Wanabodi,
Jee Roho za Waliokufa Zinaweza Kuwaita Walio Hai?.
Jibu ni yes, ndio maana kwa baadhi ya mila, wamama wajawazito hawaruhusiwi kwenda makaburini, ili waliolala wasije wakaviita vichanga, na matokeo yake vikaitika na kupata still born.
Kwenye mahusiano kuna kitu kinaitwa Soul Mates, na hii ndio subject matter ya uzi wangu huu.
Hitimisho.
Kwa vile kwa sisi binadamu wote hapa duniani tuko safari tuu, kuelekea kwenye makao ya milele na maisha ya milele, tusiwalilie waliotangulia na kuhuzunika saana kwa kuwakosa, tuhuzunike kibinaadamu, kwa kulia kwa kiasi tuu, kisha maisha ni lazima yaendelee, bali pia tujiangalie sisi wenyewe, kwa nafsi zetu, jee tumejiandaa kuitika wito wakati siku yetu na saa yetu ikitakapofika?.
Kesheni mkiomba kwa maana hamjui siku wala saa.
RIP Ephraim Kibonde na Ruge Mutahaba na wengine wote waliotangulia, nyinyi mbele sisi tuko nyuma yenu, sote sisi ni wa Kwake na Kwake tutarejea.
Paskali