Yele ya manispaa yaliisha kuna watu walitoa fedha wakarudishiwa baada ya mashamba kuisha. Mimi ni mmoja wapo wa aliyechangamkia hii fursa wakati vijana wenzangu wakiogopa kutapeliwa mimi nilikwenda manispaa physically na nikanunua ekari 100 maeneo ya Chikonji. Tangu February mwaka 2018 ilikuwa ni kazi ya kudondosha msitu mnene kwa kutumia chainsaws kama tatu hivi. Baada ya hapo ikafuatia kukatakata miti na kuikusanya na jua lilipoanza mwezi wa nane,2018 nikaanza kuchoma moto, ninaahukuru sasa hivi shamba ni jeupe na nimeingiza miche 2400 niliyoitengeneza mwenyewe kwenye kitalu. Plan ni kuotesha miche 3500 katika shamba langu lenye ukubwa wa 118 acres. Ninamshukuru Allah kwa kunifikisha hapo nilipofika ingawa nilijua itakuwa ni kazi ndogo ila ni kazi inayohitaji mtaji na kujitoa kweli kweli, ukizubaa wasimamizi wa shamba lazima waibe mafuta, vipuri vya mashine n.k.
Changamoto
1. Maji - mashambani hamna maji hivyo lazima maji ya vibarua na kunyeshea vitalu na miche shambani uyachote kijijini
2. Barabara
3. Uaminifu wa wasimamizi
4. Muda wa usimamizi
Mwisho nawashauri vijana wenzangu kutenda kwa vitendo na sio kwa maneno hapa jf. Tanzania ya viwanda inawezekana!
Sent using
Jamii Forums mobile app