Old - Hand
JF-Expert Member
- Apr 9, 2017
- 2,042
- 1,917
Sawa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umepapasa tu kuhusu ukweli wa dunia na anayeiendesha....
Endelea kujifunza na utajua hao Skull and Bones ni sisimizi tu,hata Freemason na Illuminati ni sisimizi tu...
Jifunze kuhusu Pindar utapata mwanga kidogo....
Mkuu,jifunze kuwa mstaarabu. ulikuwa na uwezo wa kuanzisha thread yako na ndo maana kuna watu huwa wanakusema kuwa una tatizo kujiona ni much know. kila mtu ana uwezo wa kuelezea kwa kiwango anachotaka au anachoona kinafaa kulingana na muktadha. si ustaarabu kudhani wewe ndo unajua kila kitu na hii inasababisha sasa wenye akili waone kuwa ni mjivuni.
kama ulikuwa na ya kuongeza haikuwa na ulazima kuja kuandika ulichoandika. unayotaja yote nayafahamu na kama kuyaandika watu wameandika vitabu vyenye kurasa mbalimbali. kuna ambaye ameandika kurasa mia na mwingine ameandika kurasa 1000. but bado hakuna anayesema ulichosema wewe. busara na hekima ni jambo muhimu sana.nliona sehemu kuna watu wameandika kuwa huwezi mfikia hata nusu xxxx. na wenye akili wakaja kukutetea kuwa lengo ni kila mtu kuandika anachokifaham kwa namna anavyotaka na si kushindana sababu mwisho wa siku hizi zoooote ni tafsiri tu hakuna mwenye ukweli halisi au aliyevumbua ukweli.
Mkuu,
Haya yalishaisha siku nyingi sana na niliomba radhi kwa wewe na wale ambao waliielewa text yangu tofauti na nilivyotaka kumaanisha...
Naomba jambo hili liishe mkuu na sikuwa lengo la mashindano na sijawahi kushindana wala kufikiria hivyo hata siku moja,kilichotokea ni watu wachache kutokuelewa kile nilichomaanisha kwenye post hiyo.....
Siwezi kumzuia mtu kuwaza atakavyo mkuu,nipo JF kwa zaidi ya miaka 6 sasa,sijawahi kabisa kushindana na mtu yoyote kwasababu sioni sababu ya kufanya hivyo na nimekuwa naandika mambo mengi sana hapa.Watu wanaoona hivyo ni fikra zao tu au labda ni uoga wao.....
Nashukuru kwa kunielewa mkuu....
Pamoja sana kiongozi.....nashukuru. amani haina haja ya kugombana. sikuwa nmeiona hiyo text. tuendelee kushare uzoefu mbalimbali.karibu sana.
Good story.....View attachment 502158
Tarehe 10 February mwaka 2017 ilikuwa ni siku ya kutimiza miaka 100 tangu kifo cha Geronimo ambaye alikuwa ni shujaa kutoka Jamii ya Apache( hawa ni mashujaa wa wahindi wekundu au wakazi asilia wa Taifa la marekani maarufu kama Red Indians) Ndugu mmoja katika jamii hii alifungua mashtaka akiwashtaki Skull and bones jamii ya Siri ambayo ilianzia chuo kikuu cha Yale huko marekani kuwa iruhusika na kuiba mabaki ya Geronimo. Miaka kadhaa imekuwa ikipigiwa kelele jamii hii ya Fuvu na Mifupa kuwa imeshikilia mabaki ya Geronimo ikiyatumia kwa shughuli zake za kiimani.
Haryln Geronimo mwenye miaka 61 anasema “ naamini kabisa toka moyoni mwangu kuwa roho ya Geronimo haikuachiliwa” akiwaambia waandishi wa habari waliokusanyika wakifuatilia tukio hili lililohusisha jamii hii ya Skull and Bones. huyu ni kitukuu cha Geronimo .
Inasemekana kuwa Wakongwe Kama Prescott S. Bush ambaye ni baba wa Aliyekuwa Rais George W. Bush na Babu wa George W. Bush . huyu na wenzie wengine wanachama wa Skull and Bones walichimba mabaki ya Geronimo toka kaburini mwaka 1918 WAKAIBA FUVU LA HUYU SHUJAA, NA MIFUPA MIWILI na mavazi ya kivita kutoka katika Kaburi lake huko Fort Sill ( Ujue kuwa hizi imani za kuchimba makaburi na kuiba vitu flan zipo hata kwa wazungu si afrika tu ) na jamii hii ikachukua mabaki haya na kuyaweka Makao yao Makuu ambayo yalikuwa yameanzishwa toka mwaka 1832.
