Fursa nchini Morocco: Biashara ya mbuzi inalipa sana

Fursa nchini Morocco: Biashara ya mbuzi inalipa sana

Kwa mbuzi mzima (live) hawezi kufika huko unless mtu utumie ndege. Option pekee hapo ni kuchinja lakini pia ukisema uchinje kikwazo ni hao waarabu watataka certification ya Halal


Tatizo la Tanzania ni ujinga ambao kwa kiasi kikubwa ulichangiwa na Nyerere na CCM yake huku akishirikiana na kanisa lake la kikatoliki.

Ujinga kuwa kila kitu cha mwarabu ni kibaya na hakifai kwa vile waarabu walitufanya watumwa.

Ujinga huu umeturudisha sana kiuchumi na nchi nyengine kutumia nafasi kibiashara.

Mfano mkubwa ni hii biashara ya mbuzi na kondoo. Kuna nchi kama somalia walikuwa na tenda kubwa ya kupeleka mbuzi Saudi Arabia na nchi nyengine za Kiarabu. Baada ya ujinga wao wa kupigana biashara ikafa na nafasi yao ikachukuliwa na Australia na New Zealand . Yaani mbuzi na kondoo kutoka Australia wanapelekwa uarabuni wazima na pia kuna Waislamu wa Australia na New zealand wanaokubaliwa na certificate kupewa ,wameajiriwa kuwachinja hao mbuzi na kondoo . Hata ukitembelea nchi za Europe utakuta zinauza nyama halali kutoka Australia na New zealand.

Tanzania baada ya kuja Samia kidogo amehuisha biashara ya nyama ya ng`ombe kwa kutembelea zile nchi . Huko amepata tenda nchi nyingi kama UAE, Oman, Qatar , na Saudi Arabia . Kidogo hii biashara imekuwa.

Mletaji mada nafikiri kama itawezekana kutembelea Saudi Arabia au UAE nafikiri ni vizuri kwani ukipata tenda unaweza ukapelekea pia kupata msaada wa kupata certificate hapa nyumbani mkubwa . pia siku hizi ndege zipo za kusafirisha
 
Niulizie na bangi mkuu kama inalipa
 
Kwenye nchi za kiarabu ikiwemo Morocco,kuna kiwanda kikubwa tu cha kuchakata nyama kinachomilikiwa na muhindi mkoani Arusha huwa kinafanya uchakataji na usafirishaji nyama (ya mbuzi tu) kwenda huko, kiwanda kina uwezo wa kuchakata hadi mbuzi mia tano kw sikuna bado wanasema soko mzigo hautoshi, ni biashara nzuri ila inahitaji mtaji mkubwa,, wat3ja huwa wanatoa order ya kuanzia mbuzi 100 na kuendelea,nilishajaribu kutafuta wateja huko kupitia Go4worldbusiness.com na nikawapata wengi tu, issue ni vigezo na masharti yanakuwa mengi huku mtaji pia ukiwa changamoto, asante kwa kutusanua tena.
Sorry naweza pata number yako?
 
Tatizo lao wanapenda kuzungumza kiarabu, hata km anajua kingereza atavunga, ila morocco kuna ela
Muhimu tuelewane. Hata akiongea "Kijerumani", kama mwisho wa mazungumzo tunafikia muafaka, hakuna shida kabisa!
 
Back
Top Bottom