Gamondi Gamondi Gamondi nakuita mara tatu

Gamondi Gamondi Gamondi nakuita mara tatu

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
9,753
Reaction score
10,747
Juzi tu hapa Nkane , Mdathir , Sureboy , Farid Mussa , Moloko , Kibwana , Walikuwa ni wachezaji hatari sana hata kama walikuwa wanatokea Sub , ukianza kuhesabu magoal ya ushindi au perfomnce zao bora hapa hutoacha kukumbuka

Nkane aliipatia Yanga goli la kuwapa Taji la ASFC 2021/22 , baada ya ku-level Score board 3-3 kisha mikwaju ya penalty ikaamua , Bado Nkane aliendelea kupata nafasi kwenye Kikosi cha Nabi na alikuwa anafanya vyema sana

Mdathir , Aliwapatia Yanga goal la Kuongoza dhidi ya Tp Mazembe CAFCC , na lile goli lilichukua goli bora la group stage CAFCC , bado alikuwa na kiwango bora sana majuzi juzi

Sureboy , Master , Atakumbwa kwa kiwango kizuri alichokionesha kwenye mchezo wa kufuzu Group stage dhidi ya Club African , ugenini lakini mwamba ile match aliwaka sana na bado alikuwa ni mchezaji mzuri sana

Farid Musa 🙌 Baller anayecheza namba nyingi pale Yanga , Beki wa kushoto , Winger wa kushoto , Middle aliwahi kuwapatia points 3 mhimu Yanga dhidi ya Tp Mazembe ugenini

Moloko , Moja ya winger nzuri kabisa na hatari sana , aliwahi kuwafungia goal la pili Yanga kwenye mchezo dhidi ya Real Bamako kwa mkapa

Kibwana Shomary , Si kulia si kushoto kote kote mdogo wangu anakaba na anashambulia ni kweli kazini kwake kuna kazi ila naye ni mzuri matches dhidi ya Dodoma Jiji , matches dhidi ya Al Merrikh ushashinda tayari na umefuzu naye anastahili kucheza

Ukiifuatilia Yanga , ilikuwa ni team ambayo kila mchezaji alikuwa ni hatari kulingana na Sub aliyokuwa anafanyiwa , lakini Yanga ya sasa et hawapati nafasi kinachoendelea ni niniii ? team ya taifa itarudi kule kule tulipo toka hakuna wachezaji wapya watakao itwa maana kibwana sasa hawezi kuitwa maana sub kila match

Coach wa Yanga ajitathmini na pengine anaweza asifike X-mas au hata mwaka mpya , mwenendo wa Kikosi cha Yanga sasa unafanya Pacome aje achoke sana ,

Japo ni coach wenu siwapangii majukumu ila huyu coach atatuulia vipaji vya hawa madogo ni vyema akasepa mapema , utaniambia nini nikuelewe kwamba Farid Musa hana kiwango cha kumpokea Max dakika za jioni ?

Tatizo hili COACH CHOYOOO SANA , Yanga ya msimu huu inaweza kuwa ndiyo Yanga nzuri kuishuhudia

@saniti
 
Sijui nani anafadhili hii kampeni yenu ya kumkataa Gamond. Na ghafla tu imeibuka baada ya mechi za kimataifa dhidi ya Medeama ili kuivuruga Yanga.

Hakuna rotation inayofanyika katika mechi ngumu zinazohitaji matokeo.

Hao wakina Nkane, Kibwana, na Farid Mussa mtawaona taratibu kwenye mechi zisizo na presha. Kila kocha lazima awe na first eleven yake ambayo ndiyo anayoiamini kwenye mechi zake ngumu, unataka kocha ampange Farid Mussa dhidi ya Al Ahly una akili wewe?

