Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mrisho Gambo, amejibu mashambulizi yanayohusiana na wito ulioibuliwa na baadhi ya madiwani wa jiji la Arusha wakimuomba Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, kuchukua fomu ya kugombea ubunge wa jimbo hilo.
Gambo amesema kuwa yeye anatekeleza majukumu yake kama mbunge kwa ufanisi na kujivunia elimu yake, akisisitiza kuwa hakuna aliye na haki ya kumzuia kufanya kazi aliyopewa na wananchi.
Soma, Pia: Kumekucha: Madiwani Arusha waomba Paul Makonda agombee Ubunge jimbo la Arusha Mjini
"Tofauti kati ya mtu aliyeenda shule na mtu ambaye shule yake ni ya mashaka ipo wazi," alisema akisisitiza kuwa ni muhimu kwa kiongozi kuwa na elimu ya kweli ili kuhakikisha kuwa anatekeleza majukumu yake ipasavyo na kusisitiza kuwa
"Ni lazima ifike mahali uoneshe tofauti ya mtu ambaye amekwenda shule na mtu ambaye shule yake ni ya kubabaisha au ni ya mashaka. Kwa sisi ambao tuna uhakika na shule zetu, kila jambo linapotokea tunahitaji kutafakari na kufikiria na kuangalia athari ya kila kinachofanyika," aliongeza.
Katika kujibu wito wa baadhi ya madiwani ambao walimuomba Makonda achukue fomu ya kugombea ubunge, Gambo amesema kuwa hakuna mtu anayekatazwa kugombea ubunge, lakini akasisitiza kuwa mbunge anachaguliwa na wananchi na sio madiwani.
"Kama mtu ana ndoto ya kuwa mbunge, aache njia za mkato. Asubiri utaratibu na aje kwenye uchaguzi, aone kama ngoma ya kitoto inakesha," alisema kwa kujiamini.
Gambo amebainisha u pia shutuma za kwamba watu wanajaribu kutumia mamlaka zao kuingilia mchakato wa uchaguzi na kutaka kumchafua.
"Kuna watu wanaona kazi inakwenda na wananchi wanatukubali, wanataka kutumia mamlaka yao kutuchafua na kuleta ajenda zisizo na msingi.
Mbunge huyo pia amekosoa vikali hali ya baadhi ya wanasiasa kutoa machozi kwa sababu ya kushindwa kupata fedha walizokuwa wakitarajia kutumika kinyume na utaratibu.
"Kama kuna mtu analia kwa kupoteza fedha alizokuwa akitarajia, machozi hayo ni ya halali kwa sababu walijua wazi kuwa wangezitumia kwa manufaa yao binafsi," aliongeza.
Kwa kumalizia, Gambo amekumbusha kuwa yeye ni mbunge anayetekeleza majukumu yake kwa manufaa ya wananchi wa Arusha Mjini, na hakutakuwa na mtu yeyote atakayemzuia kufanya hivyo kwa kufuata utaratibu.