Fursa ya safari ya kibiashara China (kwa wajasiriamali wenye mitaji midogo)

Fursa ya safari ya kibiashara China (kwa wajasiriamali wenye mitaji midogo)

BTW watanzania na hususani wajasiriamali walio wengi wamekuwa makini sana na taarifa za mitandaoni hivyo siyo mburura/ignorant kama mnavyowachukulia baadhi yenu. Utapeli wa biashara za china kwa wafanyabiashara hapo kariakoo umewafundisha wengi sana. Si rahisi mtu awe na zaidi ya 5M kwa Sasa ukamtapeli kirahisi. Waliotoa maoni kuhusu tahadhali za kuchukua kutokana na fursa iliyotolewa na Mshana Jr wamefanya vizuri tena kizalendo lakini hawapaswi kubeza idea yake. Watanzania tumekuwa tukitishana juu ya fursa ndo maana unakuta mtu ana kamtaji kake lakini kutokana na vitisho vya wengi anaambulia ama kughairi au kutochukua uamuzi na kutapanya mtaji wake. Tunachohitaji watu wawe wazalendo kwa nchi na watz wenzao, hata kama coordinator atapata chochote nae siyo mbaya ili mradi amewapa watu exposure nao wakapata pa kuanzia. Kwenda China siyo kama kwenda Kizimkazi, unahitaji watu wenye connection na exposure. Naomba tusimkatishe tamaa mleta idea na wale walionza kuhamasika japo tahadhari ni mhimu kwa Kila fursa.
Kwenda China siyo kama kwenda Kizimkazi, unahitaji watu wenye connection na exposure. Naomba tusimkatishe tamaa mleta idea na wale walionza kuhamasika japo tahadhari ni mhimu kwa Kila fursa.[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa Mshana Jr Mchina karibu atazindua kituo cha biashara hapo Ubungo ambacho kitakuwa kinatoa huduma za exhibition trading platform, cros-border E-commerce platform, commodity procurement platform kwa Made in China goods only

Hata huyo mfanyabiashara wa K/koo badala ya kwenda China anaweza kwenda Ubungo akajionea bidhaa anazopenda then akaenda kwa watu wa procure watakaokuwa na ofisi zao hapo hapo akafanya malipo akaagiza mzigo kutoka China. Ubungo itakuwa ni one stop wholesale center

Hii imekaaje?
Ni fursa pia tupo watanzania milion 60 sidhani kama Wote wataenda hapo ama wataweza masharti na vigezo... BTW kila mtu ana machaguo yake hivyo zote ni fursa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
你好大哥

Yiwu ni tofauti na Guangzhou na ina bidhaa tofauti kidogo na Guangzhou...

Kwa kuwasaidia wafanyabiashara unaowalenga ungeainisha aina ya bidhaa wanazoweza kutana nazo huko ili wajipange...
Kuna semina tutafanya kuna catalogue tutaweka na kuna samples pia na contacts ni project endelevu asante kwa mchango chanya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umesema vizuri

Maana Yiwu, Guangzhou, Guangdong ni masoko 3 makubwa China ambayo yanatofautina urahisi wa kupata aina fulani za bidhaa

Kuna aina za bidhaa ni rahisi kuzipata Guangzhou na Guangdong kuliko Yiwu

Huenda huu mpango ukawafaa baadhi ya wafanyabiashara lakini wengine usiwe hivyo

Guangzhou(city-jiji) ipo ndani ya Guangdong (province-mkoa) iliyopo kusini mwa China...province ya Guangdong ina miji mikuu mitatu ya kibiashara ambayo ni Guangzhou (retail na wholesale), Dongguan (viwanda na wholesale) na Shenzhen (silicon valley)...

Yiwu ni mji upo province ya Zhejiang mashariki mwa China...
 
Tuachane na mambo ya ukada tafadhali.. Ishu za exchange rate ni swala dogo sana sina interest na pesa za wajasiriamali hawa.. Ninacho aim ni kitu kikubwa sana ambacho nitakuwa ukombozi kwa wengi

Ningetaka kupiga hela ningepiga kupitia group za biashara za WhatsApp na Telegram kwa kutoza kiingilio kama wafanyavyo wengine.. Mimi watu wanafanya biashara za mamilion bure kabisa bila kutozwa hata thumni

Hizo group pekee zina watu 1500+ ningetaka faida wala nisingekuja Huku hao pekee wangenitosha

Angalia group hili MOJA pekee lina watu 800+ .. Hakuna kiingilio wala kitoleo.. Ningeamua kuchaji 5000 tu kwa mwezi nisingekosa si chini ya 4M kwa mwezi na kwa mwaka 48M+

Nje na tofauti zetu za kisiasa wote tunashare matatizo na changamoto zinazofanana! Nipo kusaidia sio kutengeneza faidaView attachment 2885001

Sent using Jamii Forums mobile app
Naomba link ya hilo group la telegram......ili isilete usumbufu Naomba unipm
 
Back
Top Bottom