Gadner Habash anapokula pesa za watu wa Jide

Gadner Habash anapokula pesa za watu wa Jide

Tunaomba haki zetu,basi unajua ulitutumia kwenye VIDEO YAKO KWA SIKU MBILI MFULULIZO WENGINE MPAKA kuomba ruhusa kwenye vibarua vyetu ilimradi kuitikia MWITO NA HESHIMA KUBWA,SASA KUSINGEKUWA na malipo basi ingeelezwa mapema,Wababa wa FAMILIA KWENDA KUTUZUNGUSHA KWENYE ile COSTA yako eti kwenda hapa na pale kwa jili ya uchukuaji wa Tv,tena kwa kukoddi nguo kwa gharama zetu leo hii kuwe hakuna kitu ..
USIKU WA MANANE......WEWE!!! hatutaki kusikia sijui Gadnner kala pesaa au nini,lawama ni kwako JIde kwa nini USIHAKIKISHE malipo yetu kwanza? hayo ya sijui nani kafanya nini hayakuwa makubaliano,jumatatu tunataka haki yetu,..
basi wala hatuna mengine,,na mapaka kuja humu ni bada ya maneno mengi mabovu ya baadhi ya watu wako eti tutaanza kufahamika na mengineo...TAFADHALI TUNAOMBA HAKI ZETU JUMATATU NA SISI TUNA FAMILIA.
Hapa mjini kafungueni kesi ya madai muone kama mdaiwa huwa anafungwa.
 
UNAWEZA usiamini lakini ukweli ndo huo...Jide majuzi ya tarehe 5 na 6 aliomba watu WAKE wa karibu kutafuta watu ili wamsaidie kupendezesha VIDEO ya wimbo wake mpya wenye maneno ya kinyago usinitishe.bado haujatoka na kweli jamaa wakafanya juu chini kupiga simu hapa na pale kuwapata watu tena kwa madai kwamba wawe wenye muonekano maridhawa...isitoshe wawe na mashati meupe au suti...jambo ambalo lilitimizwa kwa siku mbili mfululizo.
WE Tonny hujaelewa nini? kifupi ni kwamba bada ya jide kutoa malipo kwa vijana waliomsapoti kuipambisha video ya jide ni mpya ndo kwanza imechukuliwa majuzi na pia kwenye siku ya kuzaliwa jide...yaani aliunganishia vipande vya bethidei na nyimbo mpya,,,hapa imeongelewa story ya huyo mumewe kutogawa zile pesa za wale walioshiriki kwenye VIDEO hujawai ona hata nyimbo kama R.kELLY akishoot video kuna kuwa na watu kama wapambe kupendezesha?au unadhani huwa wanatokea tu?si kwamba wanakuwa wamesetiwa?...sasa hao ndo wanazungushwa mallipo mana kabla waliahodiwa ndo huyo BWANA MKUBWA kala mpaka tena Bi JIDE ajipapae zingine sasa huoni kama huo ni uswahil?
SI KWELI mbona havifanani wala kuingilia kama huamini fuatilia huko bahari beach times fm utajua ukweli....tena kwa kuwaunataka kuyajua mengi yasiyohusu mada..iyo bethdei aliyounganisha kwenye kuchukua iyo VIDEO alichukulia kwenye nyumba ya shoga ake huko huko BAHARI beach aliyafiwa na mume mzungu na kisha kumiliki jumba la kifahari...ndo vipande vya huo wimbo mtauona...sasa haijulikani mr. mzungu alikufa kufaaje mana ...yote yanawezekana,babu mzungu na sista duu!....sasa anaishi kama paradiso...wimbo si mtauona?
amekula pesa zetu unadhani iyo j3 ni kweli labda alitaka kutangazwa bure kama hivi mana mtu mwenye busara hata siku moja huwezi dhurumu wanyonge!mana watalalamika tu,,ni tofauti na mwenye nazo anaweza kupotezea
Ukitaka kutimba kitaa kivingine basi unatakiwa hata staili ya kunyuka pamba nayo iwe kivingine; staili ya kuongea nayo kivingine! Ni hayo tu kwa sasa.
 
