaji mkubwa wa pesa. Kwakuwa nilikuwa napata mkopo, nikaona niutumie huohuo kama mtaji. Kwanza nikatazama watu wanaonizunguka, nilikuwa naishi HOSTEL za nje, nikabaini kuna Mlinzi ambaye nilikuwa nimezoeana naye, yeye pamoja na mkewe. Basi hapo nikapata wazo la kuuza chakula kwaajili ya wanachuo ambao wanakaa kwenye mahostel yote, ya chuo na nje ya chuo.
Si kwamba hakukuwa na ma-canteen wala sehemu zingine za kula, lah! Ila mimi nilikuwa nataka nifanye tofauti kwa kuwapelekea watu vyakula mpaka mlangoni mwao, wanafunzi wa chuo wanapenda luxury life na wengine huwa wanatingwa kiasi kwamba anaona kutoka kwenda kufuata chakula anapoteza muda.
Nikamtumia yule mlinzi na mkewe. Mkewe akawa anapika. Nadamka asubuhi mno kwenda machinjioni kudaka nyama. Napitia na mchele na mahitaji muhimu sokoni, si kila siku lakini, kisha nafikisha mahali panapohitajika na kisha naenda zangu chuo.
Nilikuwa nahimiza sana chakula kipikwe kama cha nyumbani, kiwe kizuri na bei sawa na ya kule wanapokula kwengine. Japo faida ni ndogo lakini nikiipata kwa wingi SI HABA.
Basi nikachapa vikaratasi vingi sana nilivyoandika,
"JE, UNABANWA NA ASSIGNMENTS? UMECHOKA KUPIKA NA PIA KULA VYAKULA SUBSTANDARDS? USIJALI, PIGA SIMU AMA TUMA UJUMBE WA JINA LA HOSTEL NA NO. YA CHUMBA, UTALETEWA CHAKULA UPESI!"
Vipeperushi hivyo nikavisambaza sana na simu nikawa nazipokea. Nabeba chakula mwenyewe pamoja na mlinzi tunasambaza kiasi chuoni wengine wakawa wananiita kaka chakula.
Changamoto zipo, kuna siku za mwanzoni nilikuwa namwaga chakula kwa kukosa wateja. Nilikuwa nina msimamo, mtu akipiga simu saa nne kutaka chakula nilikuwa namwambia kimeisha hata kama kipo. Nilifanya hivyo kuwatengenezea belief kuwa chakula ni kizuri na inabidi wawahi kuweka orders.
Pia maneno ya wateja huwa hayakosekani na dharau za wanafunzi wenzangu vilevile!