Gabon: Rais Ali Bongo kuwania Muhula wa 3 licha ya Familia yake kutawala kwa miaka 55

Gabon: Rais Ali Bongo kuwania Muhula wa 3 licha ya Familia yake kutawala kwa miaka 55

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1689048973905.png
Kiongozi huyo aliyeingia Madarakani mwaka 2009 akichukua nafasi ya Baba yake, Omar Bongo aliyetawala kwa zaidi ya miaka 40, atawania nafasi hiyo tena katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti 2023.

Bongo alishutumiwa na Kiongozi wa Upinzani Nchini Gabon, Jean Ping akwa Wizi wa Kura katika Uchaguzi wa mwisho uliofanyika mwaka 2016 ambapo matokeo yalionesha ameziwa Kura 6,000.

Ping alifutiwa 'Passport' yake na kuzuiwa kusafiri nje ya Gabon kwa miaka 5 baada ya kujitangaza kuwa mshindi wa Urais. Hadi sasa Familia ya Bongo imetawala Nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 55.
===========

Gabon's President Ali Bongo Ondimba has announced that he will seek a third term in office in presidential elections planned for August.

The Bongo family has already ruled Gabon for 55 years.

Ali Bongo took over in 2009 from his father Omar Bongo, who had himself been in power for more than 40 years.

The last elections held in 2016 were marred by claims of fraud. Mr Bongo defeated opposition candidate Jean Ping by less than 6,000 votes.

Mr Ping declared himself the winner and contested those results.

His passport was later confiscated and he was only allowed to leave the country this year after a five-year travel ban.

BBC
 
Sawa,kama katiba yao inaruhusu.Mbona Uingereza hawana ukomo wa muda wa kuongoza; kwa mkuu wa nchi (malikia au mfalme) na waziri mkuu ambaye ndiye mtendaji mkuu wa serikali.
 
Hawawezi,as far as kule wanazengo wapo vizuri kimaisha.Ni kama Guinée Équatoriale,wananchi wapo vizuri.So wala hawajali Rais akiongoza mpaka mwisho wa uhai wake.
Hizi nchi bahna nizaidi ya unavyo fikiria maana kila uchao wao ni maajabu tu tawala kwao nikama janga la korona maana tawala zao zinaogopwa wacha, Guinee wao mtawala ni wa maisha?
 
Hizi nchi bahna nizaidi ya unavyo fikiria maana kila uchao wao ni maajabu tu tawala kwao nikama janga la korona maana tawala zao zinaogopwa wacha, Guinee wao mtawala ni wa maisha?
Ndiyo,Hapa ninasemea Guinea Equatorial. Yule babu anayeitwa Theodoro ni raisi tangia 1979 na hana mpango wa kuondoka .Kifo pekee ndo kitamtenganisha na Urais.
 
Ndiyo,Hapa ninasemea Guinea Equatorial. Yule babu anayeitwa Theodoro ni raisi tangia 1979 na hana mpango wa kuondoka .Kifo pekee ndo kitamtenganisha na Urais.
Mayo weeee wapambe watu wabaya sana maana walio pembeni wana mdanganya kwa maslahi yao binafsi, hapo wako tayari hata kuweka sanamu yake ilimradi wanufaike kwa jina lake.
 
Ndiyo,Hapa ninasemea Guinea Equatorial. Yule babu anayeitwa Theodoro ni raisi tangia 1979 na hana mpango wa kuondoka .Kifo pekee ndo kitamtenganisha na Urais.
Theodoro Obiang Nguema ana unafuu sana kuliko kengemaji wengine wa uko West Africa. Alafu tatizo la West huwa mnaweza mtoa Rais aliyepo kwa mbinde mkamuweka mbovu kupitiliza. Kama Ivory Coast walivyomleta Ouattara kwa mbinde na amekuwa wa kawaida sana. Wapinzani na watawala tofauti yao ndogo tu.
 
wanao kula mema ya nchi ndio wanamsapoti awepo hapo walai, anasaidiwa kila kutu huyu jamaa 🤣 🤣
Ni kama Paul Biya wa Cameroon, huyo anaweza kaa 5 star hotel kule Geneva kwa mwezi mzima na timu yake. Anakodi zake floor ya hotel anakaa check up na kutibiwa. Huku nyumbani wapinzani na wanaharakati wanauwawa yeye hata waliouwawa hawajui wala hajui walisema nini dhidi yake.

Ana machawa waliopitiliza, nahisi akitaka kustaafu huwa wanamkataza. Ana watu ambao wanajua akitoka tu wanapotea kwenye mifumo ya serikali. Kama ilivyotokea kwa Angola
 
Hii ni kweli kabisa hawa wanao wazunguka ndio msaada mkubwa sana kwao, hawa jamaa utrazania hawatakufa wala kuoza.
 
Back
Top Bottom