Yanga ndio kwanza kacheza mechi tisa tu za ligi kuu kuna mechi 21 zimebakia utawaona hao wachezaji kwenye mechi zingine za ligi na mechi za Azam federation cup ila sio kuingizwa ghafla tu kwenye klabu bingwa acheni ujinga
 
Huyu kocha uwezo wake haufiki hata ¼ ya Nabi
Nabi kacheza mechi gani ya kimataifa bila uwepo wa Mayele? Mnalinganisha uwezo wa kocha anayetumia Musonda na Mzize vs kocha aliyemtumia Mayele anayegombea tuzo?

Kwani ni kipi kinachokosekana Yanga zaidi ya straika wa maana? Unataka Gamondi aingie akafunge mwenyewe? Mpira unaochezwa na Yanga kwasasa hata Yanga ya Nabi haikuwahi kuucheza soka hili lenye kasi. Kina muangusha hana straika mwenye uwezo kama Mayele, magoli yanafungwa zaidi na viungo ambao inawapasa wafanye kazi zaidi na akili nyingi.

Kama Yanga wangekuwa na straika wa maana leo hii wangekuwa na point 6. Yanga ya Gamond inapiga counter, ina miliki mpira ila wakina Mzize wanajigonga gonga tu, vigugumizi vingi, kujiposition hawajui halafu lawama apewe kocha kwa lipi?
 
Hata Chama, Miquissone, Phiri, Saido, Boko walikuwa wachezaji hatari mbona sasa hawaanzi?

Yanga haitoki kwenye reli na campaign yenu mfu!

5 Tena!
Kuna kitu kinapandikizwa kwa mashabiki wa Yanga, inatengenezwa mazingira ya kuonekana kocha ni tatizo ili mashabiki wa react ili kocha atimuliwe.

Huyu kocha japo ana miezi michache ila aina yake mpira ni mpira wa kisasa, kama mapungufu kadhaa yatafanyiwa kazi ikiwepo mshambuliaji wa maana, na mawinga wa maana na beki kule wa kazi kazi kama Yao Kwasi hakika itakuwa habari nyingine kwenye soka la Africa.
 
Yaani huyu kocha miyeyusho, hii kauka nikuvae itatuletea majeruhi. Hatusemi kwamba afanye heavy rotation ya wachezaji 6 na kuendelea, NO. Tunasema kwamba angalau new faces hata 3 kila mechi zionekane na sub afanye kwa wakati. Wachezaji hata kama ni wazuri, wanachoka wale. Sio machine.
 
Nimegundua wamekuja kivingine ili Gamondi atoke baada ya 🖐🏿.

Gamondi Ana mkataba wa Miaka 2 pale yanga na ukiisha ataongezewa , raisi wa yanga sio kipindi kile cha yanga asili na yanga kampuni , sasahivi klabu ipo ki professional zaidi.

Nyambafffff
 
Yaani huyu kocha miyeyusho, hii kauka nikuvae itatuletea majeruhi. Hatusemi kwamba afanye heavy rotation ya wachezaji 6 na kuendelea, NO. Tunasema kwamba angalau new faces hata 3 kila mechi zionekane na sub afanye kwa wakati. Wachezaji hata kama ni wazuri, wanachoka wale. Sio machine.
Unataka kocha aweke ghafla tu new faces kwenye mechi ngumu za klabu bingwa Unaujua mpira kweli wewe?
 
Sijui nani anafadhili hii kampeni yenu ya kumkataa Gamond. Na ghafla tu imeibuka baada ya mechi za kimataifa dhidi ya Medeama ili kuivuruga Yanga.

Hakuna rotation inayofanyika katika mechi ngumu zinazohitaji matokeo.

Hao wakina Nkane, Kibwana, na Farid Mussa mtawaona taratibu kwenye mechi zisizo na presha. Kila kocha lazima awe na first eleven yake ambayo ndiyo anayoiamini kwenye mechi zake ngumu, unataka kocha ampange Farid Mussa dhidi ya Al Ahly una akili wewe?

