Slowly
JF-Expert Member
- Jul 7, 2016
- 10,589
- 35,268
Suala au dhana ya kwamba wana wa Mungu ni watoto wa Seth ni assumption ambayo haina back up ya Biblia hata sehemu moja.Dhana hii naifahamu sana na kuna watu wengi wanadhaniahivyo lakini ukweli ni kinyume kabisa kwasababu zifuatazi...
1;Hakuna mahali Mungu aliwakataza wana wa Seth kuoana na wana wa Kaini
2;Hakuna anayeweza kueleza ni kwanini baada ya kuingiliana kwa wana wa Seth na Kaini kingono kukasababisha kuzaliwa viumbe wa ajabu kuliko binadamu
kwasababu Seth na Kaini wote walikuwa ni binadamu wa kawaida kabisa
Kwa upande wangu mimi madai yangu kuwa wana wa MUNGU ni malaika yana back up ya maandiko...
Ayubu 1:6
6 Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda kati yao.
Hao hapo malaika wanaitwa wana wa Mungu.Dhana ya Seth na uzao wake kuwa ni wana wa Mungu ni ya kutunga tu....
Hakuna mahali ambapo biblia inasema kuwa malaika hawana jinsia,andiko uliloleta linasema "hakuna kuoa wala kuolewa kama malaika",kusema hakuna kuoa na kuolewa haimaanishi huna jinsia.Kwa upande mwingine inathibitisha kuwa wana jinsia maana kama wasingekuwa na jinsia wasingetaja kuu ya kutokuwepo kuoa na kuolewa.Mapadri hawaoi,je hawana jinsia kwasababu wamekatazwa kuoa na kuolewa?
Umenifanya nimecheka sana kwa maelezo yako haya.Unatakiwa ujifunze sana juu ya historia ya dunia hii,hapa sizungumzii hiztoria uliyosoma shuleni,nenda zaidi ya hapo...
Usichojua ni kwamba wakazi wa hilo eneo unaloliita wewe kuwa ni mashariki ya kati halikuwa na watu weupe bali weusi na halikuwahi kuitwa "mashariki ya kati" bali lilikuwa linaitwa "North east Africa".Weupe unaowaona eneo hilo walitokea Ulaya na Uturuki na hawakuwa wakazi wa eneo hilo tangu mwanzo na walipofika huko walikuwa wakiwaua sana watu weusi ambao ndiyo walikuwa wakazi halisi wa eneo hili.Historia ya eneo hilo inafanana na ya Misri.Misri haikuwa ya watu weupe bali hao ni watu wa kuja tu..
Songs of songs 1:5
5 I am black, but comely, O ye daughters of Jerusalem, as the tents of Kedar, as the curtains of Solomon.
Nikutakie tafakari njema....
Mkuu hongera kwa utafiti wako ila ninaomba nibishe nadhalia yako ya ulichosema kuhusu wana wa mungu kujitwalia wake kwa wanadam,anachosema mkuu eiyer ndicho nachokijua nakukiamini,baadhi ya biblia wamekazia hayo maneno mwanz:6 sasa ikawa kwamba hesabu ya wanadamu ilipoanza kuongezeka usoni pa nchi nao wakazaa mabinti, ndipo wana wa Mungu wa kweli wakaanza kuwaona mabinti wa wanadamu kwamba ni wenye sura ya kupendeza; nao wakajichukulia wake, yaani wote waliowachagua.so kimsingi namuunga mkono mkuu eiyer ila nae natofautiana nae aliposema malaika walioasi ndio walizaa na wanawake binadamu hapa nimeweka fungu lote sioni walioasi zaidi ni wana wa mungu wa kweli.
Mkuu mimi nimegaiza safari kbs, nilikua na mawazo yanayofanana na yako
Maelezo yanaweza kuonekana marefu but nimeyafupisha kama sitaeleweka sehemu, nijuze...Inaonekana unatumia vitabu fulani fulani alafu unaongezea na Bible... Na matokeo yake ni kuweka vitu visivyo eleweka na kusababisha confusion...still Bible ipo wazi
Wana wa Mungu ni akina nani?