View attachment 502159
Conspiracy Mbalimbali Kuhusiana na Skull and Bones
Kuna mambo mengi ambayo yamekuwa yakizungumzwa kuhusiana na kundi au jamii hii. Inasemekana hawa ndio waliohusika na utengenezaji wa bomu la nyuklia mpaka kuuawa kwa J.F. Kennedy. Ni kundi ambalo wengi nchi za huku kwetu hawajalifaham lakini kwa Huko kwa wenzetu ni Kundi kubwa na la kutisha sana. Hili ni Kundi lenye viongozi wakubwa sana duniani likihuishwa na miaka ile lilipokuwepo kundi la mafia.. kuwa hili ni kundi la mafia la kimataifa.
Skull and Bones wamehusika na Ku endesha Utajiri wa Carnegie, Rockefeller na Familia ya Ford na pia kujihusisha na CIA, American Psychological association , Baraza la Mahusiano ya Kimataifa na pia Baadhi ya Makampuni makubwa ya Sheria Kimataifa.
Mwaka 2004 wakat wa uchaguzi wa Urais waliokuwa wagombea wa Republic na Democratic walikuwa ni wanachama wa jamii hii. Ingawa haya hayakusemwa sana maana ilikuwa ni siri. Johnn Kerry alipoulizwa jambo hili alijibu kifupi tu kuwa “ni siri na siwezi zungumzia jambo hilo” na Bush W. naye pia alipata kuzungumzia hili kwa hali ya kutotaka liendelee kuwa gumzo hivyo kwa Kiswahili kingine ni kuwa alilipotezea. Uhusika wa watu katika Jamii hii ni wa siri sana.
View attachment 502161
William Russell alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Yale. Huyu ndiye aliyeanzisha jamii hii ya kishetani yenye nguvu kubwa bada ya kuwa aliwah kukaa Ujeruman akiwa mwanchama wa kundi moja la siri sana duniani likiwepo kundi pia la ILLUMINATI. Rusell alirudi USA akiwa amedhamiria kuanzisha jamii ya siri ya aina yake na akamwambia Alfonso Taft ambaye mtoto wake alikuja kuwa Rais William H. Taft kuwa mmoja ya wanachama wa Kundi hili la Udugu wa Kifo “The Brotherhood of Death” ambalo baadaye ndo likaja kufahamiaka kuwa ni “The order of Skulla and Bones” wanachama walikuwa wakimuabudu Eulogia huyu ni mungu ambaye inasemekana alikuwa na nguvu za kufanya mtu awe na nguvu ya kuongea mbele za watu na kukubalika, kutukuzwa na kuwa mwenye Umiliki wa Dunia.
Fuvu na Mifupa ilianzishwa chuo kikuu cha yale ambacho ni cha Tatu kwa Uzaman Huko Marekani kwa maana ya kuwa ni chuo cha zamani sana katika namba ya vyuo vya zaman usa kinashika namba tatu. Jamii hii imekuwa n ibada zake na mambo mablimbali ambayo yamekuwa ni alama zao I pamoja na nyoka na kutoka sadaka zao kwa mungu wao maybe actually ni shetani ila kwa jina linguine. Wanachama wa kundi hili hupatikana kwa njia ya siri sana na wala huwezi ona matangazo au mtu akijitangaza kuwa yeye ni wmanachama wa kundi hili. Baadaye hupelekwa sehemu ya ibada yao kwa ajili ya kufanyiwa ibada ya kuapishwa kuwa atakuwa mwanachama mwaminifu mpaka kufa.
Wengi wamekuwa wakisikia habari za freemason na illuminati, kundi hili ni kubwa sana na lenye nguvu kubwa sana kiuchumi na kiutawala duniani. Umakini wao umewafanya waendelee kuwa kimya pasipo kujulikana sana kama yalivyo makundi mengine. Na bado limekuwa likihusika sana katika makundi mengine kwa nia ya kujitanua na kujipa nguvu.
Hii dunia tunaishi ila kuna watu wanaiendesha na kupanga matukio mbalimbali. Kuna watu wanaamua nani awe rais na kwa sababu zao wao. Ni mambo machache sana ambayo yanatokea pasipo watu flan kuwa wamepanga yawe.
View attachment 502162
Adi nimestuka.Hapa naona umezidi mkuu, pamoja na watu kukusifu kwa uelewa wako wa haya mambo ila hapa hapana, siamini kabisa
Ichi kitu nimekiona katika movie flan imetoka mwaka huu.... kuna lines mzungu anazisema kwamba kwann blacks wako physical fit, wako accurate na wana speed, wana muono halisi(ingawa hapa sijui alimaanisha nn(true vision)).... so wanachofanya, kuna family ya mtaalamu wa nurology anawabadili memory na kupachika memory ya mzungu..... so yule mbongo anakuwa mzungu...Clone ipo mpaka kwa wasanii wengi wanaovuma wamesha kufa mfano mzuri comedian dave chappele,eminem,dr dre nk wamewareplace na clones.nimekusoma napoleone
Huyu naye ni Skull and bones au?