Yanga ndio kwanza kacheza mechi tisa tu za ligi kuu kuna mechi 21 zimebakia utawaona hao wachezaji kwenye mechi zingine za ligi na mechi za Azam federation cup ila sio kuingizwa ghafla tu kwenye klabu bingwa acheni ujinga
Pamoja na yote ukweli usemwe kocha uwezo wake mdogo, anashindwa kuwatumia wachezaji effectively, hana rotation ya wachezaji zaidi ya aliowakuta kwenye video, hana mbinu mbadala kama nabi n.k.
 
Yaani huyu kocha miyeyusho, hii kauka nikuvae itatuletea majeruhi. Hatusemi kwamba afanye heavy rotation ya wachezaji 6 na kuendelea, NO. Tunasema kwamba angalau new faces hata 3 kila mechi zionekane na sub afanye kwa wakati. Wachezaji hata kama ni wazuri, wanachoka wale. Sio machine.
Una cheti gani cha ukufunzi wa kandanda!?
 
Pamoja na yote ukweli usemwe kocha uwezo wake mdogo, anashindwa kuwatumia wachezaji effectively, hana rotation ya wachezaji zaidi ya aliowakuta kwenye video, hana mbinu mbadala kama nabi n.k.
Unataka amfanyie nani rotation!?
 
Pamoja na yote ukweli usemwe kocha uwezo wake mdogo, anashindwa kuwatumia wachezaji effectively, hana rotation ya wachezaji zaidi ya aliowakuta kwenye video, hana mbinu mbadala kama nabi n.k.
Zile mechi nne za mwanzo kabla ya mechi ya Ihefu ya tarehe 4 mwezi wa 10 kocha alikuwa ni nani tofauti na huyu Gamondi? Huyu kocha si alitumia wachezaji wote kasoro Mshery pekee ndipo kaja kupoteza kwa Ihefu kwa kuwapanga wakina Sureboy? Sasa kama kikosi tu cha pili kinashindwa kumfunga timu ndogo ya Ihefu inayoburuza mkia je utasema wachezaji wa Yanga wana ubaora sawa?

Hakuna ukweli wowote zaidi ya kuwa mashabiki msiojua mpira.
Fact ni kwamba baada ya mechi dhidi ya Ihefu, ikafuatia mchezo dhidi ya Geita away na kocha baada ya kupata funzo ikamlazimu atafute alama tatu kwa kupanga kikosi chake kamili ( first eleven)
Baada ya hiyo mechi Ya Geita, mechi zote zilizofuata ilikuwa ni mechi ngumu kwa Yanga. Wakacheza dhidi ya Azam, Singida, Simba, Coastal. Hizo mechi zote kocha alihitaji alama 12 pamoja na ugumu wake. Kisha akatoka hapo akahamia kwenye klabu bingwa, je mlitaka a risk kwenye mechi ngumu awapumzishe watu ili mradi tu wengine wapate nafasi ya kucheza?

Unaweza kunitajia kocha yupi duniani anayefanya rotation ya first eleven yake kwenye mechi ngumu anayohitaji matokeo? Huyo Pep Gurdiola, Ancelot, n.k wenyewe wana first eleven yao ambayo panga pangua kwenye mechi ngumu lazima wawepo, makocha hufanya rotation kwa mechi wanazoona ni nyepesi hazina presha.

Yaani Yanga ndio kwanza imecheza michezo tisa tu ya ligi kuu bado mechi 21 za ligi kuu, bado mechi za michuano ya Azam federation, lakini unakuja kubwabwaja hapa wachezaji hawatumiki, mnafikiria kwa kutumia nini au mpira hamjui?

Hizo mbinu mnazongumzia za Nabi zilikuwa zinafanya kazi kutokana na uwepo wa mshambuliaji mahiri Mayele, michuano ya kimataifa inahitaji mtu anayepata nafasi moja na kuitumia, na wala sio wakina Musonda na Mzize wanaopata mipira ya counter hawajui wafanye nini zaidi ya kujigonga gonga tu.
 
Back
Top Bottom