Biblia inasema wote wanaomwamini Bwana wanafanywa kuwa wana wa Mungu “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake” (Yohana 1:12).” Kwa hiyo, tokeni kati yao, mkajitenge nao, asema Bwana. Msiguse cho chote kisicho safi; ndipo nitawakaribisha kwangu. Nami nitakuwa baba kwenu, nanyi mtakuwa vijana wangu na binti zangu, asema Bwana Mwenyezi (2Wakorintho 6:17-18) hivyo tangu enzi na enzi wote walio upande wa Bwana wanaitwa wana wa Mungu. Na wakidumu kuwa hivyo mpaka siku ya kufa kwao, Basi siku ya Mwisho Mungu atawachukua nao wataishi kama Malaika ambao hawaoi wala kuolewa….!!!
Maneno “wana wa Mungu” yanaonekana katika aya tano tu kutoka katika vitabu viwili tu vya Agano la Kale. Aya mbili katika kitabu cha Mwanzo 6 wakati wa mafuriko. Na aya tatu zinapatikana katika kitabu cha Ayubu. Kutoka katika kitabu cha Ayubu, mazingira yanaonyesha wazi kwamba “wana wa Mungu” ni malaika, kwa vile wao kuingia moja kwa moja kwenye uwepo wa Mungu au lugha nyepesi walikuwepo kabla ya uumbaji wa Dunia. Hivyo wana wa Mungu first huwakilisha Malaika and second huwakilisha wanadamu waliokombolewa kwa njia ya ya Yesu kristo pale msalabani,(wale wote waliompokea walifanyika watoto wa Mungu)…na kumbuka damu ya Yesu ilikomboa wanadamu wote waliokuwa na watakaokuwa upande wa Bwana tangu enzi na enzi…hivyo hata akina Habili, Yeremia, Isaya nk… wataokolewa na Damu ya Yesu.
Binti/wana wanadamu ni akina nani?
Kama nilivyodokeza hapo awali wana wa Mungu ni malaika wa mbiguni au wanadamu wanaoshika maagizo ya Bwana..kwa upande wa Binti au wana wanadamu ni wale wasiofuata maagizo ya Mungu bali ya wanadamu ambao kimsingi husukumwa na mawazo ya ibilisi Yesu alisema “Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu.” Mathayo 15:9
Uzao wa Sethi uliwakilisha wana wa Mungu.
Biblia inakri wazi kuwa Uzao wa Sethi ulitii maagizo ya Bwana Mwanzo 4:26..Badala yake Kaini akatoka mbele za Bwana hii inamaanisha aliachana na maagizo ya Bwana pamoja na uzao wake..Mwanzo 4:16…hivyo ndoa kati ya uzao wao ilikuwa ni batili unless kama mmoja kutoka upande wa kaini atafata Maagizo ya Bwana kama ilivyotokea kwa Rahabu (Kahaba), Ruthu (kutoka Moabu), Uria (mhiti) nk…Lakini pia ieleweke kuwa kuna watu wengi wanaomwabudu Mungu huoa wapagani na ndoa zao zikasimama…hii ni sawa na mtu kufanikiwa kwa njia ya wizi au ufisadi inaweza kuwa ni maendeleo lakini mbele za Bwana si sawa...anasema ni heri kutii kuliko kuomba msamaha/dhabihu
Wana wa Mungu hawaruhusiwi kuchangamana na wana/binti za wanadamu katika mahusiano ya ndoa.
