Fursa ya biashara kwenye mafuta ya alizeti

Haya mafuta ya alizeti tunazalisha Tanzania kwa nini tuimport?

Ndugu yangu hata mimi ningependa tuzalishe zaidi ili kukidhi mahitaji lakini kwa bahati mbaya demand ni kubwa mara tano zaidi ya uzalishaji siyo tu kwa mafuta ya kupikia anza na sukari,unga wa ngano,na mengine mengi--
 
Hlo container la 40feet mnauza dola ngap?
weka na full bei ili tuangalie itatulipaje kama wafanya bisness

Ndugu yangu nakuwekea bei ya chupa moja CIF Dar es salaam Port-suala la ushuru sijaliweka utaangali wewe mwenyewe.Pitia madukani linganisha bei kama bei ipo safi basi tutangea zaidi

1L $1.32
2L $2.52
5L $6.1
 
Hlo container la 40feet mnauza dola ngap?
weka na full bei ili tuangalie itatulipaje kama wafanya bisness

Container 40 ft
Kama Chupa za lita moja pekeyake - 26 985
Kama chupa za lite 2 peke yake 12 520
Kama chupa za lita tano peke yake 5 160
 

Ukiweka na ushuru hapo inakuwa bora x100 umeenda kiwandani Singida na kuchukua alizeti yako saaaafi! Serikali hebu ifanye mkakati Wa maksudi kuinua kilimo cha alizeti hapa nchini. Wakulima wetu wanateseka na pamba wakati kuna mazao ya kuwainua kiuchumi haraka kabisa!!
 
Job ukiweka na ushuru still bei ya Msingida ipo juu kutoka na sababu nyingi tu wenzetu wameanza zamani kaka...kuna mapembejeo chungu mzima-hapo ndo utajiuliza kwa nini ukienda dukani utanunua dumu la litre tano kwa shillingi 22000TSH wakati wenzetu wakiingia supermaket wanakamata dumu la lita tano mafuta kwa shilingi 8000 za kitanzania unaona tofauti...still tatizo linakuja kuinua wakulima haitoshi inabidi kuinua uzalishaji wa kisasa unaendea na ubora wa kimataifa hilo gereni la lita tano unakuta mafuta yananuka bila vitunguu swaumu kuua harufu mama hawezi kupika...sikukatalii hoja yako mimi nipo na wewe..ila hoja yako by theoretical inawezekana kabisa lakini by practical nadhani bado...asante



 
Hivi soko la haya mafuta lipoje maana nna rafiki yangu ana lita kama 200 sasa anatafuta soko. Yeye yupo dodoma na kama ikiwezekana yupo tayar kusafirisha mpaka kwa mnunuzi. Ikiwezekana na bei ya soko kabisa.

Nawasilisha
 
Habari zenu.
Naombeni msaada nina mtaji wa milioni moja nataka kufanya biashara ya mafuta ya alizeti kutoka dodoma kuleta Dar.na hata ikibidi mikoa mingine.
Mwenye kuijua biashara hii naombeni msaada.
Asanteni
 
Labda nataka kujua Soko, ikiwa ni pamoja na Bei, Ukubwa wa soko na Changamoto Zake !
 
Kwa mahitaji ya mafuta ya ARIZETI jumla na reja reja kwa ujazo wa lita 5 tuwasiliane kwa 0652765670 au 0757995789
NB: Mafuta haya ni direct kutoka shamba na kwenda kukamuliwa mashineni,siyo kutoka viwandani lakini yana usafi wa hari ya juu.


Napatikana Mlandizi, bei ni:
1.Jumla ni Tsh. 15,000/-
2. Reja reja ni Tsh. 17,000/-
Yote ni kwa ujazo wa lita 5, ukihitaji unatoa
Order

KARIBUNI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…