Pre GE2025 Gambo ajibu mapigo ya Makonda "mimi nimeenda shule"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mrisho Gambo, amejibu mashambulizi yanayohusiana na wito ulioibuliwa na baadhi ya madiwani wa jiji la Arusha wakimuomba Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, kuchukua fomu ya kugombea ubunge wa jimbo hilo.

Gambo amesema kuwa yeye anatekeleza majukumu yake kama mbunge kwa ufanisi na kujivunia elimu yake, akisisitiza kuwa hakuna aliye na haki ya kumzuia kufanya kazi aliyopewa na wananchi.

Soma, Pia: Kumekucha: Madiwani Arusha waomba Paul Makonda agombee Ubunge jimbo la Arusha Mjini

"Tofauti kati ya mtu aliyeenda shule na mtu ambaye shule yake ni ya mashaka ipo wazi," alisema akisisitiza kuwa ni muhimu kwa kiongozi kuwa na elimu ya kweli ili kuhakikisha kuwa anatekeleza majukumu yake ipasavyo na kusisitiza kuwa

"Ni lazima ifike mahali uoneshe tofauti ya mtu ambaye amekwenda shule na mtu ambaye shule yake ni ya kubabaisha au ni ya mashaka. Kwa sisi ambao tuna uhakika na shule zetu, kila jambo linapotokea tunahitaji kutafakari na kufikiria na kuangalia athari ya kila kinachofanyika," aliongeza.

Katika kujibu wito wa baadhi ya madiwani ambao walimuomba Makonda achukue fomu ya kugombea ubunge, Gambo amesema kuwa hakuna mtu anayekatazwa kugombea ubunge, lakini akasisitiza kuwa mbunge anachaguliwa na wananchi na sio madiwani.

"Kama mtu ana ndoto ya kuwa mbunge, aache njia za mkato. Asubiri utaratibu na aje kwenye uchaguzi, aone kama ngoma ya kitoto inakesha," alisema kwa kujiamini.

Gambo amebainisha u pia shutuma za kwamba watu wanajaribu kutumia mamlaka zao kuingilia mchakato wa uchaguzi na kutaka kumchafua.

"Kuna watu wanaona kazi inakwenda na wananchi wanatukubali, wanataka kutumia mamlaka yao kutuchafua na kuleta ajenda zisizo na msingi.

Mbunge huyo pia amekosoa vikali hali ya baadhi ya wanasiasa kutoa machozi kwa sababu ya kushindwa kupata fedha walizokuwa wakitarajia kutumika kinyume na utaratibu.

"Kama kuna mtu analia kwa kupoteza fedha alizokuwa akitarajia, machozi hayo ni ya halali kwa sababu walijua wazi kuwa wangezitumia kwa manufaa yao binafsi," aliongeza.

Kwa kumalizia, Gambo amekumbusha kuwa yeye ni mbunge anayetekeleza majukumu yake kwa manufaa ya wananchi wa Arusha Mjini, na hakutakuwa na mtu yeyote atakayemzuia kufanya hivyo kwa kufuata utaratibu.
View attachment 3249376
Safi sana ,vilaza wote ni kupiga spana tuu 😂😂
 
Daudi Albert Bashite
Bashite amebahatika kuwa na mdomo mkubwa lakini ubongo kisoda. Ukiona mtu anapata division 0 form 4, jua huyo kichwani hakuna kitu kabisa.

Bashite anahangaika sana kuliziba pengo la ubongo kwa kelele na maigizo mengi sana.
 
Haya maigizo ya "nimeombwa na wananchi, madiwani,viongozi wa dini" ni maigizo ya kiwango cha uchekeshaji.
Ngoja nami nitoke hapa Rufiji kwenye msiba wa Mzee Mchengerwa then natafuta madiwani 12 na kuhakikisha account ya kila mmoja wao inasoma 5 milioni,kesho utaona wamejitokeza kuongea na waandishi wa habari kuniomba sana nipitishwe kugombea ubunge bila kupingwa.

Uchawa ni tatizo kubwa sana kuliko tunavyoliona hadharani.
Rais angefukuza huyo RC ameenda kuleta mtafaeuku badala ya Maendeleo.