Fundisho la Mungu ni the same kwa vizazi vyote, vilivyopita na vilivyopo…Mungu anaposema Msifungiwe nira na wasioamini katika 2Wakorintho 6:14 anamanisha kwa vizazi vyote means hata kizazi cha Nyuma kilikuwa na maagizo hayo hayo…angalia baadhi ya ndoa batili na matokeo yake… Samsoni(Mcha Mungu) na Delila Mfilisti(Mpagani), Mfalme Sulemani (Mcha Mungu) na Wanawake takriban 700 wengi wao kutoka falme mbali mbali za kipagani….Mfalme Ahabu ( muisraeli) na Yezebeli Msidoni(mpagani)…Ndoa hzi zilileta uharibifu mkubwa wa kimaadili na uasi…nan ndo mana Ibrahimu alisisitiza sana Mwanae Isaka apate mwanamke mcha Mungu…even Musa alisisitiza sana waisraeli wasichangamane kwa lengo la ndoa kati yao na wakanaani…
Malaika kuoa na kuolewa/natharia ya ndoa za malaika na wanadamu
Biblia ipo wazi kuwa malaika hawaoi wala kuolewa means hawana jinsia….sasa kama Malaika wana uume na uke wa kazi gani sasa?? Shetani na mashetani/majini wale ni malaika walioanguka(waovu) …uwezo wao haujapunguzwa na maumbile yao yapo vile vile kama wenzao waliopo mbiguni…kilichobadilika ni mindset zao tu…na namna wanavyotake action…watu humchora shetani akiwa na mapembe na umbo baya…hii huonyesha tu uhalisia wa matendo yake…but ni mzuri wa umbo na sura ajabu…!! Au walipofika duniani…waliumbwa upya wakawa na jinsia?? Jibu ni hakuna…kwa sababu changes zozote za kimaumbile anazifanya Mungu…sisi tunaweza modification tu kutoka kwenye kitu ambacho kipo…!!
Utafiti wa kihistoria kuhusu Nadharia ya "malaika waliasi kwa kuvaa miili ya binadamu na kuoa na kuzaa na binti za wanadamu" umegundua chanzo chake ni "Kitabu cha Henoko" ambacho hakitambuliwi kuwa ni "maandiko matakatifu yaliyovuviwa na Mungu"! Na ndo maana Mungu hakuruhusu kiwe sehemu ya biblia tuliyo nayo leo yenye vitabu 66
Kitabu hicho cha Henoko ndicho kimeandika moja kwa moja kikidai: "Malaika wa Mungu mbinguni waliwatazama binti za wanadamu duniani, wakawaona wanavutia kwa tendo la ngono wakaacha enzi yao wakashuka duniani, wakaamua (kuoana) na binti za wanadamu na kisha wazaa nao watoto wa kinefili-wanefili ambao ni majitu."
Kitabu hicho kilisomwa hata na baadhi ya wakristo maarufu wa karne za kwanza walivutwa na taarifa zake baadhi yao wakiwemo akina Tertullian, Irenaeus, Origen, na Clement wa Alexandria. Lakini baadaye Kitabu cha Henoko kilikataliwa kuingizwa kwenye orodha ya maandiko matakatifu ya Agano la Kale. Mojawapo ya sababu ya kukataliwa ni japokuwa kimetajwa kuwa ni kitabu cha Henoko lakini hakikuandikwa na Henoko mwenyewe.
Ukweli ni kuwa hakuna tendo la ndoa ambalo lipo verified kati ya shetani na wanadamu hii haipo…Shetani ndo chanzo cha matatizo duniani na hutamani sana wanadamu waharibikiwe…na kama angekuwa na uwezo wa kuzaa na wanadamu na kuleta viumbe vya ajabu ambavyo totally sio wanadamu halisi angefurahi sana
Nadharia ya majini mahaba kufanya ngono na binadamu
Yesu alitoa mfano halisi ya kwamba pepo mchafu anaweza kuugeuza mwili wa mtu kuwa nyumba yake. Na akitolewa huondoka lakini akikosa mahali pa kukaa huamua kurudi:
“Halafu husema, nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa. Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko kwanza….” (MT.12:44-45)
Kwa maandiko tuliyosoma, tunajifunza yafuatayo: 1. Pepo wachafu wana uwezo wa kuingia katika mwili wa binadamu na kukaa ndani yake. 2. Pepo akiwa ndani ya mwili wa binadamu ana uwezo wa kuathiri akili, hisia na utashi wa binadamu. 3. Pepo mchafu akiwa ndani ya mwili wa binadamu ana uwezo wa kuchochea tamaa za binadamu kufanya vitendo vya ngono kinyume na maadili ya ndoa.
