Inawezekana wewe ndiyo umejaa fikra za kidini. Sisi wengine tulikwishajikomboa kwenye hizo fikra za kijinga miaka mingi, ndiyo maana hata familia zetu zina michanganyiko mikubwa ya kiimani. Hatuunganishwi wala kutenganishwa na fikra za kiimani.
Mimi nimeweka iliyokuwa falsafa ya Gadafi iliyokuwa imelalia kwenye fikra duni za kidini. Sijawahi kumchukia Gadafi au mtu yeyote kwa sababu ya imani yake, bali kwa matendo yake.
Hadafi alikuwa katili kwa kila aliyehoji uongozi wake. Ndiyo maana alifuta hata bunge nchini mwake. Aliua kila aliyehoji. Fuatilia historia ya utawala wake. Hata askari aliyemwua alikuwa na chuki binafsi dhidi ya Gadafi kutokana na Gadafi kumkamata ndugu yake pamoja na watu wengine, jumla watu 250, kuwapeleka gerezani, kisha kuwachukua usiku kwa siri, kuwaua na kuwazika kwenye kaburi moja. Askari wote walipewa amri ya kumkamata Gadafi ili ashtakiwe, siyo kumwua. Askari aliyemwua, alipofikishwa mahakamani kwa kosa la kumwua Gadafi, akijitetea alisema kuwa hakuona sababu ya Gadafi kushtakiwa wakati yeye Gadafi aliwaua watu wengine akiwemo kaka yake, bila ya kuwashtaki kwenye mahakama yoyote. Hata alipohukumiwa kunyongwa hadi kufa alisema kuwa alikuwa ameridhika, na anafurahi kwa kuwa amelipiza kisasi kwa Gadafi kwa mauaji aliyoyafanya kwa watu wengine.
Gadafi alionekana mtu mzuri kwa watu wa chini wasioweza kuhoji chochote. Lakini kwa wenye akili wote, alionekana ni dikteta mkubwa. Tena aliweka mfumo wa hovyo wa utawala usioeleza nani anashika madaraka ya nchi kama Rais hayupo, kama wanavyofanya madikteta wote Duniani.