Fursa ya Kilimo cha Korosho Manispaa ya Lindi

Fursa ya Kilimo cha Korosho Manispaa ya Lindi

Mahitaji ya soko ni tani 1000000 uwezo wa nchi ni tani 300,000 kingine tanzania msimu wa korosho ni wa pekee wakati huku zipo wazalishaji wakubwa ivory coast brazil wanakuwa bado fursa bado ipo saana na kama tukawekeza kuwa na viwanda, faida ita triple zaidi ya bei ya mibadani na hili ndiyo lengo
kumbe Tz imebarikiwa hata parachichi ina msimu tofauti na ulaya hivyo soko ni uhakika lakini bado watanzania tumelala.
 
Habari njema kwa wakulima wenye ndoto za kuingia kwenye kilimo cha korosho.

Mkurugenzi wa manispaa ya Lindi anawaalika watanzania wote wenye nia ya kulima korosho kuja katika halmashauri yake na kuunga mkono jitihada hizo.

Mpaka sasa Halmashauri imetenga heka 45,000 kwa ajili hiyo mnaweza kuwa mnajiuliza inakuwaje mjini kukawa na mashamba naomba muelewe kuwa manispa ya lindi ndiyo manispaa inayoongoza kwa ukubwa tanzania jiji la mwanza lenye halmashari mbili linaingia zaidi ya mara mbili jiji la dar es salaam lenye manispaa tatu limeizidi kidogo sana manispaa hii.

Kilichofanyika manispaa iliongezewa maeneo ambayo yalikuwa ni Land bank mashamba ya korosho yaliyotelekezwa hifadhi ya misitu n.k ili ikidhi vigezo vya kuwa manispaa kutoka halmashauri ya mji.

Hivyo pamoja na ukubwa wake wote huu eneo linalotumika ni dogo sana eneo kubwa lililobaki ni pori au mashamba yasiyoendelezwa. Sasa manispaa imeamua kufanya mambo yafuatayo kwanza kutumia sheria za ardhi na mazingira misitu n.k kuanzisha program hii mashamba haya yamepimwa sasa tutaondoa mapori yasiyo na faida na kuanzisha misitu ya miti ya korosho hapo tutakuwa tumehifadhi mazingira lakini tumeendeleza ardhi.

Taratibu za kupata mashamba haya unatakiwa kuandika barua kwa mkurugenzi wa manispaa kuomba shamba kulingana na heka unazoona utawez kuzihudumia pia uelewe kuwa kazi ya kuendeleza mashamba haya inaanza mwezi wa pili mwaka huu hakuna kulala.

Manispaa itakupa shamba itakupatia miche ya korosho bure kwani mpaka sasa miche 1,000,000 imeoteshwa na ipo tayari kwa ajili hiyo. Miche hii itasafirishwa na manispaa mpaka eneo la shamba kazi yako ni kusafisha shamba na kupanda.

Shamba hili litamilikishwa kwako baada ya kuendeleza na kuhudumia.

Unatakiwa uelewe kuwa hawatoi mashamba kwa ajili ya kuhodhi bali kwa ajili ya kilimo katika mashamba.

Manispaa itakuletea umeme na maji shambani na njia baada ya kuendeleza.

Heka moja ya shamba inapatikana kwa tsh 10,000 kwa mzawa wa Lindi na 50,000 nje ya Lindi hakuna dalali wa hii kazi msije kuibiwa bure na fedha hii inalipwa katika akaunt ya deposit ya manispaa

Mkija huku mje na mawazo ya kulima na baada ya hapo ku process korosho viwandani na si kupeleka minadani lengo la manispaa ni kuwa na uchumi mkubwa wa kilimo cha korosho wenye viwanda vyenye kuchakata malighafi za korosho.

Hii ni plan B baada ya serikali kuchukua kodi za majengo minara ardhi sasa manispaa inataka kupata mapato yake kwenye fursa hii.

Ukipanda korosho mwaka 2018 mwezi wa 2 unauhakika wa kuanza kuvuna mwaka 2020.

Msiseme hatujawaambia karibuni kusini kwa maelezo ya ziada njooni inbox.

Kama uki copy acknowledge basi.

