Fursa ya kuingiza Pweza, Kamba, Ngisi na Dagaa wakavu (uono) Tanzania

Fursa ya kuingiza Pweza, Kamba, Ngisi na Dagaa wakavu (uono) Tanzania

ormystatus

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2019
Posts
262
Reaction score
464
Habari Jamii Forums

PART 1

Ninataarifa A to Z kuhusu biashara ya kuimport Pweza, Kamba, Ngisi na Dagaa wakavu (UONO) Tanzania lakini ninamtaji mdogo sana nahitaji Mtu wa kushirikiana nae.

ZINAKOPATIKANA BIDHAA KWA BEI RAHISI.

Hizo bidhaa zinapatikana kwa bei ya Chini Mozambique 🇲🇿 katika majimbo ya MSIMBWA na PALMA. Haya ni majimbo ambayo yapo karibu kabisa na Mtwara. Utofauti wa bei unaweza kuwa mpaka Mara 3 au zaidi baina ya Mozambique na Tanzania.

NAMNA YA KUKUSANYA.

Pweza, kamba na Ngisi wabichi hukusanywa moja kwa moja kutoka kwenye maboti ya Wavuvi, huoshwa na kugandishwa kwenye mabarafu mpaka pale mzigo wa kutosha utakapopatikana.

Dagaa pia hununuliwa kwa wavuvi, kisha huchemshwa na baada ya hapo huanikwa mpaka watakapokuwa tayari kwa kuuzwa.

USAFIRISHAJI.

Bidhaa zote husafirishwa kupitia bandari ndogo za Mtwara, Ferry au Kilambo (wenyeji wa kusini wanafahamu hizi sehemu).

MASOKO

Soko la moja kwa moja la dagaa wakavu lipo Masasi (Boss ananunua na kulipa cash hapohapo). Pia unaweza kuuza kupitia madalali palepale ferry ya Mtwara.

Soko la Dar la dagaa wakavu naendelea kulifanyia Research.

Soko la Pweza, Kamba na Ngisi ni FERRY DAR ES SALAAM ( soko kuu la Samaki). Nimefika pale na kukutana na wanunuzi wa bidhaa hizi. Niliongea nao kila kitu kuhusu hii biasahara na kubadilishana nao namba za WhatsApp.

Nafatilia Masoko mengine mazuri zaidi.

N.B

Hizo ni taarifa za juu juu tu kuhusu hii biashara.

Taarifa zote kuhusu hii biashara nimekusanya mimi mwenyewe kwa kushirikiana na Mtu wangu wa karibu sana (Mama angu) ambae mpaka sasa anaifanya hii biashara.

Makazi wakati wa kukusanya Mzigo yapo (yameshaandaliwa Misungwi).

Makazi mzigo ukishapokelewa Mtwara yapo pia. (Mimi ni mwenyeji wa huko)

Ukiwa Interested tunaweza kujadili mambo ya ushuru, gharama za Usafirishaji, na wasaidizi mpaka kufika Sokoni.

WhatsApp number 079 531 536 9

AHSANTE.

PART 2

NIMERUDI KUWAPATIA UPDATES ZAIDI.

UNUNUZI AWAMU YA KWANZA

Kama wiki 2 hivi zilizopita tulikusanya mzigo wa pweza wabichi kwa ajili ya wateja wetu wa Dar es Salaam Pamoja na samaki wabichi na wakavu kwa ajili ya wateja wa pale Mtwara. Nilifanikisha kuwasiliana na wateja watatu ambao wote wapo Dar na kunegotiate nao bei. Mteja 1 alifika bei ya 12,000/=, mteja wa pili alifika 11,500/= na mwingine 11,500/= kwa kila kilo 1 ya pweza wenye ukubwa wa kuanzia gram 500.