Mambo ambayo yanatafsiriwa isivyo sahihi kuhusiana na pepo wachafu ni kama ifuatavyo: 1. Madai juu ya pepo kujifanyia miili ya kibinadamu ili wapate kufanya ngono na binadamu. 2. Kuna tofauti kati ya kupagawa na pepo akatumia mwili wa binadamu kufanya ngono na binadamu. Lakini pepo mwenyewe hawezi kufanya ngono na binadamu kimwili.
Madai ya kwamba watu wanaolewa au kuoa majini na kuzaa nao sio sahihi. Kinachofanyika kwa wenye madai haya ni “hali ya kupagawa na majini ambayo yamo ndani ya miili yao na kuwasumbua kimawazo na kisaikolojia kuhusu ngono” lakini sio kwamba ni tendo halisi la ngono linalofanyika. Hata wenye kudai kuzaa na majini huwezi kuwaona hao watoto kwa sababu kimsingi huwa ni viini macho na mazingaombwe tu. Na hii ndiyo maana ya Yesu kusema “Shetani ni mwongo na baba wa huo.” (YH.8:44)
Wanefili/Majitu ni akina nani?
Neno la Kiyahudi linalotumiwa Nephilim hutokea katika mistari miwili tu katika Agano la Kale, katika kitabu cha Mwanzo 6 na mengine katika kitabu cha Hesabu 4, Kibiblia watu walijulikana kutokana na jina la ukoo wa baba, Lakini Wanefili hawakuwa katika ukoo wowote ule. katika kitabu cha Hesabu, tunaona kwamba wana wa Anaki ni sehemu ya Wanefili. Tangu awali Anaki alikuwa Mkanaani, kwa mantiki hii ni sahihi kusema Wanefili walikuwa binadamu wa kawaida na si malaika au mapepo.
Maandiko yaeleza machache sana juu ya Wanefili zaidi ya kwamba walikuwa mijitu mirefu sana na yenye nguvu na iliishi katika miji yenye maboma. Je walikuwa Wanefili wa siku hizi baada ya mafuriko au Wanefili katikaMwanzo 6? Kinyume na imani ya waamini wengi kwamba Wanefili hawakutokana na utaratibu wowote wa kibinadamu. Hivyo, Waanaki walikuwa kizazi wa Anaki. Hata hivyo, Wanefili hawakuwa kamwe kama ilivyoelezwa kuwa walishuka kutoka mbinguni, kama neno la Kiebrania “nephal”, ambayo lina maana ya “kuanguka juu” au “kutupwa,” likitokana na tabia yao ya kupenda vita.
Tangu Agano la Kale inaeleza Wanefili walikuwepo kabla na baada ya mafuriko, kama Wanefili walikuwepo ktk kabila au koo flani hii inaleta utata katika koo za watu wa kibiblia ambapo maandiko yanaeleza waziwazi kwamba kulikuwa na watu wanane tu waliookoka katika mafuriko wakati wa Nuhu. Kwa hivyo wale Wanefili baada ya mafuriko wametokana na watu wanane waliokuwepo kwenye safina.
