Fursa ya Kilimo cha Korosho Manispaa ya Lindi

kumbe Tz imebarikiwa hata parachichi ina msimu tofauti na ulaya hivyo soko ni uhakika lakini bado watanzania tumelala.
 

Hii fursa bado ipo?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yele ya manispaa yaliisha kuna watu walitoa fedha wakarudishiwa baada ya mashamba kuisha. Mimi ni mmoja wapo wa aliyechangamkia hii fursa wakati vijana wenzangu wakiogopa kutapeliwa mimi nilikwenda manispaa physically na nikanunua ekari 100 maeneo ya Chikonji. Tangu February mwaka 2018 ilikuwa ni kazi ya kudondosha msitu mnene kwa kutumia chainsaws kama tatu hivi. Baada ya hapo ikafuatia kukatakata miti na kuikusanya na jua lilipoanza mwezi wa nane,2018 nikaanza kuchoma moto, ninaahukuru sasa hivi shamba ni jeupe na nimeingiza miche 2400 niliyoitengeneza mwenyewe kwenye kitalu. Plan ni kuotesha miche 3500 katika shamba langu lenye ukubwa wa 118 acres. Ninamshukuru Allah kwa kunifikisha hapo nilipofika ingawa nilijua itakuwa ni kazi ndogo ila ni kazi inayohitaji mtaji na kujitoa kweli kweli, ukizubaa wasimamizi wa shamba lazima waibe mafuta, vipuri vya mashine n.k.

Changamoto
1. Maji - mashambani hamna maji hivyo lazima maji ya vibarua na kunyeshea vitalu na miche shambani uyachote kijijini
2. Barabara
3. Uaminifu wa wasimamizi
4. Muda wa usimamizi

Mwisho nawashauri vijana wenzangu kutenda kwa vitendo na sio kwa maneno hapa jf. Tanzania ya viwanda inawezekana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza heshima yako mkuu,
Pili hongera kwa ujasiri uliochukua, nami kama kijana kuna la kujifunza hapa.
Binafsi nimechelewa sana kuon ahili bandiko hapa jamvini, kwa sababu ya kutingwa na shughuli za hapa na pale.
Naomba kama fursa itapatikana sehemu nyengine unijulishe, maana mimi mwenyeji wa kusini piaa..
 
Sawa mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado hatujajipanga vzuri kwenye kilimo cha biashara lolote laweza kutokea Leo wakulima wa korosho wanalia kama wahamiaji haramu hali kadharika kwenye mazao mengne imekuwa hivyo ,mahindi watu wanayo mengi sana hawaruhusiwi kuuza watakapo choroko,kunde,mbaazi yote wakulima hawaoni faida ya kilimo cha hayo mazao serikali haijajipanga kwa kilimo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu vipi hizo machine zinaweza kubangua kiasi gani kwa siku ? Ni mda umepita sasa vipi ulifanikiwa?

God save us
 
Hili vipi hali ya sasa huko. Naweza kupata kama heka 100?

Nataka kuanza huu mradi.



God save us
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…