Pre GE2025 Gambo ajibu mapigo ya Makonda "mimi nimeenda shule"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mrisho Gambo, amejibu mashambulizi yanayohusiana na wito ulioibuliwa na baadhi ya madiwani wa jiji la Arusha wakimuomba Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, kuchukua fomu ya kugombea ubunge wa jimbo hilo.

Gambo amesema kuwa yeye anatekeleza majukumu yake kama mbunge kwa ufanisi na kujivunia elimu yake, akisisitiza kuwa hakuna aliye na haki ya kumzuia kufanya kazi aliyopewa na wananchi.

Soma, Pia: Kumekucha: Madiwani Arusha waomba Paul Makonda agombee Ubunge jimbo la Arusha Mjini

"Tofauti kati ya mtu aliyeenda shule na mtu ambaye shule yake ni ya mashaka ipo wazi," alisema akisisitiza kuwa ni muhimu kwa kiongozi kuwa na elimu ya kweli ili kuhakikisha kuwa anatekeleza majukumu yake ipasavyo na kusisitiza kuwa

"Ni lazima ifike mahali uoneshe tofauti ya mtu ambaye amekwenda shule na mtu ambaye shule yake ni ya kubabaisha au ni ya mashaka. Kwa sisi ambao tuna uhakika na shule zetu, kila jambo linapotokea tunahitaji kutafakari na kufikiria na kuangalia athari ya kila kinachofanyika," aliongeza.

Katika kujibu wito wa baadhi ya madiwani ambao walimuomba Makonda achukue fomu ya kugombea ubunge, Gambo amesema kuwa hakuna mtu anayekatazwa kugombea ubunge, lakini akasisitiza kuwa mbunge anachaguliwa na wananchi na sio madiwani.

"Kama mtu ana ndoto ya kuwa mbunge, aache njia za mkato. Asubiri utaratibu na aje kwenye uchaguzi, aone kama ngoma ya kitoto inakesha," alisema kwa kujiamini.

Gambo amebainisha u pia shutuma za kwamba watu wanajaribu kutumia mamlaka zao kuingilia mchakato wa uchaguzi na kutaka kumchafua.

"Kuna watu wanaona kazi inakwenda na wananchi wanatukubali, wanataka kutumia mamlaka yao kutuchafua na kuleta ajenda zisizo na msingi.

Mbunge huyo pia amekosoa vikali hali ya baadhi ya wanasiasa kutoa machozi kwa sababu ya kushindwa kupata fedha walizokuwa wakitarajia kutumika kinyume na utaratibu.

"Kama kuna mtu analia kwa kupoteza fedha alizokuwa akitarajia, machozi hayo ni ya halali kwa sababu walijua wazi kuwa wangezitumia kwa manufaa yao binafsi," aliongeza.

Kwa kumalizia, Gambo amekumbusha kuwa yeye ni mbunge anayetekeleza majukumu yake kwa manufaa ya wananchi wa Arusha Mjini, na hakutakuwa na mtu yeyote atakayemzuia kufanya hivyo kwa kufuata utaratibu.
View attachment 3249376
1740500610397.png
 
Kwa mtazamo wangu, ukiwa msomi wala huna haja ya kujitangaza bali matendo yako yatawaonyesha watu kuwa wewe ni msomi!! Kwa majibu ya namna hii na kujigamba kwingi, hapo shule hamna! Zaidi anaendeshwa na mihemuko!!!
Kwa hiyo anatapatapa tu muheshimiwa Gambo
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Mabosi wake wote wamekwenda shule (Wananchi ambao ni wenyenchi) Kuna comment nyingine zinaonyesha ni vipi kichwani hazimo..., Badala ya hayo maneno angetumia huo muda kuelezea ni vipi ataendelea kuwatumia mabosi wake na sio kuleta mipasho...

Mbaya zaidi watu ndio wanapenda hizi drama badala ya issues....
 
hii kauli ya shule ya mashaka anataka kusema mwakilishi wa raisi nashule ya mashaka?
 
Haya maigizo ya "nimeombwa na wananchi, madiwani,viongozi wa dini" ni maigizo ya kiwango cha uchekeshaji.
Ngoja nami nitoke hapa Rufiji kwenye msiba wa Mzee Mchengerwa then natafuta madiwani 12 na kuhakikisha account ya kila mmoja wao inasoma 5 milioni,kesho utaona wamejitokeza kuongea na waandishi wa habari kuniomba sana nipitishwe kugombea ubunge bila kupingwa.