Goliathi alikuwa na sifa za wanefili…je alitokana na ndoa kati ya mashetani na wanadamu jibu ni hakuna…kuwepo na watu wenye nguvu duniani Zaidi ya wanadamu wengine wa kawaida ni jambo liliozoeleka…angalia wachezaji mpira wa Ulaya na hata kutoka West Afrika wana miili mikubwa…angalia wanamziki, wacheza movie, makomando wa kimarekani au wacheza mieleka….ni watu wenye nguvu na wenye sifa pia around the world…wenye majigambo na kupenda vita…je na wenyewe wametokana na ndoa kati ya mashetani na wanadamu? Jibu ni hakuna…kwa nini wako vile? Jibu linajulikana…. watu wenye vidole sita na meno Zaidi ya thelathini na mbili wapo mpaka leo…
Hitimisho
Kwa sababu Biblia inaonyesha wazi kwamba malaika hawaoi wala kuolewa, ni mantiki ya kwamba hawakuwa “wana wa Mungu” waliozaliana na watoto na “binti za watu.” tafsiri bora ni kwamba “wana wa Mungu” walikuwa watu ambao walikuwa katika ukoo wa Sethi, ambaye alimfuata Bwana kwa muda (kwa kulinganisha na ukoo wa Kaini, ambayo walizaliwa “mabinti wa watu”). Hata hivyo, kabla ya mafuriko, “wana wa Mungu” walioa wake katika ukoo wa Kaini, na kwa hiyo, wakaweza kupotoka wenyewe kwa njia ya wake zao wasioamini. Hii ni moja ya sababu kubwa ya Mungu na nia ya kuharibu dunia nzima kwa maji, tu). Kwamba watu wa Mungu wa sethi wanachanganyikana na watu walioamini wa uko wa kaini. (si unajua kaini alilaaniwa na Mungu jaribu kupitia laana zile.)….Jambo hili pia lilitokea kipindi cha Suleman pale alipoamua kuoa wanawake wa kipagani na kujikuta akiangusha ufalme, the same to Samsoni…na hata hvi leo Bwana anasema msifungiwe nira na wasioamini…
Mwanzo 6 pia inawaeleza Wanefili ambao walikuwa wababe ,wenyenguvu na warefu sana, walikuwa watu wa vurugu kutokana na nguvu na ushujaa wao (Mwanzo 6:4). Inasemekana hawa watu walikuwa kizazi cha Kaini, ambao walikuwa wakati wote wakiwaza maovu katika nafsi zao. Wanefili waliokuwepo baada ya mafuriko pia walikuwa waovu wababe na wenye vurugu , lakini hawahusiani na wale walioangamia katika mafuriko, Kwa sababu watu wale wote waliangamia katika maji isipokuwa NUHU na wanawe.
Nadharia ya watu weusi.
Bado nipo kwenye investigation kuhusu hawa watu…..ninaelekea kuamini kuwa watu weusi walitokana na Hamu…Kushi na Misri walitokana na uzao wa Hamu….na kadri sku zilipoendelea wazao wake walijongea Afrika Mfano Misri ipo Afrika na kushi kwa asilimia kubwa wapo Afrika wengi wanadai Ethiopia na Sudani ni uzao wa kushi…na hzi nchi zipo Afrika….Na inasemekana pia Nimrodi aliyejenga mnara wa babeli alikuwa Mweusi(sina uhakika)
Kuhusu rangi ya ngozi….kuna kitu nilikidokeza kwenye post yangu ya awali kuwa Mungu anajaribu kumuliza Yeremia “je mkushi aweza kubadili ngozi yake? Ndo najiuliza hii ngozi ya kushi ni ya namna ipi….na ninapooanisha pia kuwa Sudani na Ethiopia ni sehemu ya kushi..ninaelekea kuamini kuwa Mungu alimaanisha rangi nyeusi… sio kwamba Hamu alizaa watoto weusi…ninavyoamini mimi watu weusi walitokea as time goes…ukichukua jogoo mweupe na kuku jike mweupe wakaishi pamoja sidhani kama watoto wote watakuwa weupe…wawili au watatu wanaweza kuwa na rangi tofauti…hakuna linalomshinda Mungu…
Zaidi ya yote sina comment kuhusu hili jambo……ambacho nakikataa moja kwa moja hapa ni hoja yako ya kuwa mtu wa kwanza alikuwa Mweusi…