Tulikuwa na bahati nzuri haswaa kwani bei ilikuwa imepaa kutoka 10,000/= (karibia ongezeko la 1,500 - 2000), lakini kulingana na mtaji wetu tulifanikiwa kukusanya mzigo wa kama kg 317 ndani ya siku 3, tuliongeza idadi ya madip freezer kwa kukodi, tulinunua mabarafu na kutunza pweza wetu.

CHANGAMOTO TULIYOPITIA (YA MUNGU MENGI)

Bhana bhana siku ya nne usiku tulipakiza mzigo kwenye chombo na matarajio ni siku ya tano usiku mzigo ufike (obvious huwa ni safari ya siku moja). Safari ilianza vizuri lakini baada ya masaa machache bahari ilichafuka (upepo ulikuwa mkali sana baharini) hivyo chombo kilikuwa kinatembea kwa masaa ili kuepusha ajali (asubuhi), (Asante kwa naodha wa chombo kwa kutupatia taarifa juu ya changamoto hiyo).

Boss mwenye chombo alifanya juhudi za kupeleka mabarafu kwenye chombo ili mizigo mibichi isiharibike, tunamshukuru kwa hilo pia. Kwa ufupi chombo kilikaa baharini kwa takribani siku tano. Na siku ya sita tuliipata mizigo yetu. Hali ya pweza haikuwa nzuri baada ya kupokea mzigo hivyo Pweza wote tuliwauzia palepale Mtwara na walichukuliwa na mtu mmoja kwa bei Pungufu wakati huohuo tulifanya mawasiliano na Wateja wetu wa Dar kuwajulisha kuhusu changamoto iliyotokea na maamuzi ya kuuza mzigo ferry-Mtwara.

Samaki wabichi na wakavu walifika vizuri na tuliwauza kupitia dalali wetu kwa mnada.

FAIDA NA HASARA

•Pweza tulipata hasara

•Samaki wabichi na wakavu walifuta hasara ya pweza na tulibakiwa na faida kidogo ingawa haikuwa tuliyotegemea kama pweza nao wangefika katika hali nzuri.

NAMNA YA KUTATUA CHANGAMOTO (FUNZO)

•Tumekuja na mbinu mpya ya kukusanya na kusafirisha mizigo kwa kuigawa ( kama ni mzigo wa Kg 400 tutaukusanya kg 200 tunasafirisha, wakati mzigo ukiwa njiani tunakusanya kg 200 zingine na kusafirisha kwa chombo kingine)

•Umuhimu wa kusafirisha mzigo kwa kutumia cool box, faida tutakazozipata kwa sasa tutatenga kiasi na kununua vifaa vya kuhifadhi ubaridi kwa mda mrefu (cool box) ili hata ikitokea dharura ya chombo kukaa mda mrefu baharini kama upepo mkali tusiathirike.

•Kutumia boda ya Kilambo ili kupunguza umbali wa kuvuka kwa bahari, hii njia tutaitumia kipindi cha upepo mkali sana na pale tu mzigo utakapokuwa unatakiwa kwa haraka sana sokoni.

UNUNUZI AWAMU YA PILI

Punde tu baada ya kuuza Mzigo wa awamu ya kwanza tulifanya maamuzi ya kukusanya mzigo wa samaki tupu kwani hatukuhitaji kufanya vitu kwa pressure ukizingatia Muhusika wa kusimamia ukusanyaji wa mzigo (Mama) yupo Mtwara (alirudi Mtwara baada ya kukusanya mzigo wa awamu ya kwanza). Hivo tumekusanya mzigo wa awamu ya pili wa Samaki tupu kupitia dalali (Samaki hawana vipengele vingi). Tumekusanya takribani Kg 200 za samaki ndani ya Siku mbili tu kupitia dalali wetu aliyopo Msimbwa-Mozambique. Mzigo umetoka Msimbwa jana usiku na leo umefika ferry-Mtwara.

