"Gaidi" wa jana anaweza kuwa shujaa wa leo? Historia ya Israel ambayo wengi hawaijui

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Posts
24,661
Reaction score
40,890
Kila mara tunaposikia kuhusu Mashariki ya Kati, jina la Hamas huibuka haraka na mara nyingi hufuatwa na neno ugaidi. Lakini historia ina ukurasa ambao watu wengi hawaujui au hawapendi kuuzungumzia.

Kabla ya Israel kuzaliwa mwaka 1948, harakati za Kizayuni nazo zilikuwa na makundi ya "kigaidi" yaliyotumia mabomu, mashambulizi ya silaha na mauaji ya kisiasa ili kufanikisha lengo la kuanzisha taifa la Wayahudi.

Kundi kubwa zaidi lilikuwa Haganah, lililoanzishwa tarehe 12 Juni 1920. Mwanzoni lilijieleza kama jeshi la kujilinda kwa walowezi wa Kiyahudi waliokuwa Palestina. Kadri miaka ilivyopita, Haganah lilikua na kuwa jeshi kamili lenye maelfu ya wapiganaji, mtandao wa ujasusi, mafunzo ya kijeshi na usambazaji wa silaha. Baadaye likaongozwa kisiasa na David Ben-Gurion, ambaye ndiye aliyekuja kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Israel.

Lakini si kila mtu ndani ya Haganah aliamini kwamba kujilinda pekee kungetosha. Baadhi ya wanachama waliona Waingereza walipaswa kulazimishwa kuondoka kwa nguvu. Ndipo walipojitenga na kuunda makundi yenye msimamo mkali zaidi.

Miongoni mwa makundi hayo, moja lililoacha alama kubwa zaidi ni IRGUN (Etzel).
images.jpeg

Menachem Begin.
Kuanzia mwaka 1943, Irgun liliongozwa na Menachem Begin. Chini ya uongozi wake, kundi hilo liliamini kwamba mabomu, mashambulizi ya kijeshi na operesheni za kushitukiza ndizo zingeharakisha mwisho wa utawala wa Waingereza katika Palestina.

Na kweli wakaanza kufanya hivyo.

Mnamo 22 Februari 1946, Irgun lilivamia vituo vitano vya Jeshi la Anga la Uingereza (RAF) na kuharibu ndege 14 za kijeshi.

Miezi michache baadaye, tarehe 22 Julai 1946, kulitokea tukio ambalo mpaka leo linafundishwa kwenye vitabu vya historia. Wanachama wa Irgun waliingiza mabomu yaliyofichwa kwenye makopo ya maziwa ndani ya Hoteli ya King David mjini Jerusalem, iliyokuwa makao makuu ya utawala wa Waingereza.

Mlipuko huo uliua watu 91; Waingereza, Waarabu na Wayahudi na kujeruhi wengine wengi. Hadi leo, tukio hilo bado linabaki kuwa moja ya mashambulizi maarufu zaidi katika historia ya eneo hilo.

King_David_Hotel_bombing,_Jerusalem_1946.jpg

Lakini huo haukuwa mwisho.

Tarehe 1 Machi 1947, Irgun lililipua Klabu ya Maafisa wa Waingereza ya Goldschmidt na kuua maafisa 17 wa Uingereza.

Mnamo 29 Septemba 1947, lililipua makao makuu ya polisi mjini Haifa kwa kutumia pipa lililokuwa na karibu tani moja ya vilipuzi. Watu 10 walikufa na zaidi ya 50 walijeruhiwa.

Mapambano yao hayakuishia Palestina pekee.

Tarehe 31 Oktoba 1946, bomu lililipuka katika Ubalozi wa Uingereza mjini Rome, Italia. Mwaka uliofuata, mabomu mengine yalilipuka katika Hoteli ya Sacher, Vienna, iliyokuwa ikitumiwa na Jeshi la Uingereza nchini Austria. Pia kulikuwa na mashambulizi dhidi ya reli na treni zilizokuwa zikitumiwa na Waingereza, ikiwemo reli iliyounganisha Cairo na Haifa.

Kutokana na mlolongo huo wa mashambulizi, mwaka 1946 mamlaka za Uingereza, zikiwemo MI5 na Bunge la Uingereza, zililitaja rasmi Irgun kama kundi la kigaidi. Umoja wa Mataifa pia ulikitambua kama kikundi cha kigaidi hasa baada ya ushiriki wao kwenye kifo cha Folke Bernadotte ambaye tutamuongelea zaidi kwenye makala ijayo.

