TANZIA Gardner G Habash mtangazaji wa Clouds Media afariki dunia

TANZIA Gardner G Habash mtangazaji wa Clouds Media afariki dunia

Kuna siku kipindi kile ndiyo wame achana tuu kuna clip moja akiwa stejini akasema hiyo kauli kwamba eti ame mkojolesha sana JIDE.
Dah!! Nili mdharau sana aisee, nilimuona mtu wa ajabu. Watu mme achana achaneni kistaarabu siyo kutoleana siri.

All in all YAMEPITA NA KWA SASA APUMZIKE KWA AMANI.

Hakusema kama wewe unavosema

Alisema siwez bishana na Mtoto wa kike niliyekua namkojoza
 
mtu kama alimzalilisha mwenzake asemwe hata kama kafariki ili tunaobaki tujifunze. Sasa maneno gani hayo alikosea sana. Hii tabia ya mtu akifa wanampamba mimi huwa ninashangaa Sana unafikri ww binadamu Hawa wa kitanzania
Ni unafki tu , watanzania kwenye sekta ya unafki hatujambo , yaani tumekuwa wanafki kupitiliza mpka tukazalisha na cheo kabisa cha uchawa.
 
Ongeza nyama maelezo hayatoshi haya
Kila kitu ktk maisha ya Binadamu hupaswa kufanywa kwa kiasi, kiujumla ukizidisha au ukipunguza hugharimu matokeo hasi. In Human beings life everything is supposed to be done by average scale, the way you maximize or minimize it totally incurrs negative outcomes.

Ubinadamu ni kazi/Humanity is a work.
 
Tunaoijua vyema hiyo Ofisi yao na kinachowakumba hasa tokea wakiwa kule Kitega Uchumi wala hatushangazwi na Vifo vya hawa Watajwa wako watatu. Tujitahidi sana Kuutumia huu Umaarufu wetu vizuri na ikiwezekana Watu wajitahidi Kuukataa kwani una Athari zake nyingi sana.

Ngoja nitafute nyimbo za Wakongo hasa zile ambazo Gitaa la Solo limepigwa na Mwamba Dally Kimoko niburudike zangu.
Mkuu nashukuru Kwa busara zako

Mara zote umekuwa mshauri muhimu sana kwenye suala hilo Kwa Vijana na watu maarufu

Mimi pia Kwa kuwa umri wangu, ningekushauri uendelee kuplay safe huko Kwa ndugu yako Mu7

Mwambie bila yeye, yule mdudu aliyeimbwa na Captain John Komba asingeikia kwenye Vyumba vya Wazee wetu Mwaka 1987 🥲🙌
 
Mtangazaji Mahiri wa Clouds FM, Gadner G. Habash (50) amefariki Dunia Leo April 20, 2024.

Gadner maarufu kama ‘Captain’ aliejizolea Umaarufu Mkubwa kupitia Kipindi cha Jahazi, alikua amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Jijini Dar es Salaam kutokana na kusumbuliwa na Pressure (Shinikizo la Damu).

Wasafi Media Tunatoa Pole kwa Familia , Clouds Media Group , Ndugu Jamaa na Marafiki . Mungu ailaze Roho yake Mahali Pema Peponi Amein

Wasafi Media

View attachment 2968923

Pia soma
- Mtangazaji Captain G. Habash alazwa JKCI kwa tatizo la Shinikizo la Damu
Pole sana familia ya Nahodha G .Habash!
 
Mara kwanza kumuona Gardner ilikuwa miaka ya 90, alikuja Kahama Mining kwenye kampuni ya Tanzoro Diomond Drilling kama Accountant akitokea Mwanza ,akatukuta pale wazee wa drilling rigs.
Alikuwa kijana mtanashati checkibobu, aliletwa pale na mke wa mmiliki wa wa kampuni, alikuwa mcanada Mzee Georgre Graham.
Mara tunaona pilika zake na mke wa bosi zimezidi, kumbe tukaja kujua ni tokea zamani, yule mzee wa canada alikuwa analiwa hela tu na yule demu.
Yule demu alikuwa na mpango wake wa kuleta ndugu zake pale, basi hata hatukudumu, akatutengenezea gozi mpaka tukafukuzwa kazi, lakini nakumbuka Gadner ndio alikuwa mhasibu pale akatuandia cheki nzuri ya kama jiwe na upuuzi.
Ndio ikawa mwisho wa kumuona Gardner, mara nashangaa namuona kwenye TV na kumsikia redioni,
R.I.P
 
Ni unafki tu , watanzania kwenye sekta ya unafki hatujambo , yaani tumekuwa wanafki kupitiliza mpka tukazalisha na cheo kabisa cha uchawa.
sema mimi mkuu huwa unafiki siuwezi.
Kuna kipindi alifariki yule msanii wa SOUTH AFRICA Aka kama sikosei sasa washkaji wakawa wanampost RIP sijui gone too young na maneno mengi kibao Halafu post ya mbele anaweka memes ya kuchekesha. sasa nikawa nashangaa hivi mtu kweli kama amekugusa maisha yako unaweza kweli ukafanya huo upuuzi yaani unapost picha ya RIP Halafu hapo hapo tupo tunachat na anacheka ana furaha zote.

HUU NI UKWELI KAMA MTU AJAWAHI KUKUGUSA KATIKA MAISHA YAKO AU SI MTU WAKO WAKARIBU HUWEZI KUUMIA AKIFA HUU NI UKWELI LAKINI HUWA HATUTAKI KUONEKANA WANAFIKI TUNAPOST ILI MRADI NI TRENDI KWAMBA UONEKANE UMEPOST.
kuna msanii hakumpost Ruge kipindi alipofariki watu walimsema sana nikaona Tanzania kweli ni Laaana yaani anaamini ukipost ndio umeumia au ulikuwa unampenda sana
 
Back
Top Bottom