Fursa ndani ya Babati - Manyara

Mkuu hakuna daladala ambayo haipigi kazi
 
We mwenyeji ndo umefafanua vzr
 
Mkuu nataka nije huko kuleta simu niwauzie wenye maduka bei ya jumla ntapata wateja kweli make mi ntakuwa nauza bei ile ile ya jumla ya kariakoo lakn mi namleteya mpaka mlangoni
 
Ndio sasahivi Babati kuna mchanganyiko wa watu wengi, Mashirika, Makampuni na Ofisi nyingi za Serikali zimeajiri watu wengi tofauti na wazawa achilia mbali wafanyabiashara. Fursa ni nyingi kwakweli[/QUOTE]

Mkuu vipi kuhusu saluni za kiume hiyo fursa inalipa? biashala ya mazao .Mahindi, unga(dona na sembe), Michele, maharage .Make na mpango was kufanya biashara pindi ntakapo graduate.
 
Mimi kwa sasa nipo Babati. Mtoa maada amedanganya kidogo. Ingawa ni kweli fursa zipo kwa sababu huu ni mji unaokua. Lakini kusema kuwa mitumba hamna si kweli....mitumba ipo kwenye madoksi...na pia sokoni (soko la mitumba) ipo na kuna watu pia huwa wanakata madeli....mpaka barabarani ipo mfano ..ukifika sehemu inaitwa kona mrara opposite na First and last utaona mitumba pemben ya barabara....kuhusu super market zipo lakini chache sana...Show room za magari hamna kabisa
 
Kuhusu Hiace...zipo sana tu...zipo Hiace/Noah kuelekea Katesh,Dareda,Bonga,Kiru,Galapo,Magugu na maeneo mengine. Kwa wawekezaji na wajasi karibuni sana, mje mfanye utafiti ...mnaweza pata cha kufanya.
 
Kwa upande wa vyuo kuna chuo kikuu huria...na kuna tawi la Chuo cha uhasibu cha Arusha...
Japo uwekezaji kwenye sekta ya elimu bado...pia tusisahau tabia za wasomi wengi hukimbilia kwenye miji mikubwa na majiji..
Kwa upande wa Garage fursa zipo...ila maduka ya jumla yapo ya kutosha (ukilinganisha na mahitaji)
 
Arusha ni mwendo wa masaa 2.5, Lakini je huoni kwamba hiyo ni moja ya Frusa?
Inaweza kuwa fursa,ila utokaji wa bidhaa ukawa changamoto mfano biashara ya magari utokaji wake si wa haraka,kwa mfano manyara unaweza ukakuta kwa mwaka mzima ukauza magari mawili,labda mtu aamue kuuza kwa mkopo
 
Nasikia huko kuna kilimo cha maharage ya ngwara. naomba ufafanuzi zaidi maana haya maharage ni big deal huko kenya
 
Tupe methodology na ukubwa wa sampuli kata na vijiji ulivyohoji
 
Nimetamani kuja kwa malengo yangu binafsi
 
Nondo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…