Tsh
JF-Expert Member
- Aug 26, 2021
- 17,022
- 36,936
Mkuu.Nalipa ada, nalisha familia najiendeleza kwa namna flani. Kilicho niumiza ni kujipoteza katika addiction hii, sija wahi kupata addiction yoyote katika maisha yangu hata pornography ilinipita!! This is the first addiction na pia mbaya zaidi losses za 1M nililkua naweza kuzi mudu na ndo maana nimeweza kufanya upuuzi kama huu.
Inaonekana mfumo wako wa utunzaji fedha ni wa personal account na mobile money, sasa Fungua account ambayo ukiweka fedha kutoa ni lazima utumie nguvu kidogo kama kuandika cheque na uende bank. Tena fungulia bank isiyo na mawakala kama BOA, MWANGAHAHIKABANK, EXIM, BARODA, EQUITY etc. Sababu akaunt unayotunza fedha inaurahisi sana wa kuivuta kuja kwenye simu na kuitumia katiba bet.
Hili likishindikana:
1-3m ni material enough hata kwa mtu mwenye uhakika wa kutengeneza kipato cha 10m each month, ongeza majukumu inaweza saidia kukufanya uone pesa uliyo nayo haitoshi na 1-3m ni kubwa sana kuipoteza.
Mfano wa jukumu:
Tafuta hata kijana asiyejiweza jiapize kumsomesha mpaka level fulani au tengeneza utaratibu wa kutoa ahadi ya mchango wa ujenzi wa madarasa, msikiti, kanisani, hospitali au vyovyote vile ilimradi uwe na jukumu litakalokufanya uone pesa unazotengeneza haitoshi na una uhitaji zaidi.