HABARI NJEMA

•Nimefanikisha kupata wanunuzi wa samaki pia kwa hapa Dar ambao bei zao zinatofautiana kulingana na aina za samaki. CHANGU bei ya leo ni 11,000/= kwa kg , TASI bei ya leo ni 9,000/= kwa kg, samaki aina nyingine nyingine ni 7,000/=

•Natafuta wanunuzi wengi zaidi nilinganishe bei.

PIA KAMBA KAMBA WANAPATIKANA KWA WINGI KIPINDI HIKI
 
Attachments

  • EAE7E12D-0B4C-4968-AB11-2CD8C159C51B.jpeg
    EAE7E12D-0B4C-4968-AB11-2CD8C159C51B.jpeg
    119.2 KB · Views: 31
  • 760F5BCB-8AD1-4E6D-A77D-BC27CE2AB0D9.jpeg
    760F5BCB-8AD1-4E6D-A77D-BC27CE2AB0D9.jpeg
    128.7 KB · Views: 35
  • 3DD2C8F0-3185-4010-B46F-3F4A08F7A66A.jpeg
    3DD2C8F0-3185-4010-B46F-3F4A08F7A66A.jpeg
    128.7 KB · Views: 31
  • 328047D2-DA1A-4DF1-984F-1DF56C77F5B3.jpeg
    328047D2-DA1A-4DF1-984F-1DF56C77F5B3.jpeg
    134.7 KB · Views: 27
  • 18DD21B7-8BDD-4870-A3EE-21C08F62689E.jpeg
    18DD21B7-8BDD-4870-A3EE-21C08F62689E.jpeg
    126.1 KB · Views: 40
  • E0AB0C04-4069-4FD6-AA1A-36450C24A697.jpeg
    E0AB0C04-4069-4FD6-AA1A-36450C24A697.jpeg
    151.1 KB · Views: 31
  • 8D4E3FC6-2787-4D3D-BD95-FB77543B971E.jpeg
    8D4E3FC6-2787-4D3D-BD95-FB77543B971E.jpeg
    140.7 KB · Views: 24
  • 23E36EBE-C2EC-49BD-A36D-4D6699E58801.jpeg
    23E36EBE-C2EC-49BD-A36D-4D6699E58801.jpeg
    53.3 KB · Views: 31
  • FF7642A1-3CEE-45CA-AE18-46E6B46CEE5D.jpeg
    FF7642A1-3CEE-45CA-AE18-46E6B46CEE5D.jpeg
    189 KB · Views: 33
  • 68483508-3122-423C-AA9C-BF18DDDE327F.jpeg
    68483508-3122-423C-AA9C-BF18DDDE327F.jpeg
    69.9 KB · Views: 32
  • 09956ECB-93D4-4997-8DCF-F3710BFE6F1E.jpeg
    09956ECB-93D4-4997-8DCF-F3710BFE6F1E.jpeg
    44.7 KB · Views: 30
  • C9325972-5AD0-4A88-94DB-E213E4F54DB7.jpeg
    C9325972-5AD0-4A88-94DB-E213E4F54DB7.jpeg
    56.8 KB · Views: 27
  • 564C5F46-1EB5-48A3-B098-44C48EFFBF05.jpeg
    564C5F46-1EB5-48A3-B098-44C48EFFBF05.jpeg
    128.7 KB · Views: 36
Cost analysis! Kuwatoa msumbiji dagaa hao hadi mwanza na kuwatoa tanga kipi bora? Mana hao dagaa kwa hapa Tanzania wanapatikana sana Tanga. Hata Unguja wanatolewa huko
 
Cost analysis! Kuwatoa msumbiji dagaa hao hadi mwanza na kuwatoa tanga kipi bora? Mana hao dagaa kwa hapa Tanzania wanapatikana sana Tanga. Hata Unguja wanatolewa huko
Tanga Munanunuaje? Ambao washachemshwa na kuanikwa au munanunua wabichi na kuwaprocess wenyewe?