Lakini historia ilikuja kubadilika kwa kasi.

Israel ilipopata uhuru mwaka 1948, David Ben-Gurion alitangaza kuwa makundi yote ya kijeshi yaliyokuwa yakifanya kazi nje ya serikali yavunjwe na wapiganaji wake waingizwe katika jeshi jipya la taifa, Israel Defense Forces (IDF).

Lakini si kila mtu alikubaliana na uamuzi huo.
1948_Arab-Israeli_War_(997008136847205171).jpg

Meli ya Altalena baada ya kushambuliwa na kombora la IDF.

Irgun lilikuwa limeagiza meli iliyoitwa Altalena kutoka Ulaya ikiwa imebeba silaha nyingi. Serikali mpya ya Israel iliona kuwa kundi hilo halikupaswa kuwa na jeshi lake wala silaha zake, kwa sababu hilo lingeweza kuhatarisha mamlaka ya dola mpya.

Mvutano huo uligeuka mapigano. IDF ilishambulia meli hiyo na zaidi ya watu 16 walifariki. Na mapigano yakaendelea katika fukwe hizo na kusababisha askari watatu wa IDF kuuwawa. Wakati huo, Menachem Begin aliwaamuru wafuasi wake wasijibu mashambulizi kwa nguvu zaidi ili kuepusha vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya Wayahudi.

Na hapa ndipo historia inapogeuka kwa namna ambayo wengi hawaitegemei.

Mtu ambaye aliwahi kuongoza kundi lililotajwa kuwa la kigaidi baadaye aliingia kwenye siasa. Mwaka 1973, Menachem Begin alishiriki kuijenga nguvu ya chama cha Likud. Mwaka 1977 akashinda uchaguzi mkuu na kuwa Waziri Mkuu wa Israel.

Mwaka uliofuata, 1978, Begin alipewa Tuzo ya Nobel ya Amani baada ya kusaini Camp David Accords na Rais wa Misri Anwar Sadat; makubaliano yaliyomaliza rasmi hali ya vita kati ya Israel na Misri.

Historia ina tabia ya kutukumbusha jambo moja muhimu: mara nyingi, mtu anayeitwa "gaidi" na upande mmoja wa historia anaweza kuja kuonekana kama "shujaa wa taifa" na upande mwingine.

Hii haimaanishi kwamba mauaji ya raia yanapaswa kuhalalishwa, wala haimaanishi kwamba makundi yote yanafanana. Badala yake, inatukumbusha umuhimu wa kuisoma historia yote, si ukurasa mmoja tu unaotufaa.
 
View attachment 3622586
Menachem Begin.
Kuanzia mwaka 1943, Irgun liliongozwa na Menachem Begin. Chini ya uongozi wake, kundi hilo liliamini kwamba mabomu, mashambulizi ya kijeshi na operesheni za kushitukiza ndizo zingeharakisha mwisho wa utawala wa Waingereza katika Palestina.

Na kweli wakaanza kufanya hivyo.

Mnamo 22 Februari 1946, Irgun lilivamia vituo vitano vya Jeshi la Anga la Uingereza (RAF) na kuharibu ndege 14 za kijeshi.

Miezi michache baadaye, tarehe 22 Julai 1946, kulitokea tukio ambalo mpaka leo linafundishwa kwenye vitabu vya historia. Wanachama wa Irgun waliingiza mabomu yaliyofichwa kwenye makopo ya maziwa ndani ya Hoteli ya King David mjini Jerusalem, iliyokuwa makao makuu ya utawala wa Waingereza.

Mlipuko huo uliua watu 91; Waingereza, Waarabu na Wayahudi na kujeruhi wengine wengi. Hadi leo, tukio hilo bado linabaki kuwa moja ya mashambulizi maarufu zaidi katika historia ya eneo hilo.

View attachment 3622589

View attachment 3622583

Asante Sana kwa makala.

Hata Yitzhak Shamir aliyekuwa Waziri mkuu wa Israel aliyehudumu kwa muda mrefu hasa enzi za Intifada ya kwanza ya Wapalestina (1983-1984 na 1986-1992) alikuwa kiongozi wa kundi la kigaidi la Lehi au Stern gang.

