Fursa Singida kwa sisi Diaspora

Fursa Singida kwa sisi Diaspora

Mkuu nimeamua kurudi bila shuruti baada ya kukaa huku 12 years, pesa ilikuwepo ila imeisha kwenye bata sasa nimeamua kurudi sababu nimeshakuwa muhenga Sana!Nina cash 5mil ndio maana nataka nikimbilie singida maana najua Dar hata mwezi hautaisha nitakuwa nimefulia
Kwenu Singida?
 
Nimeshangaa diaspora anajiita muuza simu used, sijui alikua anaziuzia huko mbele while wazungu wanacheza na brand new.
Nikikwambia mm nilishawahi kuuziwa mche wa sabuni kwa kudhani kuwa ni Simu Portugal hutaamini sababu unadhania wazungu ni miungu watu!hii staili ya kuuziana miche ya sababu nilipigwa na wazungu Euro 100,kipindi BlackBerry zipo kwenye chati
 
Braza umeizunguka dunia si mchezo, endelea kutupa maneno.
 
Km tanzania ingekuwa binadam singida itakuwa sijuj kiungo gani??!!!maana pamekaa kichovu sana
Tanzania mikoa yote imekaa kichovu chovu hata dar asilimia kubwa ni kuchovu tu ukitoa POSTA OYSTERBAT MASAKI sehemu zilizobaki za wachovu tu
 
Nilipata viza fresh lakini ilikuwa ya ujanja ujanja lakini nilivyokuja airport tukawekwa pembeni mm pamoja na raia wawili kutoka Bangladesh tukakaguliwa nadhani walihisi labda nimebeba madawa ya kulevya baada ya hapo nikaanza kuhojiwa sikuwa na sababu zilizowaridhisha kukaa Japan

Natamani saana kujua undani wa hili saana sema haupo straight kunipa story nzima... maswali gani uliulizwa? Visa ilikuwa ya nini[tourist,business n.k]?

Kwanini walikuhisi umebeba ngada?
 
Hapana mkuu!sema nataka nikajifiche mikoa ya kinyonge
Acha ulofa,Singida sio mji wa wanyonge, nj center ya nchi ambayo kwa sasa ipo connected vizuri na barabara za lami na imechangamka vizuri. Sio Singida uliyoiona mwaka 2004. Nakhshauri kwa lengo lako hilo kajifiche kwenu mkuu.
 
Ukitoka bongo ukiwa na fantasy maisha mbele ni bwerere mshiko nje nje kama biko utaishia pabaya.

Toka bongo na notion ya kubadilisha mazingira ya utafutaji au na malengo ya kuishi nchi fulani..

Ila huyu jamaa naona mzinguaji ila atanisahihisha. amekaa South 10 years bila kutoka then uzi wa nyuma yake anakuambia anauza simu used yupo Msumbiji????
Chezea JF wewe
 
Acha ulofa,Singida sio mji wa wanyonge, nj center ya nchi ambayo kwa sasa ipo connected vizuri na barabara za lami na imechangamka vizuri. Sio Singida uliyoiona mwaka 2004. Nakhshauri kwa lengo lako hilo kajifiche kwenu mkuu.
Kwetu siwezi kwenda mkuu!watanipiga mizinga ya hapa na pale nitafulia kiurahisi
 
Natamani saana kujua undani wa hili saana sema haupo straight kunipa story nzima... maswali gani uliulizwa? Visa ilikuwa ya nini[tourist,business n.k]?

Kwanini walikuhisi umebeba ngada?
Mkuu Japan ni nchi ngumu Sana kuingia kizembe!mfano mm nilikuwa na visa ya tourist lakini show money hata 400usd ilikuwa haifiki,kuhusu maswali ni kama vile nilishtukizwa tu sababu sikuweka akilini kwamba hilo litatokea!mimi nilidhani ukishapata tu viza Africa basi amemaliza mchezo unaingia tu kama home,nadhani walihisi kama nimebeba madawa sababu nilikuwa nimevaa kibaharia buti kubwa bonge la jinsi(mapigo ya kipindi hicho)na uchovu wa safari ulichangia nilikuwa nimechoka balaa imagine 16hours upo angani
 
Mfano mm naweza chukua milion moja nikawekeza kwenye kununua magunia ya alzet mwezi wa 5 wanauza mpaka 30000 alafu unayapiga store mwezi wa kumi unauza kwa 70mpaka 60 alafu hiyo nyingine unaanza na nguo za wadada na wamama dukan ukishauza alzet faida unaweka dukani mtaji unahamisha kwenye biashara ya mahindi ni mwendo wa nafaka tu lakin lazma ufanye research ya masoko kwanza
Vipi wewe ni mzoefu katika biashara hiyo
 
Km tanzania ingekuwa binadam singida itakuwa sijuj kiungo gani??!!!maana pamekaa kichovu sana
Ila kumbuka No1 billionaire anatokea singida kwa hio acheni kusingizia mazingira mjasiriamali yeyote hutafuta mazingira yenye changamoto kubuni fursa karibu singida mkuu, ila kua makini na aina ya watu utakao chagua kua nao karibu.
 
Wakuu hii ni kwa ushauri tu kwa mtu kama mimi na kwa niaba ya ma Diaspora wengine ambao kwa hiari yetu tumeamua kurudi nyumbani kwa sababu ka umri kameenda kimtindo halafu tunazubaa tu kwenye nchi za watu!mfano kwa singida biashara gani ambayo inaweza kuwa inamzunguko mzuri?vp pia kuhusu biashara ya maduka ya nguo? Mtaji ni 5mil pesa zingine tumekula ujana huku huku
Njoo Iramba anzisha kilimo cha ukweli, Hardware ya maana pia nzuri.
 
Back
Top Bottom