Fursa: Mifuko ya nailoni imepigwa marufuku ni Wakati wetu sasa kutafuta kitu mbadala

Fursa: Mifuko ya nailoni imepigwa marufuku ni Wakati wetu sasa kutafuta kitu mbadala

fikirini nje ya box nyie, acheni ushamba!!!
kwahiyo mnategemea hizo karatasi zenu ndio ziwe full replacement ya mifuko ya "Rambo/Marlboro".

assume umeenda kwa soko umenunua mchele kilo 3, unga kilo 2 na nusu, ndizi robo mkungu, nyanya za 1500, na chainizi za 1000 (ambazo hazijakatwa katwa). Je, hutu tukaratasi twenu tunaweza kuhimili vitu hivyo???

mmeona sasa ambavo hamfikirii nje ya box.
 
Conclusion:
huto tumifuko twa karatasi ni special kufungia chipsi kavu na mishkaki vibandani. Full replacement ya "Marlboro" ni kitu kingine kabisa.
 
Habari za hapa wakuu

Kama mnavyojua mifuko ya plastic(nylon) zote zimepigwa marufuku miezi michache baadae zitaacha kutumika,hilo haliondoi sababu kwamba lazima watu madukan wapimiwe sukari,unga,maharagwe,mandazi n.k nusu,robo,kilo n.k

Vijana hii ni fursa kwetu kuja na idea nzuri yakureplace mifuko ya nylon,inatumika sana,soko ni uhakika kwa 95%.

Kwa upande wa kufungia vitu dukan nina idea ya zile bahasha flani hivi nyepesi za kakii...kwa wale wanaonda kuchukua vitafunwa kwenye migahawa mikubwa na ya kati wanazijua. Bahasha flani hivi kama za pembe nne, ile ni fursa ndugu zangu.

Nawakaribisha wataalamu wa mambo wanaojua upatikanaji wa mashine ya kutengeneza zile bahasha,bei, n.k

Karibuni

Sent using Jamii Forums mobile app

Wewe unaona fursa baada ya marufukue, wenzako tumesababisha marufuku ili tuuze, ushachelewa
 
hiyo mifuko yenu inaweza kubeba kilo tatu za mchele na tikiti maji la 2000 wakati natoka sokoni??
Nadhan kwa sasa kuna umuhimu wa kununua makapu kwaajili ya mahitaji ya sokoni ,maana iyo mifuko ni kwaajili ya kuwekea vitu vyepesi na visivyo na unyevu wa aina yoyote
 
Miaka ya zamani kabla ya mifuko ya plastic kua maarufu,hii mifuko ya karatasi ilikua inatengenezwa sana,tena manual tu!

Mahitaji ni mifuko mitupu ya cement,gundi ya maji na kisu cha kukatia,unachukua mifuko ya cement unatoa zile layer mbili za juu coz zinakua chafu,pia unatoa layer ya ndani,ile mifuko huja na layer za karatasi nyingi tu,sijui kwa mifuko ya cement ya siku hizi inakujaje,

So,zamani mifuko hiyo ya karatasi ilitengenezwa sana tu mitaani,ila sina uhakika kuhusu usalama wake wa kiafya kwa kubebea hasa vyakula.
 
Nadhan kwa sasa kuna umuhimu wa kununua makapu kwaajili ya mahitaji ya sokoni ,maana iyo mifuko ni kwaajili ya kuwekea vitu vyepesi na visivyo na unyevu wa aina yoyote
hata ukinunua makapu bado uhitaji wa mifuko utakuepo mfano umenunua bidhaa tofauti tofauti sokoni huwezi zimix zote kwenye kikapu, lazima kila bidhaa utaiweka kwenye mfuko wake
 
je. Hizi karatasi zenu ni kwa ajili ya kufungia chipsi kavu na mishkaki tu ama hata kichani kimoja cha ndizi bukoba, maembe na nyanya zinabeba.
ama nyie mnaangalia kufungia chipsi tu!!
Nadhani hata kufungia chips hazifai, sana sana kuwekea sukari na unga! Ila ngoja tuone...
 
Conclusion:
huto tumifuko twa karatasi ni special kufungia chipsi kavu na mishkaki vibandani. Full replacement ya "Marlboro" ni kitu kingine kabisa.
Nionavyo, muemeaji unakuwa nakikapo chako kikubwa alafu bidhaa utakazo zinunua zinawekwa kwenye hizo karatasi alafu unatumbukiza kwenye kikapu chako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawasikitikia wanaokaa magorofani,maana walishazoea kurundika uchafu kwenye mifuko ya plastiki na kuishusha chini baada ya siku mbili au tatu,sasa hiyo mifuko mipya sijui itakuwa ya materials gani...
 
sidhani kama kuna paperbag ya kubeba tikiti maji au boga kwa mfano,sasa sijui babu zetu waliishije kabla ya plastic bag,as kwa kubeba kikapu haiwezimake,nani atakuwa anabeba kikapu mtaani mda wote,inabidi twende semina elekezi zanzibar kwanza
 
sidhani kama kuna paperbag ya kubeba tikiti maji au boga kwa mfano,sasa sijui babu zetu waliishije kabla ya plastic bag,as kwa kubeba kikapu haiwezimake,nani atakuwa anabeba kikapu mtaani mda wote,inabidi twende semina elekezi zanzibar kwanza

Kaka nessonlegend umeona na hii comment ya mdau hapa??
Sasa sijui una maoni gani.
Mie bado naona mifuko ya "Marlboro" inasaidia sana, japo inachangia uchafuzi wa mazingira.
Hebu fikiria umetoka kazini unaamua upite sokoni kununua nahitaji ya family, huna kikapu. Utafanyeje??
Bado sijaona "suitable" replacement ya mifuko hii.
 
Nimeiona, baada ya kuwa na kapu zile za entaprenyuuuua ndiyo utatumia mifuko ya kaki sasa kugawa vitu

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa mantiki yako nilivokuelewa ni kuwa:
Either inabidi tuwe tunatembea na makapu mitaani, ili ikitokea unahemea vitu usipate tabu ya kurudi nyumban kufata kikapu.

La sivyo, tuwe tunaingia gharama kununua makapu mengi each time tuko mbali na home na tunataka tuhemee. Yaani assume unataka kununua kilo tatu za mchele (mfano tu) hakuna mfuko wa karatasi unahimili mzigo huo. Hivo basi itakubidi hapohapo dukani ununue kikapu (cha 5,000 kwa mfano) ili ubebee mzigo wako.

Does it make sense???
 
Naona kuna umuhimu mkubwa sana kwa serikali, kutoa elimu bure kwa wananchi wake.... Inabidi ifanye hivyo, ikiwa ni moja ya mipango mkakati wa kutimiza mipango yake ya kubadili aina ya vifungashio.

Maana inaonyesha wazi kwamba, bado watu wana uelewa mdogo sana, juu ya hivi vifungashio talajiwa(paper bag).

Ila kwa ufupi tu, naomba niseme kwamba...si kweli kwamba vifungashio hivyo talajiwa (paper bag), ni vifungashio vitakavyo kuwa baguzi kwa baadhi ya matumizi. Maana vifungashio hivyo vya karatasi, vipo vya aina mbalimbali, material tofauti tofauti na ukubwa tofauti tofauti. Kwa msingi huo ni wazi kwamba, vinaweza kutumika kwa kubebea vitu tofauti tofauti bila shida yoyote ile.

Hivyo nadhani kwa suala hili, ni vema tukaunga mkono juhudi za serikali. Maana ni jambo la kheri na ni imani yangu kwamba, suala hili litaenda kupunguza baadhi ya hadha kubwa, zilizokuwa zikiwakumba wananchi wengi, katika maeneo tofauti tofauti ya nchi yetu.

Napenda kumalizia kwa kutoa pongezi kwa serikali hii ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa hatua hii muhimu walioichukua. Vilevile natoa rahi kwa watanzania wenzangu wote, tuwe na umoja na kuondoa tofauti zetu zote..ili kwa pamoja tuweze kupiga hatua hii muhimu, kwa mustakabali wa maendeleo ya taifa letu pendwa Tanzania.

"Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki watanzania".

Nawatakia usiku mwema, muwe na amani....kwaelini.

Asante.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom