Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Gambo amuonya Mkuu wa wilaya mbele ya Makonda, asema ameshindwa kazi
Kuna kiongozi mmoja, alisema eti mambo hayaendi kwasababu ya mgogogro wa mbunge, Baraza la Madiwani na Wataalamu, haya mlioyaona kuna sehemu mbunge anaingia hapo? Mkuu wa Mkoa kwa kuridhika na kazi yako nimetulia naomba wasinikchokonoe wasinifatefate na watimize wajibu wao.
Mkuu wa Wilaya alitakiwa akwambie kwa nini kwake mambo hayaendi, asimsingizie mbunge mimi siyomtendaji wa serikali mimi ni mwakilishi wa wananchi, hiyo ni ishara kuwa ameshindwa kuwasimimamia wataalamu ndio maana mkuu wa mkoa leo unafanya kazi kwenye wilaya mambo yote anatakiwa yeye awe ameyamaliza.
Kwa hiyo naomba Mkuu wa wilaya mimi namuheshimu sana na nimejitahidi kumkwepa kwenye kazi zake kwa sababu nataka amani kwenye jimbo letu nataka maendeleo asinichokonoe kwa sababu sina mpango wa kugombana naye. na asinilazimishe kugombana naye.
Mkuu wa Mkoa nakuunga mkono kwenye kazi unayofanya ya kupambana na wezi kupambana na mafisadi, kazi ya kupambanan na wavivu tunaopata hasara ni sisi mimi na madiwani na wenyekiti wa serikali za mtaa na Maraisi mambo yasipokwenda haya tutakaopata hasara ni sisi tutawenda kuomba kura kwa wananchi.
Nilipokuwa nasema Arusha kuna wizi, Arusha ni shamba la bibi, Arusha mambo haaendi walikuwa wanasema gambo ni mbaya, sasa leo amekaja kiboko yao. Nami naungana na kabisa na wewe unaposimamia haki, unaposimamia ukweli utapigwa vita na majungu kwenye kila kona ya nchi, lakini wanaosimamia haki mlinzi wao huwa ni Mungu na wala siyo binadamu.
Pia soma: Mkuu wa Wilaa Arusha: Migogoro baina a Baraza, menejimenti na mbunge inadhoofisha utoaji huduma au miradi ya maendeleo kwa wananchi