PreGE2025 G55 Henry Kileo, Moza Ally, Patrick Assenga, Asha Abubakari na Glory Tausi wajiondoa CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Siasa za Tanzania...

CCM kimeo, upinzani nao vilaza basi tafrani...
 
View: https://www.youtube.com/watch?v=7DyNX31-xaQ

View attachment 3333504
Henry John Kilewo, Mwenyekiti wa CHADEMA Kinondoni, atangaza kujivua Uanachama

View attachment 3333505
Henry John Kilewo: Naondoka CHADEMA tukutane kwenye jukwaa lingine, siendi kuanza upya
​

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa kichama wa Kinondoni, Henry Kilewo, ametangaza kujiondoa rasmi ndani ya chama hicho, akitaja kupotea kwa mwelekeo wa kiuongozi na uminywaji wa demokrasia ya ndani kama sababu kuu ya uamuzi wake.

Kilewo, ambaye pia ni mmoja wa waanzilishi wa kundi la G-55 ndani ya chama hicho, amesema hatua hiyo inatokana na kile alichokiita kuvunjika kwa misingi ya maadili ya chama, kukithiri kwa vitendo vya kulipiza visasi dhidi ya wanachama waliotoa maoni ya tofauti, na kukosekana kwa mazingira ya usawa wa kidemokrasia.

“Chama kama kimepoteza mwelekeo wa kiuongozi, kimepoteza mwelekeo wa kutovumiliana kidemokrasia. Haya yalionekana wazi baada ya sisi G-55 kutoa mapendekezo,” amesema Kilewo akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatano mkoani Dar es Salaam.

Ameeleza kuwa badala ya chama kuangalia hoja zilizotolewa kwa nia ya kujenga, viongozi wa juu waliibuka na kampeni za wazi za kuwashambulia na kupanga mikakati ya kuwaondoa wale waliokuwa na mitazamo tofauti, akisema hata Mwenyekiti wa sasa wa chama aliwahi kuenda majukwaani na “kukinanga chama chake mwenyewe”.

Kilewo ameongeza kuwa kinachoendelea sasa ndani ya chama hicho kinaashiria uwezekano wa hali kuzidi kuwa mbaya kwa viongozi waliobaki, akisema: “Kwa kasi hii, ipo siku tutakuta hata Mwenyekiti wa chama amefukuzwa chama. Hii ndiyo hali halisi iliyopo.”

Akieleza kujiondoa kwake CHADEMA, Kilewo amesema: “Nimetafakari sana, na nimekubaliana na nafsi yangu kuwa dhana iliyonivutia kujiunga na CHADEMA haipo tena. Kwa hiyo leo ninatangaza kujiondoa rasmi, na si mwanachama wa CHADEMA tena, wala kiongozi wa chama hicho.”

Hatua hiyo ya Kilewo inakuja siku chache tu baada ya Tawi la CHADEMA Kisutu kumwandikia barua ya wito wa kujieleza, likimtuhumu kwa kuhujumu shughuli halali za chama, usaliti, na kuendesha kampeni za kuwashawishi wanachama kuondoka.

Katika barua hiyo ya Mei 11, 2025, iliyosainiwa na Katibu wa tawi hilo, Anaely Sarakikya, Kilewo alitakiwa kuwasilisha maelezo ya maandishi ndani ya siku 14 juu ya tuhuma zinazomkabili. Barua hiyo inadai kuwa Kilewo amekuwa kinara wa “usambazaji wa mabango ya mikutano ya waandishi wa habari inayoratibiwa kwa nia ovu ya kushawishi wanachama na viongozi wa CHADEMA kuhama chama.”

Kwa sasa bado haijajulikana kama Kilewo atajibu barua hiyo au la, lakini uamuzi wake wa kujiondoa rasmi unaweza kuwa umejibu hoja hiyo kwa vitendo.

=====================

CHADEMA INAONGOZWA KWA UOGA​
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Segerea na Mhasibu wa Kanda ya Pwani, Patrick Assenga, ametangaza kujivua nyadhifa na kujiondoa rasmi ndani ya chama hicho akilalamikia kile alichokiita kukatishwa tamaa kwa watu wanaotoa ushauri na kukandamizwa kwa demokrasia ya ndani ya chama.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam siku ya Jumatano, Assenga amesema hali ndani ya chama imebadilika mno tangu uongozi mpya wa juu ulipoingia madarakani, huku wakosoaji wakibandikwa majina kama “wasaliti”, “waliopokea rushwa” au “waliohongwa”.