Amejaza machawa wanaojifanya eti wanamlilia 😂😂
 
Shule siyo hoja kwenye ubunge, hata kwenye darasa la 7 anaruhusiwa kwahiyo kama madiwani hawakutani shule yako siyo hoja, itakusaidia kufanya biashara zingine
 
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mrisho Gambo, amejibu mashambulizi yanayohusiana na wito ulioibuliwa na baadhi ya madiwani wa jiji la Arusha wakimuomba Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, kuchukua fomu ya kugombea ubunge wa jimbo hilo.

Gambo amesema kuwa yeye anatekeleza majukumu yake kama mbunge kwa ufanisi na kujivunia elimu yake, akisisitiza kuwa hakuna aliye na haki ya kumzuia kufanya kazi aliyopewa na wananchi.

Soma, Pia: Kumekucha: Madiwani Arusha waomba Paul Makonda agombee Ubunge jimbo la Arusha Mjini

"Tofauti kati ya mtu aliyeenda shule na mtu ambaye shule yake ni ya mashaka ipo wazi," alisema akisisitiza kuwa ni muhimu kwa kiongozi kuwa na elimu ya kweli ili kuhakikisha kuwa anatekeleza majukumu yake ipasavyo na kusisitiza kuwa

"Ni lazima ifike mahali uoneshe tofauti ya mtu ambaye amekwenda shule na mtu ambaye shule yake ni ya kubabaisha au ni ya mashaka. Kwa sisi ambao tuna uhakika na shule zetu, kila jambo linapotokea tunahitaji kutafakari na kufikiria na kuangalia athari ya kila kinachofanyika," aliongeza.

Katika kujibu wito wa baadhi ya madiwani ambao walimuomba Makonda achukue fomu ya kugombea ubunge, Gambo amesema kuwa hakuna mtu anayekatazwa kugombea ubunge, lakini akasisitiza kuwa mbunge anachaguliwa na wananchi na sio madiwani.

"Kama mtu ana ndoto ya kuwa mbunge, aache njia za mkato. Asubiri utaratibu na aje kwenye uchaguzi, aone kama ngoma ya kitoto inakesha," alisema kwa kujiamini.

Gambo amebainisha u pia shutuma za kwamba watu wanajaribu kutumia mamlaka zao kuingilia mchakato wa uchaguzi na kutaka kumchafua.

"Kuna watu wanaona kazi inakwenda na wananchi wanatukubali, wanataka kutumia mamlaka yao kutuchafua na kuleta ajenda zisizo na msingi.

Mbunge huyo pia amekosoa vikali hali ya baadhi ya wanasiasa kutoa machozi kwa sababu ya kushindwa kupata fedha walizokuwa wakitarajia kutumika kinyume na utaratibu.

"Kama kuna mtu analia kwa kupoteza fedha alizokuwa akitarajia, machozi hayo ni ya halali kwa sababu walijua wazi kuwa wangezitumia kwa manufaa yao binafsi," aliongeza.

Kwa kumalizia, Gambo amekumbusha kuwa yeye ni mbunge anayetekeleza majukumu yake kwa manufaa ya wananchi wa Arusha Mjini, na hakutakuwa na mtu yeyote atakayemzuia kufanya hivyo kwa kufuata utaratibu.
View attachment 3249376
Kwanza ya hayo wajiulize hao madiwani walichaguliwa kihalali au ndio ule michongo ya 2020?
Pesa mnakula hamna linaloonekana kwa wananchi majoho bila utendaji.!
Gambo yuko sawa!
 
Shule siyo hoja kwenye ubunge, hata kwenye darasa la 7 anaruhusiwa kwahiyo kama madiwani hawakutani shule yako siyo hoja, itakusaidia kufanya biashara zingine
Na ndio maana tunawaBunge wa hovyo humo bungeni hawana mchango wala msaada kwa wananchi!.
 
Amejaza machawa wanaojifanya eti wanamlilia 😂😂
🤣🤣🤣

Mbona hizo ndio huwa ni mbinu za ma-ccm.Hata samia amejaza machawa wanaojifanya wana bubujikwa na machozi. Akina tlaatlaaa, lukas mwashambwa na choice variable wote ni machawa wa samia ambao huwa wanabubujikwa na machozi.
 
Bora Samia ni Rais,Sasa huyo RC ameenda kuvamia Jimbo na anatumia nafasi ya Serikali vibaya 😂😂
 
Rais angefukuza huyo RC ameenda kuleta mtafaeuku badala ya Maendeleo.

Amejaza machawa wanaojifanya eti wanamlilia 😂😂
Utangoja sana Gambo.Sasa ndio mmejipalia mkaa.Chama hakikutaki wala huna support ya wananchi.Hutapita kwenye mchujo na pumba na kuropoka kwako kunazidi kukuharibia.
 
Halafu utasikia kule bungeni hamna kitu tunachopata,jinga sana
 
Utangoja sana Gambo.Sasa ndio mmejipalia mkaa.Chama hakikutaki wala huna support ya wananchi.Hutapita kwenye mchujo na pumba na kuropoka kwako kunazidi kukuharibia.
Kwa hiyo Mimi ni Gambo 😂😂😂😂

Anaeamua mchujo ni Rais na si vinginevyo.

Kimsingi Bashite ni brainless ni mbulula tuu ndio wanamsapoti.

Mwisho Gambo ni Tiss sio lazima awe Mbunge.
 
Na ndio maana tunawaBunge wa hovyo humo bungeni hawana mchango wala msaada kwa wananchi!.
Wabunge wa darasa la 7 ndo wanajenga hoja bungeni zinazokua related na maisha halisi ya mtanzania, kina msukuma na kishimbe hao wasomi ndo wamejaa uchawa
 
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mrisho Gambo, amejibu mashambulizi yanayohusiana na wito ulioibuliwa na baadhi ya madiwani wa jiji la Arusha wakimuomba Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, kuchukua fomu ya kugombea ubunge wa jimbo hilo.

Gambo amesema kuwa yeye anatekeleza majukumu yake kama mbunge kwa ufanisi na kujivunia elimu yake, akisisitiza kuwa hakuna aliye na haki ya kumzuia kufanya kazi aliyopewa na wananchi.

Soma, Pia: Kumekucha: Madiwani Arusha waomba Paul Makonda agombee Ubunge jimbo la Arusha Mjini

"Tofauti kati ya mtu aliyeenda shule na mtu ambaye shule yake ni ya mashaka ipo wazi," alisema akisisitiza kuwa ni muhimu kwa kiongozi kuwa na elimu ya kweli ili kuhakikisha kuwa anatekeleza majukumu yake ipasavyo na kusisitiza kuwa

"Ni lazima ifike mahali uoneshe tofauti ya mtu ambaye amekwenda shule na mtu ambaye shule yake ni ya kubabaisha au ni ya mashaka. Kwa sisi ambao tuna uhakika na shule zetu, kila jambo linapotokea tunahitaji kutafakari na kufikiria na kuangalia athari ya kila kinachofanyika," aliongeza.

Katika kujibu wito wa baadhi ya madiwani ambao walimuomba Makonda achukue fomu ya kugombea ubunge, Gambo amesema kuwa hakuna mtu anayekatazwa kugombea ubunge, lakini akasisitiza kuwa mbunge anachaguliwa na wananchi na sio madiwani.

"Kama mtu ana ndoto ya kuwa mbunge, aache njia za mkato. Asubiri utaratibu na aje kwenye uchaguzi, aone kama ngoma ya kitoto inakesha," alisema kwa kujiamini.

Gambo amebainisha u pia shutuma za kwamba watu wanajaribu kutumia mamlaka zao kuingilia mchakato wa uchaguzi na kutaka kumchafua.

"Kuna watu wanaona kazi inakwenda na wananchi wanatukubali, wanataka kutumia mamlaka yao kutuchafua na kuleta ajenda zisizo na msingi.

Mbunge huyo pia amekosoa vikali hali ya baadhi ya wanasiasa kutoa machozi kwa sababu ya kushindwa kupata fedha walizokuwa wakitarajia kutumika kinyume na utaratibu.

"Kama kuna mtu analia kwa kupoteza fedha alizokuwa akitarajia, machozi hayo ni ya halali kwa sababu walijua wazi kuwa wangezitumia kwa manufaa yao binafsi," aliongeza.

Kwa kumalizia, Gambo amekumbusha kuwa yeye ni mbunge anayetekeleza majukumu yake kwa manufaa ya wananchi wa Arusha Mjini, na hakutakuwa na mtu yeyote atakayemzuia kufanya hivyo kwa kufuata utaratibu.
View attachment 3249376
Hawaa machawa madiwani mkuu wasiwaumize kichwa kanwe YAAN wangejua ndioo wanamharibia rc kama kweli anayajuahaya

Binafsi NATAMANI Gambo asijibu maana mpaka sasa WABUNGE waneenda kinyume na Amri ya Chama kuhusu uchaguzi anyway
 
Back
Top Bottom