Bei ya wabichi ni shilingi ngapi kwa ndoo ndogo ?

Bei ya wakavu ni shilingi ngapi kwa ndoo kubwa?

Nataka nilinganishe na bei za kule.
 
Fanya research ya kutosha mkuu. Mm naishi Unguja na kuna kipind niltaka kufanya hiyo baishara, nikaja kujua hilo kuwa hata sisi kisiwani tunategemea tanga. Hao dagaa wanauzwa sana Kongo. Kuwa na data za kutosha kwa bongo
 
Sawasawa nitajitahidi kukusanya data za kutosha ingawa Mozambique bahari yao ni kubwa tofauti na Tanzania.

Kwahiyo hizo bidhaa zote zinapatikana kwa wingi.

Mfano Pweza kwa kilo wanapatikana kwa 3000 mpaka 3500 mda huu navozungumza.

Nadhani Tanga inawavutia wanunuzi wengi wa dagaa kwa sababu ya Umbali uliopo kutoka Tanga mpaka DRC, urahisi wa kukusanya na usafirishaji mzigo, inaweza kuwa ndo sehemu pekee kwa Tanzania ambayo supply ni kubwa (hakuna option nyingine), Pia huwenda wafanyabiashara hawana nguvu kazi ya kuwawezesha kuchukua mzigo Mozambique au huenda tu hawakuwa na taarifa za kutosha kuhusu Mozambique..
 
3500 kilogram mpaka inafika Dar ushachunguza ni kias gan inaweza kusimamia ili upate faida kama wholeseller?
 
3500 kilogram mpaka inafika Dar ushachunguza ni kias gan inaweza kusimamia ili upate faida kama wholeseller
Ndio, Uzuri kutoka Msimbwa (kisiwani) mpaka Mtwara ni safari ya Masaa tu, haichukui hata siku nzima.

Faida nzuri ipo ndio maana kuna wafanyabiashara wapo Mozambique wanasupply bidhaa Dar.
 
Fanya research ya kutosha mkuu. Mm naishi Unguja na kuna kipind niltaka kufanya hiyo baishara, nikaja kujua hilo kuwa hata sisi kisiwani tunategemea tanga. Hao dagaa wanauzwa sana Kongo. Kuwa na data za kutosha kwa bongo
Mzee tupatupa kila sekta upo?!!
Haya jeshini umetoka lini wewe winga wa viatu na saidia fundi??!! 😹😹😹
 
Mzee tupatupa kila sekta upo?!!
Haya jeshini umetoka lini wewe winga wa viatu na saidia fundi??!! 😹😹😹
Mm kila kona nipo na sasahiv nitaanza majukum mengine ya kazi. Mm mtu wa mapokezi now, na ni profshino artist
IMG-20251214-WA0088.jpg
 
Ndio, Uzuri kutoka Msimbwa (kisiwani) mpaka Mtwara ni safari ya Masaa tu, haichukui hata siku nzima.

Faida nzuri ipo ndio maana kuna wafanyabiashara wapo Mozambique wanasupply bidhaa Dar.
Kuna jamaa yangu humu jf ana supermarekt mtwara na bidhaa anachukua dar. Au unaongelea seafood tu? By the time huhitaj tena kuomba mtu achip in kwenye wazo lako. Jf humu wengi unga mwana we tekeleza mradi mkuu ila dagaa hapo Fatilia na Tanga kwanza
 
Ndio nimejikita kwenye sea foods pekee.

Kwa upande wa bidhaa zingine sina data za kutosha, ingawa Vitenge ni cheap Mozambique kuliko Tanzania kwa sababu bandari yao haina ushuru mkubwa.

Nitajitahidi nifatilie Tanga pia kama wanaweza supply seafoods tofauti tofauti, ili ikitokea dagaa wamepotea, iwe rahisi kuhamia kwenye products zingine kama Kamba na Pweza.
 
Back
Top Bottom