Fursa ya Kilimo cha Korosho Manispaa ya Lindi

Fursa ya Kilimo cha Korosho Manispaa ya Lindi

Mkuu Negrodemus nimefarijika sana na habari hizi, nimeamua kwa hiyari yangu kumuandikia mkurugenzi wa Lindi barua ya kuomba ekari 3 zakuanzia.
Lakini wasi wasi wangu sio mjuvi sana wa kilimo hiki. Kwa hizi ekari 3 nahitajika kua na mbolea aina zipi na kwa kiwango gani?

Nikipata na gharama itanifaa sana, nataka kuja kuweka kambi kabisa nifungashe Pesa yakutosha.
Njoo inbox
 
Japo nitakuja pm lakini Nafikiri ukiweka hapa itawasaidia wengine pia.
Korosho ni kama mti wakati miti ya kawaida kwa heka moja inaingia 800 na kuendelea korosho yenyewe inakaa miti 20-25 unahitaji samadi kwa matokeo bora ziadi ukipanda utahitaji kusafishia shamba ili kuepusha moto pia kuna dawa za kupulizia kuua wadudu na magonjwa gharama za kuhudumia zinaongezeka ikianza kuzaa napo shamba linajiendesha.

Heka tatu inaingiza miche 75 huwezi shindwa utatamani kuongeza
 
Kwa kawaida heka moja linapandwa mikorosho 20 mpaka 25 kitaalamu ila 25 ndiyo inapendekezwa miche bora ya sasa inachukua miaka 2 mpaka kuanza kuzaa na kadri unavyohudumia miaka inavyoenda ndipo mti unazidi kukua na mazao yanaongezeka.

Uzalishaji wa mti mmoja unategemea pia huduma kusafisha shamba kupiga madawa sulphur booster n.k so kadiri unapo upa huduma nzuri basi na mazao pia yanaongezeka.

Huduma ya mkorosho mwanzoni huku miaka miwili ya mwanzo itakua migumu ndiyo maana unashauriwa kupanda na mazao mengine upate fedha za kuhudumia shamba pia ukipanda mazao mengine unapoyahudumia basi na miti ya mikorosho inapata huduma.

Katika project hii kuhudumia shamba jipya la heka moja haizidi 360,000 gharama zitapungua au kuongezeka kulingana na uamuzi wako labour force n.k.

Ila kama mkorosho umeanza kuzaa kadirio la juu kilo tano kutoka kwenye kila mkorosho inatosha kuhudumia mti mmoja ws korosho mti mmoja unatoa kilo 10 - 30 za mikorosho kulingana na uduma unazolipa shamba lako umri mazao yanaweza ongezeka au kupungua.

Na kwa makadirio heka moja inatoa tani 0.28 mpaka 0.40 inategemea huduma unazoupa mti au shamba na umri wa mikorosho yako inaweza zidi au pungua.

Sokoni kwa kilo moja unaweza pata 1000-4000 inategemea hali ya soko mfano kwa siku hizi sote tumeshuhudia kuwa bei katika minada imefika mpaka 3800-4080 kwa kilo ukitoa gharama hapo za uendeshaji kama ushuru n.k unapata si chini ya 3400-3680.

Soko ni la uhakika coz hapa watu wanapeleka minadani kama watu wakaungana wakatengeneza viwanda tusipeleke mnadani tukapeleka kiwandani basi fedha inaongezeka maana wote tunajua huko mitaani korosho iliyobanguliwa inauzwa vipi kwa kilo moja inafika 30,000.
Umeelezea vizuri mpaka umenitamanisha
 
Mkorosho iliyopo ambayo inawapa wehu wazawa huku ni ya babu zao mpaka sasa ina miaka zaidi ya 50 na bado inatoa products
 
Msubiri fursa kama hii kwenye halmashauri nyingine za Lindi mfano lindi dc kilwa ruangwa nachingwea liwale n.k
 
Korosho ni kama mti wakati miti ya kawaida kwa heka moja inaingia 800 na kuendelea korosho yenyewe inakaa miti 20-25 unahitaji samadi kwa matokeo bora ziadi ukipanda utahitaji kusafishia shamba ili kuepusha moto pia kuna dawa za kupulizia kuua wadudu na magonjwa gharama za kuhudumia zinaongezeka ikianza kuzaa napo shamba linajiendesha.

Heka tatu inaingiza miche 75 huwezi shindwa utatamani kuongeza
Shukran mkuu. Ntakuona pm kwa ufafanuzi zaidi.
 
Msubiri fursa kama hii kwenye halmashauri nyingine za Lindi mfano lindi dc kilwa ruangwa nachingwea liwale n.k
Hivi kiongozi mfano mimi nina shamba langu binafsi si katika hayo ya mgao ma lipo katika hiyohiyo halmashauri ya lindi, nikihitaji hizo huduma nyengine kutoka halmashauri kama vile miche na chochote kingine je naweza pewa?
 
Duh sisi tunaofanya kazi kwenye mikoa mikubwa yenye lami na magorofa tunakosa fursa mwisho wetu mjini utakuwa mbaya..ngoja nijitahidi kuomba uhamisho maana fursa kama hizi nanahitaji uwe karibu
 
Unapata huduma zote bila shida
 
Duh sisi tunaofanya kazi kwenye mikoa mikubwa yenye lami na magorofa tunakosa fursa mwisho wetu mjini utakuwa mbaya..ngoja nijitahidi kuomba uhamisho maana fursa kama hizi nanahitaji uwe karibu
Hata mbali unaweza korosho ni mti supervision inatakiwa kubwa ila ya si kila siku ni wakati wa kusafisha shamba kupiga dawa na kuvuna kipindi kingine unakaa kwako tu umepumzika.

Mhe. Mkapa ana mashamba Nachingwea ye yupo lushoto miaka yote anasimamia vizuri tu.
 
Back
Top Bottom