Makubwa tena haya , ukisikia kuchanganyikiwa ndio huku, jide Siku izi anakaa jamii forum?? Si mumfuate polis au muende pale nyumbani lounge, kwanza msitusumbue wakat mnaitana kwenye video ulikuja kusema humu? Acheni umbea wenu, njaa tu hata aibu hamuoni kuja kudai elfu mbili umu, mlipokutana mkapeana dili za kuuza nyago mrudi uko uko mkadaiane

Wanadai haki zao cha muhimuwalipwe haraka. Umbea hapo uko wapi? Kwa nini haraka unawaambia waende polisi? kuna njia nyingiza kudai haki hata kuandika humu ni sehemu mojawapo ya kudai haki! Ni kawaida wasanii kutumia watu bure wakati wenyewe wakipta a lot of money hii haikubaliki hata kidogo.
Unamwambia aende polisi wakatiu wa process za pilisai na mahaka zitakavytochulua muda itakuwa sawa na hela wanazodai/ JD jinsi ulivyomstaarabu walipe haki yao pindi utakapopata habari hiii.
 
toa upumbafu hapa..kubwa zima unashindwa kufanya kazi ya maana unakazi ya kukata kata viuno kwenye video

Hata hiyo ni kazi kama JD aliona Video yake itauzika bila kukata viuno kwa nini awasumbue watotoi wa watu? Nadhani wkati umefika wa kuvalue 'time' na vipaji vya watu. Tena wewe huenda ndio mkodoleaji mkubwa wa hivyo viuno.
Msipende tetea hata mahalimtu anadai haki yake kama Tshs elfu 2 ni ndogo kwa nini asiwalipe fasta?????>>
 
umeulizwa unadai kiasi gani? badala ya kutaja amount wewe unajambajamba tu jinga kabisa.

mwanaume yoyote anayekwenda kukata mauno kwenye video hana akili na ni mzigo kwa Taifa
Jumlisha kukodi vazi la suti,tax,na kuzungushwa kwa siku mbili tena usiku,na ni kwa masaa 8.uliza kama unamkodi mtu hata ulaya ipo ila hutegemea na nchi na mapatano....
 
Jaman jide unaitwaa hata hauji huku unadaiwaa hebu lipa watu
 
ukweli gani?kusimamia haki....umeambiwa hapa mahakama? ......yeye si anao mkataba wa kazi walizofanya na Komando, Aende pale sarenda darajan.....hapa anajichelewesha kupata haki yk tu!
We binadamu we ! kwani jamii forums inashughulika na nini?watu wanapoleta taarifa hapa na watu kuzijadlil huwa tunachagua nani ajdiliwe na nani asijadiliwe?hii untouchable mnayotaka kumvika JIDE inatokana na nini? tuache upofu hapa, kweli Jide kipenzi chetu lakini akichefua aambiwe tu!
 
Kama kweli hili limetokea bhasi jide na gadner wamekosea na wana paswa kujirekebisha na kuwapa haki yenu mapema.

Lakini ni wazi katika hili uwezi kwenda popote maana unaonekana hauna mkataba wa hii shughuli na wala hamku andikishana bali yalikuwa makubaliano ya mdomo tuu.

Ni vyema Wasanii na Mameneja wao ifike wakati wawe wana wathamini watu wanao fanikisha kazi zao hasa Maproducer,Mamodo wanao tokea kwenye video zao.Si mara ya kwanza kusikia malalamiko ya namna hii.

Ni vyema watu wakathaminiana na kupeana haki kwa wakati.

Sitaki kuamini wewe Heloo una wasingizia kabisa maana sioni sababu hiyo lakini hebu tueleze
:mlikubalia kiasi gani kama :::malipo?
:mlipewa huduma ya chakula?
:gharama za.kurudi kwenye makazi yenu nani aliingia?

Lakini katika maelezo yako hakuna sehemu ambapo umeonesha kudhurumiwa bali kucheleweshewa haki yako.

Nakushauri ufatilie haki yako japo umefanya haraka sana kulileta jambo hili humu.