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15]Nitajitahidi kufupisha kwa namna nitakavyoweza ili nisiandike maandishi mengi japokuwa siyo jambo zuri maana kuna mengine hutayajua...
Bara la Atlantis ni bara lililokuwa kwenye bahari ya atlantic baina ya bara ulaya na Amrerica ya kaskazini.Bara hili lilijulikana kama kitovu cha maendeleo duniani na wakati huo dunia ilikuwa na maendeleo makubwa mara kumi ya sasa.Jambo hili linafichwa sana kwa sababu maalum.Bara hili waliishi magiant [Nephilims] ambao waliendesha utawala duniani utawala ambao ulimuumiza sana binadamu wa kawaida.Kulikuwa kukifanyika kafara za binadamu na viungo vya binadamu vilikuwa vikitumika kwa shughuli mbali mbali za nguvu za giza.Ilifikia mahali damu ya binadamu ilikuwa ikitumika kama kinywaji cha kawaida kwa hawa viumbe..
Unaweza kujiuliza hawa Nephilim ni nani au akina nani.Nephilims ni viumbe ambao walikuwa nusu binadamu na nusu malaika ambao walipatikana baada ya malaika waasi kufanya ngono na wanawake wanadamu.Malaika waasi ndiyo waliowafundishwa wanadamu elimu za unajimu,utoaji wa mimba,kutengeneza silaha na teknolojia nyinginezo ambazo ni za hali ya juu sana.Binadamu baana ya kupata ujuzi huu walianza kuuana wao kwa wao na ndipo Mungu alipoingilia kati na kuleta gharika lililowasambaratisha viumbe wote na kuwasalimisha walioingia kwenye safina...
Maisha ya wakati huu yalikuwa ya kishetani haswa.ni maisha ya kutisha sana maana binadamu alikuwa akiishi kama vile mbuzi leo maana alikuwa akiwindwa vilivyo hadi pale ambapo Mungu alipoamua kuingilia kati.Anayetaka kulirudisha bara hili na ustaarabu ule ni Semjaza,miongoni mwa malaika wakuu walioasi wanataka kuuleta ufalme wao hapa duniani wakishirikiana na binadamu wachache wasiojua ukweli na wanaoujua wachache sana lakini kwa umakini na udanganyifu mkubwa sana wa kisayansi....
Wanataka watawale dunia na jambo hili litatokea siyo miaka mingi kutokea sasa maana wanamalizia tu na wanataka kuwaleta tena hao malaika kutoka walipo kupitia kinachoendelea kule kwenye mitambo yao ya LHC [Large Hadron Collider] kwenye project yao maarufu ya Cern ambapo wanataka kufanya kitu ambacho dunia haitakuja kusahau kamwe...
View attachment 503610 View attachment 503611
LHC
Sananda ni kiumbe wa roho ambaye anajifananisha na Yesu,picha inayotumika kwenye makanisa na ambayo watu wanaamini kuwa ni ya Yesu ni ya Sananda,kuna mengi kumhusu huyu lakini kwa hapa inatosha kusema hivyo.Watu wanadai ni picha ya Cecare Borgia lakini ukweli ni kwamba ni picha ya Sananda.Kiumbe huyu ni miongoni mwa wale malaika waasi na huyu atatumika kudanganya watu wakati watakapo fake ujio wa Yesu.....
View attachment 503607 View attachment 503608 View attachment 503609 View attachment 503609
Sananda...
Sanat Kumara ni Azazel ambaye hujulikana kama Satan Kumara maana jina lake la kwanza limebadilishwa tu herufi.Huyu inasemekana ni Shetani mwenyewe au ni second in command kwenye himaya yao hawa malaika waasi....
Nadhani nimekupa mwanga angalau kidogo....