“Tumeshangaa, baada ya uongozi mpya kuingia haturuhusiwi tena kuhoji. Ukishauri jambo unaitwa msaliti, unaitwa umehongwa, unaitwa umepewa pesa. Sisi tulianzisha G-55 kwa malengo ya kushauri chama,” amesema Assenga.

Akiwa mmoja wa waanzilishi wa kundi la G-55 ndani ya CHADEMA, Assenga amesema kundi hilo lililenga kuibua hoja za maboresho ya chama, lakini sasa linatazamwa kama tishio.

Assenga pia amewataja kwa majina baadhi ya viongozi wa juu wa CHADEMA, akiwemo Mjumbe wa Kamati Kuu, Godbless Lema, na Makamu Mwenyekiti Bara, John Heche, akidai wamekuwa wakihusishwa na biashara zisizoeleweka huku wakishindwa kujibu hoja za msingi wanazotakiwa kueleza kwa wanachama.

“Lema amesema hawa watu wamepewa milioni mia. Nafikiri amezoea hizi biashara ambazo wao na Makamu wamekuwa wakifanya. Tumeshazungumza mara kadhaa, tumemwambia Mheshimiwa Heche ajitokeze atueleze magari anayomiliki, ameyatoa wapi, na mahusiano yake na baadhi ya mawaziri,” amesema kwa ukali.

Assenga ameongeza kuwa chama sasa kinaendeshwa kwa woga, na kimekosa mwelekeo wa wazi wa kisiasa, akisema hali hiyo imemlazimu kuchukua hatua ya kujiondoa.

“Wamekuwa waoga. Chama kimekosa mwelekeo. Chama hiki hakiwezi kwenda mbele. Najivua uanachama, naachia uhasibu wa Kanda na uenyekiti wangu wa Segerea,” ametangaza rasmi mbele ya wanahabari

Sasa sijui tuite hii ni timu Mbowe au uchaga ndiyo tatizo?
 
Tuliwaambia Chagadema mkabisha

Aya wanaondoka huku mbaki mkijua chama chenu ni chenye sura ya Kidini na Kikabila
Nilijua utasema Chagadema
Nilijua utasema Saccos ya Mh. Mbowe

Au majina haya hayapo tena??
 
CHAMA KIMESHAPASUKA MNANGOJA NINI HUMO ONDOKENI FASTA, HAKUNA CHAMA HAPO NI CHUKI TU NA VISASI.
FB_IMG_17471903337194185.jpg
 
Kinachofurahisha ni wtz tumewapuuza na katika medali slza siasa walikuwa ni watu duni ..... Mchango wao katika mapambano ya hakibna Demokrasia sio sawa na waliopo madarakani!!.
 
Hao ndio wasaliti na watu wenye uchu wa madaraka,chama kinaimba no reform NM o election wenyew wanaimba no election no space for contest
 
Huko field kuna one man show. Heche ni shoka la msitu. Anaendesha mapambano, dhidi ya serekali, ccm na wasaliti. A.k.a njaa 55.
Wacha waende. Bora kuwa kibogoyo kuliko kuwa na meno mengi mabovu.

NoReformNoElection.
 
View: https://www.youtube.com/watch?v=7DyNX31-xaQ

View attachment 3333504
Henry John Kilewo, Mwenyekiti wa CHADEMA Kinondoni, atangaza kujivua Uanachama

View attachment 3333505
Henry John Kilewo: Naondoka CHADEMA tukutane kwenye jukwaa lingine, siendi kuanza upya
​

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa kichama wa Kinondoni, Henry Kilewo, ametangaza kujiondoa rasmi ndani ya chama hicho, akitaja kupotea kwa mwelekeo wa kiuongozi na uminywaji wa demokrasia ya ndani kama sababu kuu ya uamuzi wake.

Kilewo, ambaye pia ni mmoja wa waanzilishi wa kundi la G-55 ndani ya chama hicho, amesema hatua hiyo inatokana na kile alichokiita kuvunjika kwa misingi ya maadili ya chama, kukithiri kwa vitendo vya kulipiza visasi dhidi ya wanachama waliotoa maoni ya tofauti, na kukosekana kwa mazingira ya usawa wa kidemokrasia.

“Chama kama kimepoteza mwelekeo wa kiuongozi, kimepoteza mwelekeo wa kutovumiliana kidemokrasia. Haya yalionekana wazi baada ya sisi G-55 kutoa mapendekezo,” amesema Kilewo akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatano mkoani Dar es Salaam.

Ameeleza kuwa badala ya chama kuangalia hoja zilizotolewa kwa nia ya kujenga, viongozi wa juu waliibuka na kampeni za wazi za kuwashambulia na kupanga mikakati ya kuwaondoa wale waliokuwa na mitazamo tofauti, akisema hata Mwenyekiti wa sasa wa chama aliwahi kuenda majukwaani na “kukinanga chama chake mwenyewe”.

