G7 yapiga marufuku ununuzi wa mafuta Urusi

G7 yapiga marufuku ununuzi wa mafuta Urusi

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Mataifa yenye uchumi mkubwa Duniani yanayounda Kundi la G7 yametoa kauli ya pamoja ya kupiga marufuku au kutonunua mafuta ya Urusi ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa vikwazo kwa taifa hilo lililoivamia Ukraine kijeshi tangu Februari 24, 2022.

Wamechukua maamuzi hayo baada ya mkutano wao wa mtandaoni jana Mei 8, 2022 kwa kuwa wanalenga moja ya chanzo kikubwa cha Urusi kuingiza mapato.

G7 ambayo inajumuisha Nchi a Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan, Uingereza na Marekani imefanya kampeni hiyo ili kummaliza nguvu Rais wa Urusi, Vladimir Putin.

“Hii itakuwa na athari kubwa kwa uchumi wa Rais Vladimir Putin na kumnyima mapato anayoyahitaji kufadhili vita vyake,” inaeleza kauli ya G7 baada ya mkutano kwa njia ya mtandao.

Baada ya mkutano wao huo pia walipata nafasi ya kuzungumza na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky ambapo wlaimjulisha juu ya mipango yao hiyo.

..................................................................................................

Leaders of the Group of Seven have committed to phasing out their countries’ dependency on Russian energy as they announced fresh sanctions as part of an “unprecedented” package of coordinated sanctions to punish Russia over its invasion Ukraine.


After meeting virtually with Ukrainian President Volodymyr Zelenskyy on Sunday, the leaders also pledged to “elevate” a campaign against Russian elites who support President Vladimir Putin.
The latest show of support for Ukraine comes as Russia prepares to celebrate the defeat of Nazi Germany during World War II.

Putin is expected to preside on Monday over a parade in Moscow’s Red Square of troops, tanks, rockets and intercontinental ballistic missiles, making a speech that could offer clues on the future of the two-month old conflict.

Source: Aljazeera
 
Hununui mafuta alafu bado Una nunua gesi kutoka kwake kweli western mwaka huu wamepatikana unanunua ngano, mafuta ya Kula, makaa ya mawe, gesi si angeacha kununua vyote tuone kama wao ni jeurii sana
 
Hununui mafuta alafu bado Una nunua gesi kutoka kwake kweli western mwaka huu wamepatikana unanunua ngano, mafuta ya Kula, makaa ya mawe, gesi si angeacha kununua vyote tuone kama wao ni jeurii sana
Kama urussi ana jeuri angegoma kuwauzia hizo bidhaa nchi za magharibi.

Yani watu wakuwekee vikwazo, washike Mali yako, wamsaidie na silaha adui yako alafu kisha bado unafanya nao biashara.

Hapa urussi kashikishwa ukuta
 
Kama urussi ana jeuri angegoma kuwauzia hizo bidhaa nchi za magharibi. Yani watu wakuwekee vikwazo, washike Mali yako, wamsaidie na silaha adui yako alafu kisha bado unafanya nao biashara. Hapa urussi kashikishwa ukuta
Kama wanaweka vikwazo, Ili tuwaone wako sirious wangeweka na vikwazo vya kuagiza mbolea na Gas kutoka Russia. Lakini hicho wanqchofanya ni unafiki kwa UKRAINE, wapeleke na majeshi yao kabisa wamtoe PUTIN Ukraine wamfuate mpaka Russia wamchakaze Ili asirudie kwa nchi nyingine. Tofauti nahapo wanafanya unafiki wakumkopesha silaha Ukraine Ili OP ikiisha waangalie namna gani watalipwa.
 
Hao waliokataa wanamafuta wametunza wanaweza tumia nusu karne! Sasa jitekenye mwenzangu namimi uone kisokorokwinyo kinavokushuka kihoro..😂
Hawana mafuta hao yakutumia nusu Karne, mafuta wanayo kweli lakini pia Matumizi yao nimakubwa sana kuliko mafuta waliyonayo, ndio maana mafuta hata katika nchi zao yamependa sana.
 
Hununui mafuta alafu bado Una nunua gesi kutoka kwake kweli western mwaka huu wamepatikana unanunua ngano, mafuta ya Kula, makaa ya mawe, gesi si angeacha kununua vyote tuone kama wao ni jeurii sana
Hapa ndipo tatizo lilipo, mtanzania wa kawaida kuona ana akili kuliko viongozi wa mataifa hayo na systems zao zote.
 
Kama urussi ana jeuri angegoma kuwauzia hizo bidhaa nchi za magharibi.

Yani watu wakuwekee vikwazo, washike Mali yako, wamsaidie na silaha adui yako alafu kisha bado unafanya nao biashara.

Hapa urussi kashikishwa ukuta
Sijui watu tatizo ni shule au ni nini, kwani kati ya muuzaji na mnunuzi, anayemhitaji mwenzie zaidi ni nani? Si anayeuza? Tafsir ya kuuza ni kwamba wewe una uhitaji, usipokuwa na uhitaji huwezi kuuza.

Russia ktk hili ndio muathirika zaidi, ni vile tu nchini kwake vyombo vya habari vyote vimezimwa kutoa ripoy negative ktk hii inayoitwa operation.

Hawa vijana wanaojiita mashabiki wa putin wanapaswa kutazama hili sakata kwa mapana.
 
Kesho utasikia
"Hatuwezi kususia mafuta na gas kutoka Russia, ili kulinda uchumi wa ujeruman na watu wake" Chancellor wa ujeruman.

"Japan haiwezi kuachana na mradi wake wa bomba la mafuta kutoka urusi, kwasababu ni mradi wenye masilahi mapana kwa uchumi wa taifa letu"

"USA yaendelea kuagiza mafuta Urusi japo imepunguza asilimia kama njia moja wapo ya kutounga uvamizi wa urusi nchini Ukraine" White house.

Hiyo ndo nguvu ya G7 inayopelekwa mputa mputa na Nguvu ya giant mmoja anaejulikana kama G1 A.k.A jeshi la mtu mmoja.
 
Back
Top Bottom