Shamir ni mmoja wa wahusika wakuu wa mauaji ya mpatanishi wa kwanza wa mzozo wa Mashariki ya Kati aliyeteuliwa na UNO ( Count Folke Bernadotte) ambaye aliuliwa na magaidi wa Lehi 17, Septemba 1948.
 
Hii dhana ya ugaidi ipo biased sana ukizingatia watu fulani wakifanya hayo inaonekana ni ujasusi mzuri na ukombozi ila wakifanya wengine wanaonekana ni wadini na wauaji.
 
Hawa magaidi wa kizayuni kina Begin, Shamir walikuja kuwa Mawaziri wakuu wa Israel tena huyu Begin mpaka tuzo ya amani ya Nobel alipewa baada ya mkataba wa amani kati ya Israel na Misri.

Huyu Alshara Rais wa Syria wakati akiitwa Al Jolani kiongozi wa Alnusra/HTS aliitwa gaidi na wamagharibi tena alikuwepo kwenye 'hit list' ya FBI na CIA, ila kwa Sasa ni mshirika wa Marekani japo Israel inampinga.

Hili neno 'gaidi' ni kama vazi tu muda wowote unaweza kuvishwa na baadae kuvuliwa ni kama Mbowe na kesi ya ugaidi alitoka Mahabusu na kupelekwa Ikulu muda huo huo.
 
Ni sahihi hata Mandela alitambuliwa kama gaidi na US na baadae akatolewa..

Ila wayahudi wengi hadi leo wanafanya ugaidi..
 
Hii dhana ya ugaidi ipo biased sana ukizingatia watu fulani wakifanya hayo inaonekana ni ujasusi mzuri na ukombozi ila wakifanya wengine wanaonekana ni wadini na wauaji.
Israel wanafanya ugaidi kila siku, ila wanalindwa, lakini Hamas wakijitetea dhidi ya ugaidi wanaofanyiwa wao huitwa magaidi.

Hata hivyo kwa haya yaliyotokea hivi katibuni ni kama Israel imeanza kuchokwa hata na wale walikuwa wakiilinda..

Kwa US waue hio AIPAC ni kundi la pro Israel ambao wanahonga wagombea ubunge ili wakishinda uchaguzi wawatumie kwenye agenda zao kwa manufaa ya Israel..

Wananchi wengi sasa hawaitaki AIPAC na kuna baadhi ya wanasiasa wameanza kukataa ufadhili kutoka AIPAC..

Israel pasipo kubebwa na US pale middle east hawana chao, na hio kazi inafanywa na AIPAC..

Ingawa Israel ina vyombo vingine vya diplomasia, hakuna chombo cha ndani ya Marekani chenye nguvu, mtandao, na uwezo wa kifedha wa kulinda maslahi ya Israel kama AIPAC.

AIPAC ikifa Israel ndipo imefikia mwisho...
 
Kizazi cha Sasa huko Marekani na hata Ulaya magharibi wanahoji sana kuhusu hii jinai ya Israel na namna Kodi zao zinavyotumika kufadhili hilo.

Ni kweli Israel imechokwa na hata wao wanakiri hii serikali ya mrengo mkali wa kulia ya Netanyau imesababisha nchi yao kuchafuka kimataifa.

Tatizo ni kwamba mrengo wa kushoto wenye kuunga mkono 'mataifa mawili' hawana nguvu na ushawishi kama wale wahafidhina wanaohubiri chuki dhidi ya Wapalestina.

Suluhisho ni Marekani na Ulaya magharibi siku waipige vikwazo hapo ujanja hawana.
 
Kabisa...

Na hili shirika ndio moja ya mashirika yanasababisha US ionekane inaendeshwa na Israel..

Ndio maana pro Israel watakuambia US si chochote kwa Israel..

Lakini ni kizazi kipya US na EU hawataki ujinga, na Netanyahu mwenyewe amezungumza kuhusu kujiondoa kabisa na misaada kutoka US kwa miaka 10 ijayo...

Hii naona ni kwa sababu Israel inakuwa haina uhuru wa kufanya maamuzi hasa katika kipindi hiki kuna mgogoro na Iran, Israel inapangiwa masharti na kufuata.