Kilewo ameongeza kuwa kinachoendelea sasa ndani ya chama hicho kinaashiria uwezekano wa hali kuzidi kuwa mbaya kwa viongozi waliobaki, akisema: “Kwa kasi hii, ipo siku tutakuta hata Mwenyekiti wa chama amefukuzwa chama. Hii ndiyo hali halisi iliyopo.”

Akieleza kujiondoa kwake CHADEMA, Kilewo amesema: “Nimetafakari sana, na nimekubaliana na nafsi yangu kuwa dhana iliyonivutia kujiunga na CHADEMA haipo tena. Kwa hiyo leo ninatangaza kujiondoa rasmi, na si mwanachama wa CHADEMA tena, wala kiongozi wa chama hicho.”

Hatua hiyo ya Kilewo inakuja siku chache tu baada ya Tawi la CHADEMA Kisutu kumwandikia barua ya wito wa kujieleza, likimtuhumu kwa kuhujumu shughuli halali za chama, usaliti, na kuendesha kampeni za kuwashawishi wanachama kuondoka.

Katika barua hiyo ya Mei 11, 2025, iliyosainiwa na Katibu wa tawi hilo, Anaely Sarakikya, Kilewo alitakiwa kuwasilisha maelezo ya maandishi ndani ya siku 14 juu ya tuhuma zinazomkabili. Barua hiyo inadai kuwa Kilewo amekuwa kinara wa “usambazaji wa mabango ya mikutano ya waandishi wa habari inayoratibiwa kwa nia ovu ya kushawishi wanachama na viongozi wa CHADEMA kuhama chama.”

Kwa sasa bado haijajulikana kama Kilewo atajibu barua hiyo au la, lakini uamuzi wake wa kujiondoa rasmi unaweza kuwa umejibu hoja hiyo kwa vitendo.

=====================

CHADEMA INAONGOZWA KWA UOGA​
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Segerea na Mhasibu wa Kanda ya Pwani, Patrick Assenga, ametangaza kujivua nyadhifa na kujiondoa rasmi ndani ya chama hicho akilalamikia kile alichokiita kukatishwa tamaa kwa watu wanaotoa ushauri na kukandamizwa kwa demokrasia ya ndani ya chama.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam siku ya Jumatano, Assenga amesema hali ndani ya chama imebadilika mno tangu uongozi mpya wa juu ulipoingia madarakani, huku wakosoaji wakibandikwa majina kama “wasaliti”, “waliopokea rushwa” au “waliohongwa”.

“Tumeshangaa, baada ya uongozi mpya kuingia haturuhusiwi tena kuhoji. Ukishauri jambo unaitwa msaliti, unaitwa umehongwa, unaitwa umepewa pesa. Sisi tulianzisha G-55 kwa malengo ya kushauri chama,” amesema Assenga.

Akiwa mmoja wa waanzilishi wa kundi la G-55 ndani ya CHADEMA, Assenga amesema kundi hilo lililenga kuibua hoja za maboresho ya chama, lakini sasa linatazamwa kama tishio.

Assenga pia amewataja kwa majina baadhi ya viongozi wa juu wa CHADEMA, akiwemo Mjumbe wa Kamati Kuu, Godbless Lema, na Makamu Mwenyekiti Bara, John Heche, akidai wamekuwa wakihusishwa na biashara zisizoeleweka huku wakishindwa kujibu hoja za msingi wanazotakiwa kueleza kwa wanachama.

“Lema amesema hawa watu wamepewa milioni mia. Nafikiri amezoea hizi biashara ambazo wao na Makamu wamekuwa wakifanya. Tumeshazungumza mara kadhaa, tumemwambia Mheshimiwa Heche ajitokeze atueleze magari anayomiliki, ameyatoa wapi, na mahusiano yake na baadhi ya mawaziri,” amesema kwa ukali.

Assenga ameongeza kuwa chama sasa kinaendeshwa kwa woga, na kimekosa mwelekeo wa wazi wa kisiasa, akisema hali hiyo imemlazimu kuchukua hatua ya kujiondoa.

“Wamekuwa waoga. Chama kimekosa mwelekeo. Chama hiki hakiwezi kwenda mbele. Najivua uanachama, naachia uhasibu wa Kanda na uenyekiti wangu wa Segerea,” ametangaza rasmi mbele ya wanahabari

G55 wameshafukuzwa kwani ni lazima afanye press conference? Hawana impact hela za Samia na Mbowe hazina kazi. NO REFORM NO ELECTION.
 
Back
Top Bottom