Pamoja tunaweza

Korosho Dhahabu ya kijani

Mawasiliano

Mkurugenzi wa manispaa
Halmashauri ya manispaa Lindi
S. L. P 1070
Lindi

Hii fursa bado ipo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yele ya manispaa yaliisha kuna watu walitoa fedha wakarudishiwa baada ya mashamba kuisha. Mimi ni mmoja wapo wa aliyechangamkia hii fursa wakati vijana wenzangu wakiogopa kutapeliwa mimi nilikwenda manispaa physically na nikanunua ekari 100 maeneo ya Chikonji. Tangu February mwaka 2018 ilikuwa ni kazi ya kudondosha msitu mnene kwa kutumia chainsaws kama tatu hivi. Baada ya hapo ikafuatia kukatakata miti na kuikusanya na jua lilipoanza mwezi wa nane,2018 nikaanza kuchoma moto, ninaahukuru sasa hivi shamba ni jeupe na nimeingiza miche 2400 niliyoitengeneza mwenyewe kwenye kitalu. Plan ni kuotesha miche 3500 katika shamba langu lenye ukubwa wa 118 acres. Ninamshukuru Allah kwa kunifikisha hapo nilipofika ingawa nilijua itakuwa ni kazi ndogo ila ni kazi inayohitaji mtaji na kujitoa kweli kweli, ukizubaa wasimamizi wa shamba lazima waibe mafuta, vipuri vya mashine n.k.

Changamoto
1. Maji - mashambani hamna maji hivyo lazima maji ya vibarua na kunyeshea vitalu na miche shambani uyachote kijijini
2. Barabara
3. Uaminifu wa wasimamizi
4. Muda wa usimamizi

Mwisho nawashauri vijana wenzangu kutenda kwa vitendo na sio kwa maneno hapa jf. Tanzania ya viwanda inawezekana!

Kwanza heshima yako mkuu,
Pili hongera kwa ujasiri uliochukua, nami kama kijana kuna la kujifunza hapa.
Binafsi nimechelewa sana kuon ahili bandiko hapa jamvini, kwa sababu ya kutingwa na shughuli za hapa na pale.
Naomba kama fursa itapatikana sehemu nyengine unijulishe, maana mimi mwenyeji wa kusini piaa..
 
Sawa mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado hatujajipanga vzuri kwenye kilimo cha biashara lolote laweza kutokea Leo wakulima wa korosho wanalia kama wahamiaji haramu hali kadharika kwenye mazao mengne imekuwa hivyo ,mahindi watu wanayo mengi sana hawaruhusiwi kuuza watakapo choroko,kunde,mbaazi yote wakulima hawaoni faida ya kilimo cha hayo mazao serikali haijajipanga kwa kilimo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika hili jambo siasa zote zipite zituache tufanye mambo yetu wakija kushtuka tumeshika soko la korosho la ndani unalima unavuna unapeleka kiwandani kuongeza thamani na si mnadani.

Kwa kuanza nimefanya safari SIDO nimekuta kuna mashine za ku process korosho kwa kuanzia na kiwanda cha nyumbani unapata kila kitu kwa 10,500,000/=.

Mmezoea kuona Diamond karanga soon mtakuja kukutana na vitu vyangu ila vitakua vya korosho
Mkuu vipi hizo machine zinaweza kubangua kiasi gani kwa siku ? Ni mda umepita sasa vipi ulifanikiwa?

God save us
 
Yele ya manispaa yaliisha kuna watu walitoa fedha wakarudishiwa baada ya mashamba kuisha. Mimi ni mmoja wapo wa aliyechangamkia hii fursa wakati vijana wenzangu wakiogopa kutapeliwa mimi nilikwenda manispaa physically na nikanunua ekari 100 maeneo ya Chikonji. Tangu February mwaka 2018 ilikuwa ni kazi ya kudondosha msitu mnene kwa kutumia chainsaws kama tatu hivi. Baada ya hapo ikafuatia kukatakata miti na kuikusanya na jua lilipoanza mwezi wa nane,2018 nikaanza kuchoma moto, ninaahukuru sasa hivi shamba ni jeupe na nimeingiza miche 2400 niliyoitengeneza mwenyewe kwenye kitalu. Plan ni kuotesha miche 3500 katika shamba langu lenye ukubwa wa 118 acres. Ninamshukuru Allah kwa kunifikisha hapo nilipofika ingawa nilijua itakuwa ni kazi ndogo ila ni kazi inayohitaji mtaji na kujitoa kweli kweli, ukizubaa wasimamizi wa shamba lazima waibe mafuta, vipuri vya mashine n.k.

Changamoto
1. Maji - mashambani hamna maji hivyo lazima maji ya vibarua na kunyeshea vitalu na miche shambani uyachote kijijini
2. Barabara
3. Uaminifu wa wasimamizi
4. Muda wa usimamizi

Mwisho nawashauri vijana wenzangu kutenda kwa vitendo na sio kwa maneno hapa jf. Tanzania ya viwanda inawezekana!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hili vipi hali ya sasa huko. Naweza kupata kama heka 100?

Nataka kuanza huu mradi.

God save us
 
Back
Top Bottom