Kingine naona ni kejeli wanazopata kila siku kutoka kwa wananchi wa US na viongozi wao kuhusu msaada wanaopewa unaotokana na kodi zao...

Lakini natabiri, Israel watakuja kuingia kwenye mgogoro na US wakipata uwezo kamili wa kujitegemea , maana jamaa huwa hawana shukurani...
 
Kila mara tunaposikia kuhusu Mashariki ya Kati, jina la Hamas huibuka haraka na mara nyingi hufuatwa na neno ugaidi. Lakini historia ina ukurasa ambao watu wengi hawaujui au hawapendi kuuzungumzia.

Kabla ya Israel kuzaliwa mwaka 1948, harakati za Kizayuni nazo zilikuwa na makundi ya "kigaidi" yaliyotumia mabomu, mashambulizi ya silaha na mauaji ya kisiasa ili kufanikisha lengo la kuanzisha taifa la Wayahudi.

Kundi kubwa zaidi lilikuwa Haganah, lililoanzishwa tarehe 12 Juni 1920. Mwanzoni lilijieleza kama jeshi la kujilinda kwa walowezi wa Kiyahudi waliokuwa Palestina. Kadri miaka ilivyopita, Haganah lilikua na kuwa jeshi kamili lenye maelfu ya wapiganaji, mtandao wa ujasusi, mafunzo ya kijeshi na usambazaji wa silaha. Baadaye likaongozwa kisiasa na David Ben-Gurion, ambaye ndiye aliyekuja kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Israel.

Lakini si kila mtu ndani ya Haganah aliamini kwamba kujilinda pekee kungetosha. Baadhi ya wanachama waliona Waingereza walipaswa kulazimishwa kuondoka kwa nguvu. Ndipo walipojitenga na kuunda makundi yenye msimamo mkali zaidi.

Miongoni mwa makundi hayo, moja lililoacha alama kubwa zaidi ni IRGUN (Etzel).
View attachment 3622586
Menachem Begin.
Kuanzia mwaka 1943, Irgun liliongozwa na Menachem Begin. Chini ya uongozi wake, kundi hilo liliamini kwamba mabomu, mashambulizi ya kijeshi na operesheni za kushitukiza ndizo zingeharakisha mwisho wa utawala wa Waingereza katika Palestina.

Na kweli wakaanza kufanya hivyo.

Mnamo 22 Februari 1946, Irgun lilivamia vituo vitano vya Jeshi la Anga la Uingereza (RAF) na kuharibu ndege 14 za kijeshi.

Miezi michache baadaye, tarehe 22 Julai 1946, kulitokea tukio ambalo mpaka leo linafundishwa kwenye vitabu vya historia. Wanachama wa Irgun waliingiza mabomu yaliyofichwa kwenye makopo ya maziwa ndani ya Hoteli ya King David mjini Jerusalem, iliyokuwa makao makuu ya utawala wa Waingereza.

Mlipuko huo uliua watu 91; Waingereza, Waarabu na Wayahudi na kujeruhi wengine wengi. Hadi leo, tukio hilo bado linabaki kuwa moja ya mashambulizi maarufu zaidi katika historia ya eneo hilo.

View attachment 3622589
Lakini huo haukuwa mwisho.

Tarehe 1 Machi 1947, Irgun lililipua Klabu ya Maafisa wa Waingereza ya Goldschmidt na kuua maafisa 17 wa Uingereza.

Mnamo 29 Septemba 1947, lililipua makao makuu ya polisi mjini Haifa kwa kutumia pipa lililokuwa na karibu tani moja ya vilipuzi. Watu 10 walikufa na zaidi ya 50 walijeruhiwa.

Mapambano yao hayakuishia Palestina pekee.

Tarehe 31 Oktoba 1946, bomu lililipuka katika Ubalozi wa Uingereza mjini Rome, Italia. Mwaka uliofuata, mabomu mengine yalilipuka katika Hoteli ya Sacher, Vienna, iliyokuwa ikitumiwa na Jeshi la Uingereza nchini Austria. Pia kulikuwa na mashambulizi dhidi ya reli na treni zilizokuwa zikitumiwa na Waingereza, ikiwemo reli iliyounganisha Cairo na Haifa.

