TAJIRI MKUU WA MATAJIRI
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 11,999
- 24,328
Rubani ambaye pia ni raia wa Oman aliyetaka kuiangusha Ndege ya Flydubai iliyobeba abiria wengi wao wakiwa raia wa Israel ameelezwa kuwa ni mtu wa dini sana (religious extremist). Kwamba anaswali sana na mara kwa mara kila siku na hataki kushikana mikono na wanawake ikiwa ni ishara ya kuwa ni mtu aliyeshiba dini.
Rubani mwenzake ameiambia Channel 16 ya Israel kuwa rubani huyo alijiunga na Flydubai miezi 8 iliyopita. Wakati Ndege hiyo ikiruka toka Dubai kwenda Israel jana na ikiwa angai, rubani huyo alimchoma rubani kiongozi na akaanza kuiangusha Ndege. Rubani kiongozi alifanikiwa kufungua mlango wa chumba cha kuongozea Ndege kabla hajazimia akapiga kelele kuomba msaada. Abiria walifanikiwa kumdhibiti rubani aliyegeuka gaidi na wakaiongoza Ndege kutua salama kwa dharura nchini Saudi Arabia.
Soma Pia: Jaribio la kigaidi: Rubani kumchoma kisu rubani mwenzie na kulazimisha ndege kubadili njia
Ndege hiyo ilibeba abiria 174 ambapo karibu wote wakiwa raia wa Israel. Mtu aliyeiokoa hiyo Ndege isianguke ni raia wa Israel aliyeelezwa kuwa fundi bomba wakati rubani aliyechomwa kisu ni raia wa India.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?