Mkuu hapo kwenye human Clones umenikumbusha series moja inaitwa Orphan Black.Eiyer,nilikua sjawai kupitia maandiko yako ila leo ume thibitisha mengi,..big up sana,..mi pia nafaham haya mambo ingawa sio level yako,..especialy naunga mkono hapo kwenye true Human beings ambao ndo kiumbe halisi cha Mungu ni kwel ni black race,na hawa wenzetu ni mixer kat ya fallen angels na wanadam.ndo chimbuko la rang nyeupe,..ndomana chuki ya mzungu au mweupe kwa mweus maisha yote ni kubwa,kutufanya slaves etc,lengo ni kuiondoa kabsa ulimwenguni,..pia kwenye hili la underground domes ni kweli,hivi viumbe kwel vipo,na ndo chanzo cha technolojia kubwa kubwa zoote na kuna ulimwengu ambao hatuuoni ila wao wako ahead of time,na ndomana kuna dhana ile ya TIME TRAVEL..n machines etc,ni kwel,hawa viumbe ni IMMORTAL,hawafi,wako kitambo sana na ndo hao wanaandika historia za dunia kwamfano vitab vya din,n wanatengeneza events za kutumiza maandiko hayo,mfano MPANGO WA KUFAKE MWISHO WA DUNIA,watatengeneza mazingira hayo,had malaika had Yesu ambae ata perfom miujiza etc,..kuna kitu kinaitwa HUMAN CLONES,..yan unatengenezwa mtu exactly kama wew mwenyew ila mwenye agenda yao af wew orijino unauwawa,hii ina apply kwa viongoz sana sana,..pia kuna projects ziko kwenye series znafanywa na hawa jamaa,mfano za technolojia,kuandaa viongozi etc, pia mfaham kila kitu kinachohappen ulimwengun hapa kiko kwenye ubao,yan ni planned,kwa ufupi ni haya tuu ila yapo mengi na yakutisha,..kuanzia HIV,HAARP,GAYSM etc..kwenye genetic engeneering ndo kunatisha,watu wanatengeza pests,bacteria,wadudu for specific purposes,nyi mnaona mbu hawaish tuu,..na ngoz nyeus dunian imebak sehem ndogo sana,yan ni kusin mwa jangwa la sahara ndo tumebak,sasa na huu ukimwi wa kupewa,malaria,tb,ebola etc plus njaa na vita vya wenyew,soon lengo lao litatimia
tugusie kidogo jina la hicho chama, mm ni member wa chama fulani lakini sio freemason tunajihusisha na jua na sayariHahahaaa...
Nimecheka sana ila sio mbaya mmejitahidi kuandika na kusimuliana vyema lakini kumbuka uchawi upo tena wa aina nyingi sana duniani ni uchawi wa kila namna unafanyika tofauti ni majina na sehemu tu...!! ila uchawi ni ule ule.
kumbukeni yote kwa yote hizo habari ni watu walikaa wakahisi na kuandika juu ya habari hizo, Freemasonry na illuminati ambao mungu wao anaitwa the baphomet ni vyama ambavyo sio vya siri kwa sababu kila huduma zao na kila kitu chao kipo wazi na vinajulikana, kuna vyama ambavyo ni vya siri la hasha ni siri kweli kweli.
Yote kwa yote sitaeleza mengi kwa sababu hata mimi nilikuwa mfuatiliaji mzuri na nikabahatika kupata wakala ambaye alinifanyia mpango wa kuingia kwenye chama fulani hivi kilicho anzishwa hapa Tanzania na afrika ya mashariki mwaka 1948.
Endeleeni kujifunza mengi zaidi lakini ukweli ni kwamba hamjaweza kufikia hata robo ya ukweli kuhusu mambo yao.
Ukweli ni mpaka mwanachama halisi atakapo amua kuwaambia na yeye pia hawezi kujua vyote ni kwa sababu ya matabaka tofauti ( levels )
Yote kwa yote muwe na siku njema iliyo na amani tele.
Mkuu nipe address I naonekana wewe mwanachama mtiifuHahahaaa...
Nimecheka sana ila sio mbaya mmejitahidi kuandika na kusimuliana vyema lakini kumbuka uchawi upo tena wa aina nyingi sana duniani ni uchawi wa kila namna unafanyika tofauti ni majina na sehemu tu...!! ila uchawi ni ule ule.
kumbukeni yote kwa yote hizo habari ni watu walikaa wakahisi na kuandika juu ya habari hizo, Freemasonry na illuminati ambao mungu wao anaitwa the baphomet ni vyama ambavyo sio vya siri kwa sababu kila huduma zao na kila kitu chao kipo wazi na vinajulikana, kuna vyama ambavyo ni vya siri la hasha ni siri kweli kweli.
Yote kwa yote sitaeleza mengi kwa sababu hata mimi nilikuwa mfuatiliaji mzuri na nikabahatika kupata wakala ambaye alinifanyia mpango wa kuingia kwenye chama fulani hivi kilicho anzishwa hapa Tanzania na afrika ya mashariki mwaka 1948.
Endeleeni kujifunza mengi zaidi lakini ukweli ni kwamba hamjaweza kufikia hata robo ya ukweli kuhusu mambo yao.
Ukweli ni mpaka mwanachama halisi atakapo amua kuwaambia na yeye pia hawezi kujua vyote ni kwa sababu ya matabaka tofauti ( levels )
Yote kwa yote muwe na siku njema iliyo na amani tele.
Makubaliano yangu na chama changu bado hakijafikia muafaka wa kutoa siri. Lakini usijali ninachoweza kukuambia ni kuweka nguvu kubwa wa kutafuta wakala ambaye atakuunganisha na chama upendacho, ni wakala tu na aliye muaminifu. Nakutakia maisha mema.