KERO Garage bubu zimekuwa kero Ilala, mamlaka zinatakiwa kushughulikia hili

KERO Garage bubu zimekuwa kero Ilala, mamlaka zinatakiwa kushughulikia hili

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Nimezaliwa mwaka 1997, na Ilala ilikuwa sehemu nzuri sana kwa watoto kuishi na kukua kwa sababu ilikuwa karibu na maeneo mengi ya kucheza, huku miundombinu ikiwa tayari imefika maeneo hayo.

Hata hivyo, baada ya zile kota za pale Karume kuvunjwa na kujengwa Uwanja wa Karume wa mpira, pamoja na ujio wa Machinga Complex, kumekuwa na wimbi la mafundi gereji wengi kuanzisha shughuli mitaani, katika maeneo ambayo watu wanaishi na familia.

Watoto wadogo wanashindwa kucheza nje kwa sababu maeneo yao yamekuwa yakimilikiwa na gereji bubu zinazofika hadi mlangoni kwako. Ukisema utoke nyumbani uende kazini, unaweza kunasa hata lisaa limoja kwa sababu fundi ameshusha engine mlangoni kwako.

Ningependa serikali za mitaa zichukue hatua kuhusu suala hili. La sivyo, watoto wetu wataharibika, kama hawajaharibika tayari. Mungu awanusuru, maana mipango ya kuziondoa hizi gereji ilikuwepo, lakini kila mwaka haitimii.
 
waache watu wajitafutie vipato vyao mkuu, unataka watu waachie ufundi waingie kwenye uwizi?
 
Nchi imekuwa ya ajabu sana. Pale Gerezani kuna shule ya sekondari nafikiri inaitwa Dar sec nje ya shule kwenye pavements kuna garage bubu hata pa kutembea wameziba na magari mabovu.
 
Acha vijana watafute ridhiki. Mkiwakataza watatukaba tukiwa tunasaka spare used mkiwatoa watafutieni eneo hata pale Jangwani
 
Hapo ujue Ilala imeshakua sio sehemu ya kuishi na familia tena
 
Back
Top Bottom