Gadna G Habash kurudi tena kusikika redioni

Gadna G Habash kurudi tena kusikika redioni

Pinokyo Jujuman

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2012
Posts
552
Reaction score
104
Aliyekuwa Mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kupitia Redio Clouds Fm Gadna hivi karibuni anatarajiwa kusikika tena kupitia Redio zetu hapa Tanzania.

Inasemekana kuwa Gadna atarudi kivingine kupitia Times Redio na kurusha kipindi kitakacho fahamika kwa jina la MASKANI na kitarushwa kuanzia Jumatatu saa Kumi jioni hadi saa moja.

My Take: Je suala la kurudi redioni ni ugumu wa maisha mtaani au ni kusema kazi ya utangazaji ndo iko damuni, na vipi tena kuhusu ile kampuni ya maji ya kunywa ya Mamaa Samfudi?
 
Kabla ya kujadili kwa kina tungejua sababu zilizomfanya akaacha kutangaza Clouds, je kulikuwa na ugomvi au la? pia kwanini kipindi kianze saa kumi sawa na kile cha akina Kibonde ambacho yeye alikuwa muasisi wake?
 
Mmh mbona kama anapoteza raman me nilijua majukumu kwenye familia yamekua mengi akaamua kuacha kaz ili aongeze nguvu kwenye hotel yao kumbe nilikua wrong
 
Mguu pande! Mguu sawa! Ruka kichura chura! Mbele tembea.......Njoo hapa......FastaKimbia dukan!

Ohooo ohooo ohooo haya siyo maisha, bora kurudi kijijini kulima!
 
Kama ntakuwa nina kumbukumbu nzuri kipindi anatoka Clouds alisema anaenda kufanya majukumu binafsi wakishirikiana na Mkewe naye ndo msimamizi mkuu so asingeweza kumudu na kazi yake ile ya awali; hata ikasemekana wana mpango wa kuanzisha kampuni yao ya kusambaza maji ya kunywa wakatuletea na Brand name ambayo wengi kupitia mitandao hii ya kijamii hatukulipenda na tuliliponda sana, sasa nalo sijui liliishia wapi tena!!
 
nafkiri tungejua kilichomtoa clouds ni nini tungepata jibu mana kipindi alichotangaza muda ni ule ule na atakachotangaza kuna jambo hapo lazma
 
Ameshatangaza rasmi kuanza kazi Times Fm, atakua akitangaza kipindi kiitwacho MASKANI saa 10 jioni.
Gadna anaungana na wafanyakazi wenzake waliokuwa Clouds FM, Fina Mango, Masoud Kipanya, Tayana, Bandago, George Njogopa
 
Ameshatangaza rasmi kuanza kazi Times Fm, atakua akitangaza kipindi kiitwacho MASKANI saa 10 jioni.
Gadna anaungana na wafanyakazi wenzake waliokuwa Clouds FM, Fina Mango, Masoud Kipanya, Tayna, Bandago, George Njogopa

The rise and fall of clouds FM.
 
Kwani hao Times wana ugomvi na Clouds hadi kuwachukulia wafanyakazi wake kwa kasi ya ajabu hivyo? Halafu huyu Gadna si alisema kuwa anapumzika ili aiimarishe Nyumbani? Kweli duniani wanafiki hawaishi amani! Yaani sikutegemea kabisa kuwa mtu mtaarabu kama Captain angeweza kufanya mambo ya kipwani kama haya.
 
alitaka kwenda kulea mtoto na jide...bt Mimba ya mama si iliharibika...naona kaona itachukua muda kupata kid tena
 
alitaka kwenda kulea mtoto na jide...bt Mimba ya mama si iliharibika...naona kaona itachukua muda kupata kid tena
mambo ya mimba ni majaaliwa ya Mwenyezi Mungu sio suala la kumkashifu mtu, hujafa hujaumbika sidhani kama wana furahia kukosa mtoto ni Mungu tu ndiye mwenye maamuzi kuhusu hilo. Tusimkufuru Mungu jamani
 
Ameshatangaza rasmi kuanza kazi Times Fm, atakua akitangaza kipindi kiitwacho MASKANI saa 10 jioni.
Gadna anaungana na wafanyakazi wenzake waliokuwa Clouds FM, Fina Mango, Masoud Kipanya, Tayna, Bandago, George Njogopa

Hawa akina Kipanya,Fina?Njogopa, Tayna na Bandago wanafanya vipindi gani?
 
Ameshatangaza rasmi kuanza kazi Times Fm, atakua akitangaza kipindi kiitwacho MASKANI saa 10 jioni.
Gadna anaungana na wafanyakazi wenzake waliokuwa Clouds FM, Fina Mango, Masoud Kipanya, Tayna, Bandago, George Njogopa

fina yupo magic mdau,,,,,,
 
Back
Top Bottom