Fursa ya safari ya kibiashara China (kwa wajasiriamali wenye mitaji midogo)

Fursa ya safari ya kibiashara China (kwa wajasiriamali wenye mitaji midogo)

Kutakuwa na safari ya kibiashara kwa wajasiriamali wenye mitaji kidogo nchini China mji wa YI WU mwezi wa tatu mwaka huu wa 2024 tarehe kumi hivi
Safari itakuwa ya pamoja kwa watu wasiopungua 10 na wasiozidi 20.. Faida ya safari hii ya pamoja
.Kupata barua ya mwaliko kwa bei nafuu
. Kupata tickets kwa bei nafuu
. Malazi ya pamoja ya bei nafuu uwapo huko
. Usafiri wa bei nafuu
. Ukalimani
. Mtandao wa maduka ya jumla makubwa na madogo
.Kupata connection mbalimbali za wafanyabiashara na wazalishaji wa China
. Gharama nafuu za chakula, vinywaji matembezi nknk
. Gharama nafuu na za uhakika za kusafirisha mizigo kurudi nchini..

Hii ni fursa mpya na wale watakaoweza kwenda ndio watafungua pazia kwa wengine huko mbeleni
Yale mambo ya kuagiza online ama kumuagiza mtu na kuishia kutapeliwa sasa yanafika mwisho.. Lakini vilevile kununua kitu kwa picha nayo yamafikia ukomo wake

Nitaweka mawasiliano rasmi kwa wale wote walio tayari.. Dirisha la waendaji litafungwa wiki ya pili ya mwezi February siku ya wapendanao

Nyongeza:
Kwa vijana wasio na mishe naweza kuwapa mizigo ya mali kauli kama wakitimiza vigezo na masharti

Sent using Jamii Forums mobile app
mshana hii kitu ni ya uhakika au
basi nami niunge kwenye hiyo list
 
Nimeipenda hii
 
Naongea kutokana na uzoefu hiyo pesa kwa kuanzia inatosha hasa ukiamua kuchukua
Fulana
Sox
Chupi
Urembo
Chaja za simu
Saa
Cover za simu nknk
Hivi ni vitu vinavyouzwa kwa marundo na kwa kilo.. Mfano saa za mkononi saa 10 unauziwa Yuan 10 sawa na Tsh 3000.. Na huo mzigo wote unakuja nao kwenye mabegi yako yasiyozidi 20kg

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante Kwa taarifa
 
Hapa nilipo ndio asubuh nipo mji mmoja hiv uko kaskazin mashariki ya china karibu na Russia ni barafu tupu. Miaka minne nyuma nilijilipua kufanya utafiti kuna tyre flan za Magar nilikuwa naifuatilia utokaji wake bongo ni mkubwa sana. Nimetoka kuweka order kama wiki mbili zilizopita kabla viwanda kufungwa. Ishu hapa ni mpunga. Ili mchina akupe tenda inakulazimu uweke mpunga wa maana Chin kama Bond. Ili wasimpe mwingine uagent in East Africa. Sasa kwasababu hela ni ndefu by then nikawatafuta wabongo tushee hiyo fursa wakatema. Nikaenda lusaka na Lubumbashi kuna washkaji tuliwah kukutana kwenye huu upambanaji mmoja msomali ana duka lusaka na mmoja mkasai nae ana duka Lubumbashi. Tulichokifanya tumefungua kampuni itakayokuwa na makao yake Dar. Ambayo Mimi ndio naisimamia na Agent mkuu zambia ni msomali na Congo ni mkasai na Mimi nawasuplaia. Imekuwa very simpo na tyre kwa mtindo huo inafaida ya kutosha. Sasa haya yote nawaeleza ili mpate kujua faida ya kutembea. We ukipata fursa ya kutoka usiangalie gharama kuna faida lukuki mbelen. Cku ukiotea viela flan unajua pa kuanzia. Ukiwa unafanya kaz na mtu usiangalie yeye anakupiga kias gan we angalia uwepo wake pale unakusogeza kias gan. Mi kwangu ukiwa mfanyakz wangu kama huna emotional za kaz nakufukuza nahtaji mtu ambae sio mwaminifu sana ila mpambanaji Sana. Kila akikaa ili aibe lazima aivushe kampuni.
Duh, hongera aisee
Sasa wenye akili hii ni Wachache sn
Na watakakuelewa hapa Wachache, wengi wanaangalia faida ya pesa kwanza!
Mi Nina roho ngumu😅,nilienda SA (jorbeg) na basi ,ila nilirudi Kwa ndege na nilijifunza vitu kibao ile nataka nianze mishe ndo COVID ikaingia mipaka ilafungwa Kila kitu kikaharibika....😅
Mi kwakweli nikipata nauli na kulala naenda sitakosa kujifunza kitu chochote,bongo exposure Bado sana ..
 
Back
Top Bottom