Gardner adaiwa kumpandisha Jide kortini

Gardner adaiwa kumpandisha Jide kortini

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
18,037
Reaction score
33,681

Mke wa Gardner G Habash, Judith Wambura Mbibo, ‘Lady Jaydee' akipozi.


Prizenta aliyetua Radio E-FM hivi karibuni akitokea Radio Times FM, Gardner G Habash ‘Kapteini' anadaiwa kumpandisha kortini mkewe, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee' kisa kikisemekana ni mgawanyo wa mali hivyo anataka haki yake baada ya kuwepo kwa madai mazito ya ndoa yao kuvunjika.Kwa mujibu wa madai hayo, inasemekana kwamba Gardner amekimbilia mahakamani akidai apewe talaka na waweze kugawana mali walizochuma wote ili kila mmoja achukue hamsini zake.

Chanzo hicho ambacho ni mtu wa karibu wa familia hiyo kililiambia gazeti hili kwamba, siku chache baada ya kutengana na huku hali ikizidi kuwa mbaya, mtangazaji huyo alichukua hatua ya kutafuta msaada kwa wanasheria.
"Msinitaje jina ila ninachowaambia ni kwamba Gardner tayari ameshampata mwanasheria anataka kumshitaki Jaydee.

"Anachohitaji ni kugawana mali zao, kila mtu afanye maisha yake na ukiangalia tu Gardner hana mpango tena wa kuendelea na maisha ya ndoa na Jaydee ila Jide yeye bado ana matumaini ya kurudiana wawe pamoja na hasa kinachomuuma ni kugawana mali.

"Yaani Gardner ameshafanya kila aina ya jitihada ya kutaka waachane kiroho safi lakini Jaydee anaonekana kutokubaliana na wazo hilo kwani anaogopa ule usemi kwamba mwanamke mjinga huvunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe," kilisema chanzo hicho na kuongeza:"Ishu ya kugawana mali ya Gardner na Jide ndiyo habari ya mjini na ili jamaa apate chake ameona heri atafute mkono wa sheria."

Chanzo hicho kiliendelea kumwaga ‘ubuyu' kwamba, kitendo cha Jaydee kutangaza kubadili mwelekeo wa mali zake akianza kwa kubadili jina la ule mgahawa wake kutoka lile la Nyumbani Lounge na kuuita M.O.G ndicho kimemshtua Gardner na watu wake wa karibu.

Kilendelea kudai kwamba, pia ishu ya Jaydee kubadili jina la Bendi ya Machozi na kuiita Lady Jaydee and the Band, nayo imemchochea Gardner na kuamua kukimbilia mahakamani. Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, gazeti hili lilimtafuta Gardner ili aweke wazi madai ya kutaka kumburuza mahakamani mkewe huyo na haya ndiyo majibu yake mafupi: "Kaka kusema kweli hiyo ishu nashindwa kuizungumzia maana hata sijui wewe umeipata wapi dah."

Gardner na Jaydee ambao walifunga ndoa mwaka 2005, wamekuwa wakidaiwa kuwa hawapo pamoja tena huku majukumu ya mtangazaji huyo ambaye alikuwa meneja wa mwanamuziki huyo yakichukuliwa na ndugu wa Jide ambaye ni msanii wa Bongo Fleva aitwaye Wakazi.


Chanzo: GPL


 
hatariiii....!!!
ndo ubaya wa kutegemea mke
gadna ndo ujiju hvyoo
 
Waende kwa gwajima wakasuluhishe ndoa
 
Duuh kweli dunia inazunguruka zamani tulizoea kusikia wanawake ndio wanadai Talaka ila Fresh ndio fifite fifite inayoongelewa kwenye katiba mpya

Namuunga mkono G Habash kwa 100% hawa wanawake wanatuonea sana ni kichaa peke yake asiyejuwa mchango wa G Habash kwenye mali walizochuma ndani ya ndoa na hakuna kisingizio cha kutogawanywa mali maana hawana watoto, wangekuwa na watoto tungesema mali ni za watoto.

Cc Pasco si haki itendeke tu bali ionekane imetendeka.
 
Last edited by a moderator:
Hahahahahaaaaa!! Sipati Picha ingekuwa Gadna yuko mbele yako hata singi ungemsukuma nalo. Nimecheka sana.
Lakini mambo ya ndoa ndivyo yalivyo wangu yanapofikia hatua kama hiyo, kila upande unakuwa ukitaka kukomoa upande mwingine. Huwa halikwepeki hili.
Ova

Garder hataki kumkomoa Jide bali anastahili mgawanyo wa mali, Wanaume wengi huwa tunaona aibu kuflame kesi kama hizi lakini kwa umri nilioishi nimeona mengi na namuunga mkono Gardner licha ya kwamba mimi ni mshabiki wa Jide ila kwenye haki nasimama upande wa haki.
 
Mahakama ndio itajuwa mgawanyo wa haki, nampongeza sana Gardner wanaume tunaonewa sana tunakufa na tai shingoni huyu ameonesha njia.


Kwa level ya kudai talaka? Au hii ni chumvi ya mwandishi kunogesha habari yake?
 
Namuunga mkono G Habash kwa 100% hawa wanawake wanatuonea sana ni kichaa peke yake asiyejuwa mchango wa G Habash kwenye mali walizochuma ndani ya ndoa na hakuna kisingizio cha kutogawanywa mali maana hawana watoto, wangekuwa na watoto tungesema mali ni za watoto.

Cc Pasco si haki itendeke tu bali ionekane imetendeka.
You're very right, Gadner ana mchango mkubwa sana katika mafanikio ya Jide sema tu watu wanashindwa kuona! Gadner ni mtu wa watu... kwa maana ya networking! Ukaribu wake na akina Kusaga ulimsaidia sana na yeye kujisogeza karibu na watoa michongo hapa mjini!! Hizi networking za Gadner zimefanya mengi sana kwa Jide kuanzia redioni, Nyumbani Lounge hadi kwenye sponsorship za hapa na pale! Atakayekataa mchango wa Gadner ni yule tu ambae hafahamu biashara za hapa mjini zinaendaje... kwa msanii unaweza kuwa na kila kitu lakini usipokuwa na watu wenye network wa kuweza kukupa back up, then you're done!
 
Back
Top Bottom