Pole.
 
Last edited by a moderator:
inaonekana huyu mleta mada ni mmoja wa wathirika wa hii kitu.
 
ukitaka kutimba kitaa kivingine basi unatakiwa hata staili ya kunyuka pamba nayo iwe kivingine; staili ya kuongea nayo kivingine! Ni hayo tu kwa sasa.

aisee! Ina maana hii habari ilishaletwa humu? Duu pengine ana uchungu sana.

NasDaz lakini naona ana haki ya kupata haki yake japo kafanya haraka kuleta hili swala humu.
 
Last edited by a moderator:
Sielewi kwanini wadau wanakushambulia wakati ki haki ilitakiwa aandamwe JIDE ili ijulikane kama ni kweli au la ,wapi ule uthubutu wa JF kusimamia ukweli?

Kweli kabisa Mkuu nashangaa sana wenye haki ndio kushambuliwa. Ushabiki huu wa JF unanishangaza sana. Wakimpenda mtu/CHama/ Kitu basi hata akifanya ndivyosivyo wanakuwa upande wake tu! Let us be neutral , kama mtu kakosea alelezwe!
 
kweli kabisa mkuu nashangaa sana wenye haki ndio kushambuliwa. Ushabiki huu wa jf unanishangaza sana. Wakimpenda mtu/chama/ kitu basi hata akifanya ndivyosivyo wanakuwa upande wake tu! Let us be neutral , kama mtu kakosea alelezwe!

hakika! Ni kweli inabidi sote tusimamie haki bila kujali ni nani lakini me naona bado mtoa mada hajadhulumiwa kabisa na inabidi afatilie mpaka atakapo ambiwa apewi japo hali ina onesha amezungushwa sana.

Na katika hili kama ni kweli basi ni dosari kwa jide na gadner kufanya mambo kama haya na ni aibu kwa status zao.

Lakini mkuu Heloo haja weka wazi walikubaliana kiasi gani kwenye hii shughuli?

Mkuu Mwana katika hili lets wait ukweli utajulikana na siamini mtoa mada ni kichaa au ana wasingizia.

Watu ni vyema waka jifunza kuwapa haki wenzao kwa wakati maana pesa huwa ina poteza thamani kama hita chelewa.

Naamini jide na gadner hawajapanga kuwanyima haki yao kama kulikuwa na makubaliano lakini katika hili inabidi wajirekebishe.
 
Last edited by a moderator:
Kweli kabisa Mkuu nashangaa sana wenye haki ndio kushambuliwa. Ushabiki huu wa JF unanishangaza sana. Wakimpenda mtu/CHama/ Kitu basi hata akifanya ndivyosivyo wanakuwa upande wake tu! Let us be neutral , kama mtu kakosea alelezwe!

kweli kabisa mkuu, jf watu wakimpenda mtu/chama uwa wanafumbia macho mabaya yake na kujifanya hawayaoni.. kama kweli gadner kafanya hivi, atakuwa anamwangusha mkewe :....
 
ULICHOSEMA NI KWELI unajua ingekuwa free sidhani kama kungekuwa na haja ya kulalama,ila kulikuwa na mapatano tena kwa kusema hata izo nguo kama suti na mashati meupe tulijigharamia kwa mapatano kwamba hata kama mtu ni nguo zako ama ulikodi basi yatalipwa pamoja na huo muda...usiku kwa usiku,,na wengi wetu tuliingia hata gharama za tax kurudi nyumbani mana gari la jide liliishia nyumbani lounge,kwani hata gari la jide hulala pale nyumbani lounge dereva wake anaitwa SAID....POA TU DUNIA INA MAJARIBU NDO HAYA!

Mna risiti za kukodisha hizo nguo au mnaropoka tu bila kujua nini mnataka ww mtu awaambie kama kuna gharama atalipa halafu unakuja na maneno bila stakabadhi ni wizi ru
 
Kutoka kuwa mkata majani/mlinzi TBL Mwanza,,muuza kanda FM pale Mwanza hadi alipo lazima asahau alikotoka
 
Back
Top Bottom