Kutokana na mlolongo huo wa mashambulizi, mwaka 1946 mamlaka za Uingereza, zikiwemo MI5 na Bunge la Uingereza, zililitaja rasmi Irgun kama kundi la kigaidi. Umoja wa Mataifa pia ulikitambua kama kikundi cha kigaidi hasa baada ya ushiriki wao kwenye kifo cha Folke Bernadotte ambaye tutamuongelea zaidi kwenye makala ijayo.

Lakini historia ilikuja kubadilika kwa kasi.

Israel ilipopata uhuru mwaka 1948, David Ben-Gurion alitangaza kuwa makundi yote ya kijeshi yaliyokuwa yakifanya kazi nje ya serikali yavunjwe na wapiganaji wake waingizwe katika jeshi jipya la taifa, Israel Defense Forces (IDF).

Lakini si kila mtu alikubaliana na uamuzi huo.
View attachment 3622583
Meli ya Altalena baada ya kushambuliwa na kombora la IDF.

Irgun lilikuwa limeagiza meli iliyoitwa Altalena kutoka Ulaya ikiwa imebeba silaha nyingi. Serikali mpya ya Israel iliona kuwa kundi hilo halikupaswa kuwa na jeshi lake wala silaha zake, kwa sababu hilo lingeweza kuhatarisha mamlaka ya dola mpya.

Mvutano huo uligeuka mapigano. IDF ilishambulia meli hiyo na zaidi ya watu 16 walifariki. Na mapigano yakaendelea katika fukwe hizo na kusababisha askari watatu wa IDF kuuwawa. Wakati huo, Menachem Begin aliwaamuru wafuasi wake wasijibu mashambulizi kwa nguvu zaidi ili kuepusha vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya Wayahudi.

Na hapa ndipo historia inapogeuka kwa namna ambayo wengi hawaitegemei.

Mtu ambaye aliwahi kuongoza kundi lililotajwa kuwa la kigaidi baadaye aliingia kwenye siasa. Mwaka 1973, Menachem Begin alishiriki kuijenga nguvu ya chama cha Likud. Mwaka 1977 akashinda uchaguzi mkuu na kuwa Waziri Mkuu wa Israel.

Mwaka uliofuata, 1978, Begin alipewa Tuzo ya Nobel ya Amani baada ya kusaini Camp David Accords na Rais wa Misri Anwar Sadat; makubaliano yaliyomaliza rasmi hali ya vita kati ya Israel na Misri.

Historia ina tabia ya kutukumbusha jambo moja muhimu: mara nyingi, mtu anayeitwa "gaidi" na upande mmoja wa historia anaweza kuja kuonekana kama "shujaa wa taifa" na upande mwingine.

Hii haimaanishi kwamba mauaji ya raia yanapaswa kuhalalishwa, wala haimaanishi kwamba makundi yote yanafanana. Badala yake, inatukumbusha umuhimu wa kuisoma historia yote, si ukurasa mmoja tu unaotufaa.
Nitarudi
 
Miaka ya 1960s mpaka 1980s, Tanzania ilitoa support kwa vyama vya kisiasa nchi za Kusini mwa Afrika, Frontline States
Vyama kama SWAPO (Namibia), ANC (South Afrika), ZANU PF (Zimbabwe), FRELIMO (Mozambique) vilipokea misaada ya mafunzo na silaha kutokea Tanzania
Vyama hivi huko kwao vilionekana ni vyama vya kigaidi kutoka kwa watawala wakoloni, Makaburu na England

Tanzania pia ilikuwa ni lauching pad ya Yoweri Museveni na chama chake wakati anaanza mapambano na serikali ya Uganda

Kwa tafsiri ya sasa ya ugaidi, Tanzania nayo ilikuwa nchi ya “kigaidi” kama Iran kwa kutoa support kwa Hamas na Hizbullah.

Mandela alienda US akiwa Rais wa South Afrika lakini kule bado kulikuwa na records kwamba ni “gaidi” na ilibidi kupata special clearance au waiver kuingia US

IRA na Sinn Fein ya Ireland pia ilikuwa designated kama chama cha kigaidi licha ya kutetea uhuru kutoka UK

Kwa context hiyo pia kuna Jomo Kenyatta, Fidel Castro, Che Guevara, Paul Kagame, Jonas Savimbi na John Garang wote kwa wakati mmoja waliwahi kuitwa magaidi na utawala wa nchi zao

One man’s terrorist is another man’s freedom fighter.
 
Back
Top Bottom