Uchawa ni tatizo kubwa sana kuliko tunavyoliona hadharani.
🤣 🤣 🤣 🔊
 
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mrisho Gambo, amejibu mashambulizi yanayohusiana na wito ulioibuliwa na baadhi ya madiwani wa jiji la Arusha wakimuomba Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, kuchukua fomu ya kugombea ubunge wa jimbo hilo.

Gambo amesema kuwa yeye anatekeleza majukumu yake kama mbunge kwa ufanisi na kujivunia elimu yake, akisisitiza kuwa hakuna aliye na haki ya kumzuia kufanya kazi aliyopewa na wananchi.

Soma, Pia: Kumekucha: Madiwani Arusha waomba Paul Makonda agombee Ubunge jimbo la Arusha Mjini

"Tofauti kati ya mtu aliyeenda shule na mtu ambaye shule yake ni ya mashaka ipo wazi," alisema akisisitiza kuwa ni muhimu kwa kiongozi kuwa na elimu ya kweli ili kuhakikisha kuwa anatekeleza majukumu yake ipasavyo na kusisitiza kuwa

"Ni lazima ifike mahali uoneshe tofauti ya mtu ambaye amekwenda shule na mtu ambaye shule yake ni ya kubabaisha au ni ya mashaka. Kwa sisi ambao tuna uhakika na shule zetu, kila jambo linapotokea tunahitaji kutafakari na kufikiria na kuangalia athari ya kila kinachofanyika," aliongeza.

Katika kujibu wito wa baadhi ya madiwani ambao walimuomba Makonda achukue fomu ya kugombea ubunge, Gambo amesema kuwa hakuna mtu anayekatazwa kugombea ubunge, lakini akasisitiza kuwa mbunge anachaguliwa na wananchi na sio madiwani.

"Kama mtu ana ndoto ya kuwa mbunge, aache njia za mkato. Asubiri utaratibu na aje kwenye uchaguzi, aone kama ngoma ya kitoto inakesha," alisema kwa kujiamini.

Gambo amebainisha u pia shutuma za kwamba watu wanajaribu kutumia mamlaka zao kuingilia mchakato wa uchaguzi na kutaka kumchafua.

"Kuna watu wanaona kazi inakwenda na wananchi wanatukubali, wanataka kutumia mamlaka yao kutuchafua na kuleta ajenda zisizo na msingi.

Mbunge huyo pia amekosoa vikali hali ya baadhi ya wanasiasa kutoa machozi kwa sababu ya kushindwa kupata fedha walizokuwa wakitarajia kutumika kinyume na utaratibu.

"Kama kuna mtu analia kwa kupoteza fedha alizokuwa akitarajia, machozi hayo ni ya halali kwa sababu walijua wazi kuwa wangezitumia kwa manufaa yao binafsi," aliongeza.

Kwa kumalizia, Gambo amekumbusha kuwa yeye ni mbunge anayetekeleza majukumu yake kwa manufaa ya wananchi wa Arusha Mjini, na hakutakuwa na mtu yeyote atakayemzuia kufanya hivyo kwa kufuata utaratibu.
View attachment 3249376
kwa bahati mbaya, bashite sio tu amenunua machawa wengi madiwani, amenunua hadi viongozi wa dini, na atadondokea pua kama alivyodondokea kwa ndungulile, isipokuwa kwa sasa aliyepo madarakani hana sauti kwake pengine tusemeje sasa? ila kuanzia ubongo hana (elimu) na anachojua ni kutafuta sifa tu sio kufanya jambo lenye matunda.
 
Makonda kama unataka ubunge, njoo ugombee jimbo la Kibamba, huku mbunge ni kama picha tu hakuna alichopambania wananchi.
 
Wote ni viazi tu, huyo aloenda shule angekaa tu kimya afanye kazi then waje washindane kwenye sanduku la kura, otherwise naona wanapiga tu taarabu. Maendeleo ni ya wananchi, wote kazi yao ni kuwatumikia wananchi wa Arusha, sasa wanachogombea nini?! Hii nchi hii kupata maendeleo tutasubiri sana maana viongozi wanapenda sana kutukuzwa na kuabudiwa, mko sehemu moja kama viongozi afu mnaanza kugombana na kuoneshana umwamba, hicho ndicho wananchi na serikali imewatuma?!
 
Nje ya mada basi Leo nimepita mahali kuna jamaa nimemkuta kamfumania mkewe
Nikasikia jamaa anasema kwa Sauti

"Yani wewe mwanamke nimekuvumilia na hilo pua lako kubwa Kama pumbu za mtoto mdogo afu bado unanisaliti"[emoji1787]watu pale wote Hoi vicheko" [emoji119]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom