Habari za hapa wakuu
Kama mnavyojua mifuko ya plastic(nylon) zote zimepigwa marufuku miezi michache baadae zitaacha kutumika,hilo haliondoi sababu kwamba lazima watu madukan wapimiwe sukari,unga,maharagwe,mandazi n.k nusu,robo,kilo n.k
Vijana hii ni fursa kwetu kuja na idea nzuri yakureplace mifuko ya nylon,inatumika sana,soko ni uhakika kwa 95%.
Kwa upande wa kufungia vitu dukan nina idea ya zile bahasha flani hivi nyepesi za kakii...kwa wale wanaonda kuchukua vitafunwa kwenye migahawa mikubwa na ya kati wanazijua. Bahasha flani hivi kama za pembe nne, ile ni fursa ndugu zangu.
Nawakaribisha wataalamu wa mambo wanaojua upatikanaji wa mashine ya kutengeneza zile bahasha,bei, n.k
Karibuni
Sent using
Jamii Forums mobile app