Pre GE2025 Gambo: Mkuu wa Wilaya asinichokonoe, ameshindwa kuwasimamia Wataalamu, aache kumsingizia Mbunge

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
DC anatakiwa afahamu mkuu wa mkoa na mmbunge ni washikaji kitambo toka wanajitafuta wakiwa CCM.

Mmoja hapo alienda azima suit ya harusi kwa mwenzake wote wakiwa apeche alolo; majungu ya mmbunge kwa mkuu wa mkoa ni sawa kumchomea Mchengerwa kwa ‘bi-tozo’.

Imenikumbusha msanii mmoja marekani zama hizo kaenda kutafuta deal la label yake iwe chini ya Columbia Records amekutana na president anamwaga sera zake tunataka kuwa wakubwa kushinda So-So def records, kwanza Jermaine Dupri is overrated na kamsagia humo ndani.

Jamaa mkutano umeisha karudi kwa washakaji zake anawaadithia jinsi president alivyokuwa anamsikiliza kwa makini anadhani watapatq deal lao la label, washkaji zake wakamwambia huyo president Columbia records ‘Michael Mauldin’ ndio baba yake mzazi Jermaine Dupri kama umempondo hivyo mtoto wake sahau ilo deal.
 
Hapo kwenye kuchokonolewa tu.
 
Nimeipenda hii!, haswa hiyo ya kutaka kumchonganisha baba na mwana, kwa kuichonganisha record label ya baba na mwana, Columbia Records ya Michael Mauldin ambaye ni baba mtu, na Def Jam Records ya Jermaine Dupri ambaye ni mwanae!. Thanks for this, I didn't know this!.

Baada ya Makonda kuletwa Arusha, Lema, Gambo na Ole Sambaya, wanajitafakari sana kuhusu ubunge wa 2025!, kama Konda Boy aliachia mkoa wa Dar kugombea Ubunge, akidumu Arachuga hadi 2025, akaamua kutinga mjengoni kutokea Arusha, Lema, Gambo na Ole Sambaya hawana chao!.
P
 
Makonda na Gambo ni ndugu wa kufikia.

Gambo ndio alimuazima suti yake Makonda siku ya harusi yake.

Ndio maana kapewa mic hapo amsute DC mbele ya wananchi, wanajuana hao kitambo; walishawahi simulia historia yao wote wakiwa wakuu wa mikoa.
 
Naunga mkono hoja,Gambo amekuwa anafichua Ufisadi Arusha mara Kwa mara kuanzia Bungeni na kwingine lakini Serikali haichukui hatua.

Pale Arusha kulikuwa na syndicate ya Ufisadi kuanzia Halmashauri, Watumishi Hadi viongozi wa CCM.

Nakumbuka walimtenga Gambo ila Sasa ujio wa Makonda Gambo amefurahi sana ngoja awafyatue.
 
Nadhani ilikuwa ni story tuu, suti ya Gambo ni mwembamba haiwezi kumtosha Makonda ana kifua kipana!.
P
Sio Makonda huyu wa leo, ndoa yake Makonda kafanyia Arusha ghafla ghafla tu, ilibidi aende kwa Gambo zama hizo.

Kama ni story sawa Iła kuna siku waliwahi simulia walipotokea.

Nadhani ilikuwa kwenye mkutano wa Makonda dar akiongea na vijana dar au UVCCM akamwalika na Gumbo akiwa mkuu wa mkoa Arusha. Kwenye kuhamasisha wasikate tamaa na ndoto zao ndio wakakumbushia wao walipotokea.
 
Hii nchi imegeuka kuwa ya wasanii na wapenda maigizo.
Na hii ni toka juu hadi chini.
Kinachofanyika sasa hivi ni kuwekwa wazi ubovu wa serikali ya CCM na waweka wazi ni wanaccm wenyewe.
Wakati wapinzani walipokuwa wanasema ilionekana ni kelele na kuwa wanapinga kila kitu, sasa hao wanaounga mkono kila kitu ndio wanaoweka sasa uchafu wao wote hadharani
 
Huyo hata kipindi akiwa mkuu wa wilaya Uvinza alipandisha bei viwanja mpaka watu wa chini wameshindwabkununia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…